Serikali kuanzisha sarafu mpya ya mia tano

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
227
Ndiyo Wakuu! Katika kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu,serikali kupitia gavana bank kuu ,Prof Ndulu inatarajia kuanzisha sarafu ya miatano .Amedai kuwa noti hizo zinachakaa sana kwa sababu mzunguko wake ni mkubwa. Je ule ubora uliokuwa unasemwa uko wapi wakati noti hizo zinatoka? Au ndo ni amini kuwa jamaa walisha kula cha kwao? Hivi ni lini serikali hii ita anzisha vitu endelevu? Tunahitaji tafukuri nzito kama Taifa kuelekea Tanzania tuitakayo. Source: Taarifa habar Cloudz
 
Kuleta source ya hii inf yako ni muhimu sana, kama ni kweli naomba serikali wawe wakweli tu mara zote hubadili noti na kuwa sarafu baada ya fedha yake kuporomoka dhamani ndivyo ilivyo hata sasa ukisema inamzungoko mkubwa si wana recycle
 
kuleta source ya hii inf yako ni muhimu sana

kama ni kweli naomba serikali wawe wakweli tu mara zote hubadili noti na kuwa sarafu baada ya fedha yake kuporomoka dhamani ndivyo ilivyo hata sasa ukisema inamzungoko mkubwa si wana recycle

si kaandka hapo source:clouds fm..tatzo wana jf tume kariri mtu akileta mada tu bila hata kumaliza kusoma "source"..
 
lakini watanzania hatuna utaratibu mzuri wa kutunza noti!! sasa mtu anashika noti mikono mibichi au masizi ya mkaa wewe unategemea nini
 
kuleta source ya hii inf yako ni muhimu sana

kama ni kweli naomba serikali wawe wakweli tu mara zote hubadili noti na kuwa sarafu baada ya fedha yake kuporomoka dhamani ndivyo ilivyo hata sasa ukisema inamzungoko mkubwa si wana recycle

Mkuu usemayo ndio ukweli wenyewe. Hii ni manifestation ya prevailing inflation/hyperinflation!.
 
sarafu zenyewe za shilingi 50, 100 na 200 hazina ubora kama za zamani zinachubuka mapema. Gavana anahitaji kueleza sababu zaidi ya hiyo moja.

Noti za Mia tano za Dr Balali zilikuwa bora kuliko hizi za Dr. Beno Ndulu.

Naunga mkono kama ni kwa nia njema.
 
imi nashauri hela zote tanzania ziwe sarafu.
benki ziwekwe zile jackpot tukifika pale tunatumbukiza tunachapa mwendo ukihitaji unaenda pale unchomoa tu.:poa
 
Kutokana na umasikini wa watanzania mzunguko wa noti za sh. 500 ni mkubwa hivyo kuchakaa kwake hakuepukiki ni bora kuwa na sarafu badala ya noti.
 
wakitengeneza noti nyingine waziache na noti mbili zilizotangulia ili tuwe na aina tatu ya noti moja
 
Sarafiu yenyewe iking'aa kama hilo kombe itakuwa safi sana.

8_4f4a89aa88b51737967074.jpg
 
lakini watanzania hatuna utaratibu mzuri wa kutunza noti!! sasa mtu anashika noti mikono mibichi au masizi ya mkaa wewe unategemea nini

Nasubiri wanauchumi watupe majibu ya hili ila naamini au nijuavyo mimi.kuchapisha not mpia nikwamba uchumi unashuka pia thaman ya noti imeshuka au huna noti kwenye mzunguko ndio unato chapa ili ziwe nyingi. Yote kwa yote nikua thamani ya shiling yetu imepotea na inazidi kupotea kilasiku.

Hatuko mbali watu kwenda sokoni na masanduku ya hela kununua mahtaji ya nyumbani kama ilivyokua kwacha ya zambia miaka ya nyuma japo sasa kidogo wanajtahd
 
Kutokana na umasikini wa watanzania mzunguko wa noti za sh. 500 ni mkubwa hivyo kuchakaa kwake hakuepukiki ni bora kuwa na sarafu badala ya noti.

Nashukuru kwa leo kukubali kuwa serikali ya ccm imewafanya watanzania kuwa maskini. Nashukuru sana kwa kukili hilo.
Ila wapelekee taarifa kwamba, there is a breaking point, uvumilivu wa watanzania una mwisho, na huo mwisho hauko mbali sana.
Lazima tutawaweka vijiti kama wananchi wa libya walivyofanya.
 
Ndiyo Wakuu! Katika kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu,serikali kupitia gavana bank kuu ,Prof Ndulu inatarajia kuanzisha sarafu ya miatano .Amedai kuwa noti hizo zinachakaa sana kwa sababu mzunguko wake ni mkubwa. Je ule ubora uliokuwa unasemwa uko wapi wakati noti hizo zinatoka? Au ndo ni amini kuwa jamaa walisha kula cha kwao? Hivi ni lini serikali hii ita anzisha vitu endelevu? Tunahitaji tafukuri nzito kama Taifa kuelekea Tanzania tuitakayo. Source: Taarifa habar Cloudz

Hii ni ishara nzuri ya kumkamata Beno Ndullu ajumuishwe na wale wenzake walioingiza mashine za kuharibu noti kumbe hazikuwa zinahitajika. Kwa hesabu la haraka-haraka, kiasi cha fedha kilichotumika kutengeneza noti mpya za 500 ni kiasi kikubwa na ndani ya miaka mitatu zimechakaa...!! Kiasi hiki cha uharibifu kwa rasilimali za umma kinampasa aliyethibitisha kuwa ni bora ashitakiwe mara moja, au kunyongwa! Wanafanya mzaha maana tumeishia kuongea tu na hakuna hatua za maana zinachukuliwa! Ni Beno Ndullu, na sio mwingine, akamatwe! Alisema Noti mpya zikifuliwa zinatoa rangi, sio tatizo ila hiyo ndiyo alama yake ya 'kiusalama'? kumbe ndio kuchakaa kwenyewe anakokubali sasa! Hawezi kusema zinachakaa mapema kutokana na mzunguko wake kuwa mkubwa, dola zinazunguka sana, hazichakai! Noti za zamani za 500, 1000, na 2000, hata 5000 zinazunguka zana, mbona hazichakai??....Hii yote 'chai' tu...viongozi wamefilisika, wamejaa uongo, sababu tu hakuna wa kuwahukumu....! Rais mwenyewe hata hajui kama noti ya mia tano inazunguka au la....! May God help us!
 
Ndiyo Wakuu! Katika kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu,serikali kupitia gavana bank kuu ,Prof Ndulu inatarajia kuanzisha sarafu ya miatano .Amedai kuwa noti hizo zinachakaa sana kwa sababu mzunguko wake ni mkubwa. Je ule ubora uliokuwa unasemwa uko wapi wakati noti hizo zinatoka? Au ndo ni amini kuwa jamaa walisha kula cha kwao? Hivi ni lini serikali hii ita anzisha vitu endelevu? Tunahitaji tafukuri nzito kama Taifa kuelekea Tanzania tuitakayo. Source: Taarifa habar Cloudz
Hakuna serikali yoyote duniani inachapisha sarafu fulani kwa sababu ya uchakavu wa noti. Kigezo kimojawapo kinachofanya sarafu kubwa kuchapishwa ni uporomokaji wa uchumi wa nchi husika. Mfano miaka ya hadi 1985 noti ya juu Tz ilikuwa 100. kulikuwa na noti za sh. 5,10,20, 50.
Leo hii miaka karibu 15 tu, tupo hapa tulipo, na sasa wanataka kuchapisha sarafu ya miatano kusingizia uchakavu, what shame, what stupidity in their minds. Wanadhani wote ni wajinga wa kuamini haraka kuwa sababu ya uchakavu wa noti inafanya wachapishe sarafu? Kwanini basi wasichapishe hela yote katika sarafu hadi noti ya elfu kumi, ili tuachane na usumbufu wa uchakavu wa noti kwa miaka ijayo? Ili pia tuonekane nchi ya kwanza duniani kuwa na hela ya sarafu tu.
Ni jambo la kusikitikia kuliko kufurahia. Uchumi wa Tz unaporomoka kila kukicha. Waliopewa dhamana ya kuulinda uchumi wetu wapo usingizini, au hawajali, au yote pamoja.
Ni Mkapa tu, pamoja na madhaifu mengine ya kiufisadi ya serikali yake, alijitahidi kurudisha heshima ya uchumi wetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom