Serikali kuanza kujenga barabara za juu kupunguza msongamano wa magari Dar!

magufuli kashapoteza credibility yake kwa watanzania, yahani anadanganya kweupee mchana? dar yenyewe bado barabara za vumbi kibao na hata hizo za lami zenyewe ni vilaka na mashimo kibao. Nadhani wamemwambia adanganye ili CCM watuibie kura tena. Ndio yaleyale ya Jairo
 
Hapo ndipo magufuli atachemsha kama wanafanya kisiasa hii inakula kwao
hata barabra ngapi zingemnge juu kwa mfumo wa hizi daladala na kila mtu na gari kwenye mjini
hakuna nafuu yeyote

kama wanataka yangengwe maegesho ya magari pembeni mwa miji na mabasi makubwa yatumike kutoa watu hapo kwenye mjini ,yaani katika ya miji
ndivyo wenzetu walivyo ishinda kwa mbali trafic jam lakini haya mengine hakuna faidi
TEMBEA UONI

wafanye STUDY KWANZA JAMANI DUH hela nyingi hizo zipotee tu
 
Unapoomba msaada kuna mawili kupewa au kunyimwa, Je waziri anataka kutuambia kwamba sisi Watanzania hatuna pesa za kujenga fly-overs Ubungo junction, mwenge junction, buguruni, Pugu Road, Kilwa Road, Salendar bridge pamoja na kupanua barabara kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kwa kiwango cha highway kama hapa chini? Uwezo tunao na sababu tunazo pesa wanazokula wageni kwa tax holiday na wanazokula mafisadi zinatosha kabisa. Tumechoka na ajali.




Hatuwezi kutegemea wafadhili kutatua matatizo yetu,

Japan wanapalilia soko lao la magari,
ni wakati wa kufanya uamuzi sisi wenyewe.


Ooops kuna jamaa kanitonya mbona kuna hard shoulder hapo ni ya nini? Teh teh ... ... ...
 
kwanini wasianze na barabara za uchochoro?mfano mbezi goba tangi bovu ambayo itaondoa folen za ubungo kwa wale waendao mwenge,tgt,mikochen etc it wl mean that sio lazima atokae kimara aende ubungo.pia lami itoke mbezi mwisho kwenda airpot.wasisingizie halmashauri kwan hela wanayopewa haitoshi.najua wakitenga kma bilion 40 wanawezafanya la maana.
 
Barabara za chini zimewashinda za juu wataziweza?
Ni sawa na kutaka kujenga choo kabla ya nyumba

Hii kaka ikaa vibaya haijatulia kabisa, unalosema kweli kabisa barabara zimesha washinda za kawaida tu sasa hizo za juu labda lipewe kampuni kuweza kuzi manage maana wabongo wala hazitachukua miezi sita utasikia zimeeanza kuangukia watu.
 
Kupinga barabara za juu DSM ni kupinga maendeleo,huwezi kuwaweka wafanyakazi masaa matatu katika foleni na ukasema unataka uchumi wa nchi ukue,Kujenga barabara za juu ni moja kati ya ufumbuzi wa tatizo lakini kuna haja ya kupanua mji kwa maana ya baadhi ya ofisi na shughuli nyingine kuhamia nje ya mji sio kila kitu Posta na Kariakoo tu.SHIDA YANGU NI JE SERIKALI HII YA ****** ILIYOKOSA UELEKEO INAWEZA KWELI KUJENGA HIZO BARABARA AU NI SIASA NYEPESI TU WANAFANYA?

Mkuu mimi nadhani watu hawapingi barabara za juu ila wanataka wawe na uhakika kwamba foleni itapungua hapa dar. Hebu fikiria kwamba barabara ya juu inajengwa pale kamata (pale kwenye mataa) na siyo kwamba inapita juu kwa juu hadi mjini bali ni pale tu penye kupishana magari. Sasa kama hakuna barabara nyingine mbadala si magari toka gongo la mboto, airport na pugu yatakuja kulundikana pale njia panda ya chang'ombe?

Fikiria pia kwamba fly over inajengwa ubungo na inapeleka magari manzese si magari yatakwama pale manzese kuelekea magomeni. Suluhu bora ni kuimarisha na barabara za vichochoroni ili kupunguza msongamano kwenye barabara kuu.

Pia suluhu ni kujenga kitu inaitwa ring roads kwa mfano unaunganisha Nyerere Road na Bagamoyo Road kwa kupitia Kinyerezi unakatiza Morogoro Road unapita mbezi ya kimara, hadi huko bunju. Kwa hiyo mtu toka Airport/vingunguti akiwa anaenda Bagamoyo ama Bunju ama Morogoro hatakuwa na haja ya kupita Tazara ama Ubungo.

Kwa hiyo fly overs zikisaidiwa na vitu kama hivyo itakuwa sawa ila kupiga kelele tu kwamba tunajenga fly overs kupunguza foleni tutakuwa tunajidanganya.
 
Flyover zitapunguza foleni ubungo na TAZARA bt foleni ya Dar ni kila mahali tbt, kkoo, mjini, kurasini etc. inatakiwa solution nyingi za pamoja maana miaka 5 ijayo sijui hali itakuwaje.

masterplan ya Dar ni jehanamu na kuirekebisha inahitaji viongozi wa kweli
 
Hapa Nairobi tayari wameanza, wachina wapo kazini, sisi Bongo tunaendelea na stori kila leo. Daraja la Kigamboni kila mwaka linatajwa lakini hadi leo hatuoni kitu.
 
Tusubili tuone maana jamaa amewakilisha kwa mbwembwe sana.

Ngugu yangu hata Sheria ile ya Uchaguzi si Ulionaga Mbwembwe zake kwenye Ku-Sign baadae Tukaambiwa inahitilafu Inabidi Ikakalabatiwe!
Mbwembwe ndio Hulka ya Watanzania hasa wanasiasa Wetu!
 
Hebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
Mpango huu wa serikali hauna tija na ni ufujaji wa rasilimali ya nchi. Nina uhakika wataalam hawajashauri njia hiyo ya kutatua kero ya foleni.

Nimeesikia mapendekezo ni kujenga fly over pale ubungo na tazara. Cha kujiuliza ni kwamba zitakuwa na tija? Kumbuka hapatakuwa na flyover pale shekilango, wala magomeni au fire au hata makutano ya morogoro na bibi Titi. Je, traffic itakayopita ubungo toka mbezi itaflow vipi katika junctions hizo? Nikitafakari sana nakumbuka ule utaratibu wa njia tatu wa enzi za Lowassa!

Naishauri serikali hii ya ccm iache kukurupuka na ifanye mambo kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam na kwa kufanya tafiti. Hizo pesa za fly over zitumike kuboresha feeder roads kwanza!
 
Hebu tusiibeze serikali wakati inapotaka kufanya mambo ya maana. Flyovers Dar ni muhimu na sioni kwa nini mtu atilie shaka kwamba serilkali haitaweza. Tuipe muda serikali ijenge hizi flyovers
Hiyo kwa sasa sahau japokuwa magufuli ni waziri mahiri na mchapakazi na hodari sana kuliko mawaziri wenzake wote na huwa anachokisema ndicho anachokifanya, si mbabaishaji wala mwongo km wenzie na ni waziri anayeaminika kwelikweli ila KWA HILI NAAMINI KUWA KATUDANGANYA LIVE namshauri afute kauli yake itamcost sana
 
Hizo barabara za chini zenyewe mbovu nazikijengwa ni muda mfupi zinakuwa na mabonde sasa zikijengwa za juu tutakuwa salama kweli ama ndo wanataka kutumaliza
 
Siku hizi hata wakuja wote mnamagari, halafu hakuna maendeleo? Mnanshangaza!
 
Swala la ujenzi wa nyumba za serikali ni swala ambalo yeye magufuri anatakiwa atupe majibu ya uhakika kwa vile ndiye aliyeuza zile zilizokuwapo wakati huo. Je serikali ilipata faida gani katika kuuza nyumba zile, na je ujenzi huu mpya utaleta faida gani kwa serikali ambayo iliamua kuuza zile ilizokuwazo zamani?
 
Siku hizi hata wakuja wote mnamagari, halafu hakuna maendeleo? Mnanshangaza!

kwako wewe maendeleo ni magari? Je unajua kuwa katika nchi nyingine maskini wa kutupwa kabisa wanalala kwenye magari yao? Yaani magari ndiyo nyumba yao?
 
Waziri wetu aache uswahili; ACTIONS SPEAKS LAUDER THAN WORDS. Wenzetu Kenya hawakuwa wanaliongelea kila siku toka Rais, Waziri Mkuu, Waziri Wa Ardhi na Wabunge.... Wao walitenga pesa na kuanza kujenga kabla hata BUNGE lao kulijadili... WE WANT ACTION FIRST!!!!
 
kwanini wasianze na barabara za uchochoro?mfano mbezi goba tangi bovu ambayo itaondoa folen za ubungo kwa wale waendao mwenge,tgt,mikochen etc it wl mean that sio lazima atokae kimara aende ubungo.pia lami itoke mbezi mwisho kwenda airpot.wasisingizie halmashauri kwan hela wanayopewa haitoshi.najua wakitenga kma bilion 40 wanawezafanya la maana.
Umenena Mkuu!
Ila 40Billion ni Kidogo kwa kutatua tatizo la Barabara Bongo hata hizo zinazoitwa Feeder Roads!
 
Swala lingine ni la kujenga nyumba 47/48 Dar na mbili Idodomia. Hivi mandate ya serikali kujenga nyumba haiko chini ya NHC? Kwa nini kila wizara inataka kujenga nyumba zake na sio kutumia shirika la NHC? Je wamegundua nini ambacho NHC hawawezi kufanya? Au ndio danganya toto ile ile ya kukwapua mpunga wa walipa kodi?

Ninachoelewa mandate ya kujenga nyumba za serikali iko chini ya wakala wa majengo ya serikali (Tanzania Building Agency) iliyopo chini ya wizara ya ujenzi. NHC ni shirika la nyumba linalojitegemea likiwa chini ya wizara ya ardhi na makazi na linajenga nyumba za kukodisha - wao wako kibiashara zaidi.
 
Back
Top Bottom