Serikali iwekeze zaidi Elimu mikoa ya Lindi na Mtwara...wengi wao hawathamini Elimu

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Ni muhimu sana kuwekeza Katika elimu ya primary,secondary na hatimaye elimu ya vyuo vya kati na vyuo vikuu.

Na pia uwekezaji Katika elimu ya ufundi ukizingatia viwanda vingi vimejengwa Mkoa wa Pwani itawasaidia sana ktk ajira.

Wadau mbalimbali na Imani kuwa hiyo nayo ni fursa Katika uwekezaji ili kwenye elimu kusadia vijana wetu wa mikoa hii miwili ili kuwafanya wawe wapate ufahamu wa kukabiliana na mazingira na kupunguza kujiingiza Katika tabia hatarishi kama mimba za utotoni na ndoa za mapema.

Na hata kupunguza vijana kutumiwa na watu wenyewe nia mbaya kwenye vitendo vya uhalifu.
 
Sijui kama wasimamizi wa elimu wanalijua hilo.. Mwanafunzi wa form one hajui kusoma alphabet A-Z wakati shule ya msingi kuna somo la English.
Mwanafunzi wa form one hawezi kunakili neno lililoandikwa ubaoni.
Mwanafunzi wa form one hajui kusoma Kiswahili ambacho kwacho amejifunzia kwa miaka Saba.
Mwanafunzi huyu huyu tunasubiri afaulu vizuri akifika form four.
Maoni yangu elimu ya msingi iboreshwe. Serikali iwe serious, sio kufurahia mwalimu afundishe darasa moja lenye zaidi ya wanafunzi 100 hapo hapo ana vipindi zaidi ya 50 kwa wiki. Hakomolewi mwalimu ila watoto wetu ndo wanaopata hasara kwa kukosa haki ya kupata elimu.
Haki Elimu mko wapi? Ni ipi ratio ya mwalimu kwa wanafunzi?
 
Naunga mkono hoja... kusema tu kwamba eti watu wa maeneo hayo hawaipendi elimu na kuwaacha tu kama walivyo bila kuwapa shinikizo la namna yoyote si kuwatendea haki. Serikali ina jukumu la kuweka mkazo maeneo hayo. Hii ni nchi yetu sote.
 
Hilo la msingi
 
CCM mnayoichagua kila mara inatakiwa iwasaidie kwahilo.

Mikoa ya Kaskazini wengu hawakuisubiri serikali iwasaidie katika hilo.

Mbali na Missionaries pia juhudi zao thabiti zilitufanya kuendelea kielimu.

Wazazi wenu pia wanapaswa kuhimiza elimu kwa vijana na watoto plus nguvu kutoka CCM.
 
1._Ni kosa, na upendeleo kwa kqnda fulani.
2. Kuna namna nyingi za kuboresha Elimu, kama kuwapa wazazi changamoto, na waliosoma kupata ajira. Ikiwa kama bijana wapo mitaani hawana ajira, Je kwa nini mzazi asione kuvua na kucheza ngoma ni muhimu?
3. Elimu Vila Malipo ilikosewa. Luna haja ya kuboresha Elimu ya Juu kupata wataalamu. Wazazi wasumbukie Elimu ya msingi na sekondari. Ndio kutimiza wajibu.
4._Je Luna haja gani ya kuwahimiza watu wafanye Nazi ili hali kila kitu unataka uwape bure?
 
Sijui kama wasimamizi wa elimu wanalijua hilo.. Mwanafunzi wa form one hajui kusoma alphabet A-Z wakati shule ya msingi kuna somo la English.
Mwanafunzi wa form one hawezi kunakili neno lililoandikwa ubaoni.
Mwanafunzi wa form one hajui kusoma Kiswahili ambacho kwacho amejifunzia kwa miaka Saba.
Mwanafunzi huyu huyu tunasubiri afaulu vizuri akifika form four.
Maoni yangu elimu ya msingi iboreshwe. Serikali iwe serious, sio kufurahia mwalimu afundishe darasa moja lenye zaidi ya wanafunzi 100 hapo hapo ana vipindi zaidi ya 50 kwa wiki. Hakomolewi mwalimu ila watoto wetu ndo wanaopata hasara kwa kukosa haki ya kupata elimu.
Haki Elimu mko wapi? Ni ipi ratio ya mwalimu kwa wanafunzi?
Haki elimu wanajitahidi sana kuusaidia umma kuyaelewa mapungufu yetu katika suala zima la kutoa elimu. Hivyo haishangazi kuona likipata misukosuko mingi katika kutekeleza majukumu yake. Kuna wasiwasi kama watapona katika usajiri mpya wa NGOs kwa vile wakati mwingine wamekuwa too critical.
 
....serikali sikivu...
 
Back
Top Bottom