Serikali kuchunguza juu ya adhabu ya kufungiwa kwa Mwakinyo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
SERIKALI imesema kuna haja ya kufuatilia mwenendo wa mashtaka ili kubaini uhalali wa adhabu iliyotolewa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) ya kumfungia bondia Hassan Mwakinyo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) jijini Dar es Salaam.

“Sisi kama wizara tutakaa na BMT (Baraza la Michezo la Taifa), lakini tutakaa pia na TPBRC, ili kuweza kupata taarifa rasmi ya nini kimetokea na misingi ya hiyo adhabu, baada ya kupata taarifa hiyo ndipo tutashauriana na wahusika wote namna adhabu hiyo ilivyotolewa, uhalali wake kama adhabu hiyo ni sahihi ataitumikia, au kama kuna mushkeli kidogo tutakaa na kushauriana kuona tunafanyaje,” amesema waziri huyo.

Mnamo Oktoba 10, mwaka huu TPBRC ilitangaza kumfungia Mwakinyo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya Sh milioni moja kwa kile kilichoelezwa kuwa Septemba 29 mwaka huu, bondia huyo aligomea kupanda ulingoni katika pambano lililofahamika ‘The Return of Champ’ huku pambano lake likiwa ndio kuu.

NIPASHE
 
Tayari imeisha hiyo...!

Wenyewe wana muita Oddo... wapambanie ndg zako wa TA...!
 
Hii wizara nayo haina kazi, kila siku wachezaji wa mpira wanafungwa ,makocha, viongozi na hata washabiki wa mchezo huo.
Hizo adhabu za faini sasa ,mbona hawaikiki waliingilia kati?
 
Hongera sana Waziri kwa hatua hii muhimu, kwakuwa Tanzania inahimiza sana uwekezaji tutambue kwamba hata sanaa na michezo ni uwekezaji unaoweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi, hivyo tuwakuze wasanii wetu kwa kila hali na pia tuepukane na hivi vyama sijui mamlaka sijui kamisheni zinazoundwa na wala jasho la vijana wetu zisiwe kikwazo katika mafanikio ya sekta ya sanaa na michezo nchini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom