Serikali kuanza kutoza ushuru wa bidhaa wa 5% kwenye magari yenye uwezo wa injini kati ya 1,000CC-2,000CC

Gotze Giyani

Senior Member
Feb 28, 2022
121
180
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia tano kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa kati ya 1,000 CC hadi 2,000CC.

“Ushuru huo utatozwa ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana. Magari hayo ni yale yanayotambuliwa kwenye H.S Codes 8703.40.00, 8703.50.00, 8703.60.00 na 8703.70.00,”amesema

Dk Nchemba ameyasema hayo leo Alhamis Juni 15, 2023 akiwasilisha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Hivi hapa wadau ni wameshusha kodi au, kama kuna aliyeelewa naomba anieleweshe.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaanza kutoza ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia tano kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa kati ya 1,000 CC hadi 2,000CC.

“Ushuru huo utatozwa ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana. Magari hayo ni yale yanayotambuliwa kwenye H.S Codes 8703.40.00, 8703.50.00, 8703.60.00 na 8703.70.00,”amesema

Dk Nchemba ameyasema hayo leo Alhamis Juni 15, 2023 akiwasilisha hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Hivi hapa wadau ni waneshusha kodi au kama kuna aliyeelewa naomba anieleweshe
Ushuru na kodi ni kitu kimoja? Maana habari inaongelea ushuru wewe unauliza kodi. Pia habari inasema wataanza kutoza ushuru, nadhani hawamaanishi kupunguza au kuongeza ila wanaanza(kitu kipya). Nimejibu kutokana na utangulizi wa swali lako, sina taaluma ya kodi.
 
Naombeni ufafanuzi katika ukurasa wa 107 kitabu Cha bajeti ambapo serikali imependeza kama ifatavyo:

iv) Kutoza Ushuru wa bidhaa kwa kiwango cha asilimia 5 kwenye magari yenye uwezo wa injini (Engine Capacity) wa kati ya 1000cc hadi 2000cc yaliyotokana na ukuaji wa teknolojia ili kuwianisha na magari mengine yenye ukubwa unaofanana yanayotozwa ushuru huo. Magari hayo ni yale yanayotambuliwa kwenye H.S Codes
8703.40.00, 8

Maswali yangu...
1. Je, kuna ongezeko la ushuru wa manunuzi kwa haya magari au ushuru umeshuka?

2. Je, huu ni ushuru mpya?
 
Back
Top Bottom