Serikali kuanzisha sarafu mpya ya mia tano

hii inaonyesha thamani ya shilingi ilivyo shuka leo hii sh500 ni ndogo sana hivyo mzunguko wake ni mkubwa ndio maana zinachakaa
 
Ndiyo Wakuu! Katika kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu,serikali kupitia gavana bank kuu ,Prof Ndulu inatarajia kuanzisha sarafu ya miatano .Amedai kuwa noti hizo zinachakaa sana kwa sababu mzunguko wake ni mkubwa. Je ule ubora uliokuwa unasemwa uko wapi wakati noti hizo zinatoka? Au ndo ni amini kuwa jamaa walisha kula cha kwao? Hivi ni lini serikali hii ita anzisha vitu endelevu? Tunahitaji tafukuri nzito kama Taifa kuelekea Tanzania tuitakayo. Source: Taarifa habar Cloudz

Hii ni ishara nzuri ya kumkamata Beno Ndullu ajumuishwe na wale wenzake walioingiza mashine za kuharibu noti kumbe hazikuwa zinahitajika. Kwa hesabu la haraka-haraka, kiasi cha fedha kilichotumika kutengeneza noti mpya za 500 ni kiasi kikubwa na ndani ya miaka mitatu zimechakaa...!! Kiasi hiki cha uharibifu kwa rasilimali za umma kinampasa aliyethibitisha kuwa ni bora ashitakiwe mara moja, au kunyongwa! Wanafanya mzaha maana tumeishia kuongea tu na hakuna hatua za maana zinachukuliwa! Ni Beno Ndullu, na sio mwingine, akamatwe! Alisema Noti mpya zikifuliwa zinatoa rangi, sio tatizo ila hiyo ndiyo alama yake ya 'kiusalama'? kumbe ndio kuchakaa kwenyewe anakokubali sasa! Hawezi kusema zinachakaa mapema kutokana na mzunguko wake kuwa mkubwa, dola zinazunguka sana, hazichakai! Noti za zamani za 500, 1000, na 2000, hata 5000 zinazunguka zana, mbona hazichakai??....Hii yote 'chai' tu...viongozi wamefilisika, wamejaa uongo, sababu tu hakuna wa kuwahukumu....! Rais mwenyewe hata hajui kama noti ya mia tano inazunguka au la....! May God help us!

AKINA NDULLU NA WAZIRI WA FEDHA WAKAMATWE TU...HATUNA JIBU LINGINE...WNAZIDI KUUA UCHUMI HALAFU TUNAWAFURAHIA NA KUCHEKA CHEKA!!
 
huu umekuwa ni mchezo wa hawa jamaa wa BOT wakichacha wanajifanya kutengeneza sarafu ya mi tano, watanzania msiwe wajinga muda mfupi tu mnasahau hebu ziangalieni sarafu zilizopo na ubora wake, kitu ni kile kile. tenda anapewa mchina then watu wanakula 10% yao. huu ni ****** hawa jamaa wanacheza na kodi zetu. nimeagiza sniper watakuja juta subirini
 
Ki uchumi sio Vizuri kuwa na sarafu za thamani kubwa ,uchumi ulikomaa inafaa kuwa na sarafu zenye value ndogo au noti isiyo zidi mia tano 500 ,mfano UK and US hwana hata noti ya 1000 maana yake kuwa uchumi umekuwa,nashauri wachapishe pesa mpya na kiwango cha juu cha noti iwewe buku na wafanye kazi ya kufufua uchumi na kusitisha tabia mbaya ya ufisadi.
 
niulize tu waungwana,hivi hii habari ni siasa mpaka imewekwa ktk jukwaa hili la siasa?au imewekwa hapa tuitizame na kuijadili kisiasa?viongozi wetu wafanye kila kitu kisiasa nasi wananchi tuwe hivyohivyo ukombozi wa nchi hii utatoka wapi?nawasilisha
 
hii inaonyesha thamani ya shilingi ilivyo shuka leo hii sh500 ni ndogo sana hivyo mzunguko wake ni mkubwa ndio maana zinachakaa
nafiri tunahitaji kuwa wahalisia zaidi kuliko kuleta siasa.Noti za miatano sio imara(zilichakachuliwa mwanzo kwa maslahi binafsi) ndio maana hazidumu na sio kama huyu jamaa anavyotudanganya eti zinachakaa kwasababu ya mzunguko mkubwa ktk uchumi,ukijaribu kuzifuatilia hata hizi nyingine zinazobaki huwezi linginasha ubora wake na zile za awali.
 
Ki uchumi sio Vizuri kuwa na sarafu za thamani kubwa ,uchumi ulikomaa inafaa kuwa na sarafu zenye value ndogo au noti isiyo zidi mia tano 500 ,mfano UK and US hwana hata noti ya 1000 maana yake kuwa uchumi umekuwa,nashauri wachapishe pesa mpya na kiwango cha juu cha noti iwewe buku na wafanye kazi ya kufufua uchumi na kusitisha tabia mbaya ya ufisadi.

mmmmmmmmmh huu uchumi wakufaulu kwa videsa!
 
Ndiyo Wakuu! Katika kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu,serikali kupitia gavana bank kuu ,Prof Ndulu inatarajia kuanzisha sarafu ya miatano .Amedai kuwa noti hizo zinachakaa sana kwa sababu mzunguko wake ni mkubwa. Je ule ubora uliokuwa unasemwa uko wapi wakati noti hizo zinatoka? Au ndo ni amini kuwa jamaa walisha kula cha kwao? Hivi ni lini serikali hii ita anzisha vitu endelevu? Tunahitaji tafukuri nzito kama Taifa kuelekea Tanzania tuitakayo. Source: Taarifa habar Cloudz
Tutakapokuwa sisi wananchi kuwa ndio waajiri wa viongozi wetu ndio watafanya kile tunachota, sasa wanafanya watakavo maana wanajua uchaguzi ukifika pilao.,pombe za kienyeji, kofia, t-shirt, vitenge, kanga na kwa wale wabishi zaidi 5,000 na 10,000 inatumika kazi kwisho wanasongesha maisha tuu
 
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT), imeanza mchakato wa kufanyia mabadiliko ya noti mpya ya Sh500, ili iwe ya sarafu baada ya kujiridhisha kuwa inachakaa kwa haraka zaidi.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kutoka Arusha, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu, alisema mchakato kuifanyia mabadiliko na noti hiyo ili iwe katika sarafu, inazingatia ukweli kwamba fedha iliyoko katika mzunguko mkubwa katika jamii.

Profesa Ndulu alisema noti ya Sh500 inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi wengi, jambo linalosababisha kuchakaa haraka kabla ya wakati uliopangwa.

“Tunafanya mchakato wa mabadiliko ya noti hizi zinazochakaa kwa haraka kwa sababu zenyewe zinatumika zaidi,” alisema Profesa Ndulu.

Alisema hatua hiyo haitaathiri mzunguko wa fedha na kwamba sarafu ya Sh500 itakapoanza kutumika, noti hiyo itaondoka polepole.

Alisema sarafu hiyo ya Sh 500 itaanza kupatikana katika kipindi kifupi kijacho na kuwawezesha wananchi kuitumia.
“Watanzania wasishituke mabadiliko hayo ya noti za Sh500 kwenda sarafu maana hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa watoa chenji,”alisema.

Source: Mwananchi
 
mbona hata noti za shilingi elfu 1 zinachakaa haraka au matumizi yake yatapungua tutakapoanza kutumia sarafu ya shilingi mia 5 ?
 
hizi sababu zingine wanazozitoa huwa haziingii akilini....wajiulize kwa nini all of a sudden demand ya noti za shs. 500 imekuwa kubwa, ni kwa sababu ya kushuka kwa uchumi wa bongo hivyo shs. 100 na 200 hazina tena thamani kama zamani. tusipoangalia tutakuja kutengeneza sarafu ya shs. 5000 kwa sababu "zinachakaa haraka"......halafu tunasema tuna wachumi wanaotupa cheap answers kama hizi!
 
Tofty, focus ilikuwa mbona noti za sh 500 ni mbovu sana? Aliulizwa kuhusu ubora wa noti mpya, na ndio swali alilojibu. Alisema noti za sh 500 hazirudi bank, mahali ambapo huwa zilizochakaa zinahifadhiwa. Nilijifikiria kwa jinsi hela ya madafu isivyo na thamani huwezi weka bank sh 15,500 labda kama unadaiwa! Manake kabla hujavuka barabara mia tano ushaitumia.
But still, come to think of it sijawahi kukutana na noti ya $1 iliyochoka kama kichaa!
 
Cheap answer!!!! Matumizi ya sarafu yenye thamani kubwa maana yake isiyo wazi ni kuporomoka kwa thamani ya pesa husika!!!
 
wezi wakubwa hawa, hivi vinoti wamevitengeneza juzijuzi tena kwa mabilioni ya pesa leo wanasema eti wanabadili tena. KWENYE NCHI HII KILA MTU ANAJIFANYIA ATAKAVYO ILIMRADI AJINUFAISHE
 
Watu wengine muwe mnapitia thread kbl ya kupost!

Tangu juzi hii post tumeshapata na tumechangia!

Lakini hizi noti kuanzia 500,1000,2000,5000 na hata 10,000 karibu yote ni feki! Wangerekebisha karibu zote!

Ni mtazamo wangu!
 
Ndiyo wakuu! Katika mwendelezo wa usalama wa Taifa kugeuka uhasama wa Taifa ,leo mhadhara wa Mh.Tindu Lisu kuhusu utaratibu wa kutengeneza katiba na matatizo ya urais wa kifalme umezuiliwa katka mazingira tatanishi baada ya kupata ruhusa jana toka uongozi wa chuo.MWL NYERERE ALIPATA KUSEMA"CHUO KIKUU NI TAASISI YA ELIMU YA JUU AMBAPO AKILI YA BINADAMU HUFUNDISHWA KUFIKIRI KWA UHURU,KINA NA KUCHAMBUA PAMOJA NA KUTATUA MATATIZO KWA HALI YA JUU. SIKO TAYARI KUWAONA WASOMI WAKIPIGA MAGOTI KWA DHANA YA NIDHAMU YA WOGA KWA WATAWALA BALI KATIKA KULINDA MISINGI YA KIKATIBA KWA KUHESHIMU UHURU WAO WA KUELEZA FIKRA NA DHAMIRA YAO KWA MSTAKABALI WA NCHI YAO " Ombwe la uongozi limekuwa sifa ya serikali ya ccm, nchi hii imekumbwa na inaendelea kukumbwa na matatzo mengi sana kamavile madawa ya kulevya,dawa feki,mayai feki, utoroshwaji wa twiga na pembe za ndovu , sumu kwa Mwakyembe, wizi wa madini yetu,ubadhirifu wa pesa za umma karibia taasisi zote za serikali,wizi wa mitihani,uchakachuaji wa kura,ufisadi n.k hawa usalama wa Taifa wanafanya kazi gani kama si makanjanja? Tazama tunaelekea kwenye mchakato wa katiba mpya lakini bado wasomi vyuoni wananywimwa fursa ya kupata elimu hii tena free of charge. KARL MAX ALIPATA KUSEMA" YOU CAN LIQUADATE A PERSON/ORGANISATION BUT CHANGES ARE UNAVOIDABLE." Serikali ya ccm ilipolifikisha Taifa hili hapa ni vigumu sana kuuzima huu upepo wa mabadilko ,kwa kufanya hivo ni sawa na tembo kujificha kwenye shamba la maharage.Kumuzuia Tindu Lisu kufanya mhadhara chuoni ni sawa na kumpiga chura mteke kwani unampunguzia umbali wa kutembea. Hicho ndo kilicho tokea leo kwani Kamanda Lisu kafikisha ujumbe kupitia viwanja vya tawi la Cdm-SAUT huku akiwa amezungukwa na halaiki kubwa ya wasomi na raia wanaozunguka chuo hicho. MUNGU BARIKI TANZANIA,MUNGU BARIKI ACTIVISM. Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom