Serikali kujenga barabara nne za juu Dar es Salaam

kimpe

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
911
861
Dar es Salaam. Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara nne za juu ‘flyover’ katika jiji la Dar es Salaam ndani ya miaka mitatu na daraja la Kigamboni Juni mwakani, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli amesema.

Pia amesema Serikali imetenga Sh2 bilioni kununua kivuko cha mwendo kasi kitakachokuwa kikitoa huduma kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo na kukamilika kwa ujenzi wa barabara za pembezoni katika jiji hili.



Waziri Magufuli alisema hayo jana katika ziara ya kukagua ujenzi wa barabara za jiji zinazojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

“Tunajenga ‘flyover’ nne katika makutano ya Tazara, Ubungo, Gerezani na DIT (Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam) na ninaomba niwaahidi wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kwamba ndani ya miaka mitatu foleni itabaki kuwa historia,” alisema na kuongeza:

“Tumetenga Sh28 bilioni kujenga kilomita 76.9 za barabara za pembezoni au pete ambazo zikikamilika zitawezesha kupunguza foleni.”

Alisema daraja la Kigamboni limekamilika kwa asilimia 60 kwa gharama ya Sh214 bilioni, fedha kutoka Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF), Barabara ya Mwenge - Tegeta kwa Sh89 bilioni, Daraja la Tazara na Gerezani Sh100 bilioni.

‘Flyover’ Ubungo

Akizungumzia barabara hiyo ya juu ya Ubungo, Mkuu Idara ya Usanifu na Viwango wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Ebenezer Mollel alisema katika eneo la Ubungo kutakuwa na barabara za ngazi tatu ambazo zitakuwa katika mifumo isiyowezesha msongamano wa magari.

Mollel alisema barabara za mabasi yaendayo haraka (BRT) itaendelea kufanya kazi kama kawaida ikiongozwa na taa, huku magari yanayotoka barabara ya Sam Nujoma na Mandela, mfano Buguruni - Mwenge au Mwenge - Buguruni yatakuwa yakipita juu.

“Katika barabara ya kwanza magari kutoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Buguruni (Mandela) na Kimara (Morogoro) kwenda Mwenge (Sam Nujoma) yataongozwa na taa. Magari yanayotoka Buguruni kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatafuata mfumo wa taa,” alisema Mollel.

“Katika barabara ya pili magari yanayotoka mjini (Barabara ya Morogoro) kwenda Mwenge na Kimara kwenda Buguruni nayo yatatakiwa kuongozwa na taa na hii ‘Flyover Interchange’ haitakuwa na msongamano kwani kila gari litakuwa na njia yake na hakutakuwa na msongamano wowote.”

Alisema Serikali imekubaliana na Benki ya Dunia kufadhili mradi wa barabara hiyo itakayoondoa adha katika eneo la Ubungo Mataa.Meneja BRT, Barakael Mmari alisema barabara ya mradi huo awamu ya kwanza kutoka Kimara kwenda Kivukoni imekamilika lakini baadhi ya wananchi wameanza kuharibu miundombinu yake kama taa, alama na kuiba mifuniko ya majitaka.

“Tulitakiwa kuikabidhi barabara hii leo (jana) ili tubaki kumalizia vituo tu, lakini Mheshimiwa Waziri (Dk Magufuli) wananchi wameiba taa za barabarani pindi zinapogongwa na madereva wasiozingatia sheria,” alisema Mmari

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki aliwataka wananchi kulinda miundombinu ya barabara hizo ili iwanufaishe watu wengi zaidi.
Source:Mwananchi.
attachment.php
 

Attachments

  • barabara.jpg
    barabara.jpg
    11.5 KB · Views: 3,397
nafikiri kwa mchoro huo, taa ni kwa ajiri ya wale wanaopinda tu mf kimara to buguruni, town to mwenge, mwenge to kimara, buguruni to town. BRT hawatatumia taa.

ni plan nzuri hasa kwa kuzingatia eneo kuwa dogo
 
Good news, ila msiwe mnashangaa pia mkiona deni la Taifa likipaa,hizo zinazotoka mifuko ya hifadhi ya jamii sijui zitarudishwa lini ..
 
Sasa kukiwa na flyover let say Ubungo. Magari yaendayo mjini yatakwama magomeni na jangwani. Kwani yatakuja mengi kwa kasi kutoka ubungo lakini kuanzia manzese kuendelea miundombinu itabaki vile vile hivyo kusababisha foleni ya ajabu
 
Uongo usiokubalika kwanini hamkufanya sasa pamoja na mradi mabasi ya mwendokasi
 
Kwa Tanzania mipango mizuri tunayo ya kutosha, ila tatizo ni utekelezaji na wengi kuingia katika ukoo wa panya.
 
Kama hayo yote sawa Magufuli ataacha historia za kina Sokoine japo tayari anayo historia hiyo!

Sokoine kawacha historia ipi? mashimo barabarani? na hizo hizo barabara mbovu ndiyo zikamuuwa, nini zaidi?

Hivi mnapoandika huwa mnafikiria kabla?
 
Sokoine kawacha historia ipi? mashimo barabarani? na hizo hizo barabara mbovu ndiyo zikamuuwa, nini zaidi?

Hivi mnapoandika huwa mnafikiria kabla?
sokoine angekuwa muislamu ungemsifia kama mtume Muhhamad
 
hizo flyovers ziko wapi sasa, , ,watanzania wanazidi kudharaulika kwakuwa wanaonekana wanavichwa vya kuku kuendelea kuchagua ccm,migodi itaisha,wanyama wataisha,misitu watamaliza then trust me tanzania itakuja kuitwa taifa maskini zaidi duniani zaidi ya somali
 
Kuliko kujenga hizo barabara ni bora kuzipanua na kuweka lami feeder roads...
 
Back
Top Bottom