Serikali isipowapiga marufuku 'Mitume na Manabii' wa mchongo, miaka michache ijayo tutakuwa na Taifa la ovyo sana

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,282
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia huduma zinazotolewa na hawa manabii na mitume wanaoibuka kama uyoga hapa nchini.

Nimegundua Serikali isipochukua maamuzi magumu kuwapiga marufuku hawa watu, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa na kizazi zembe na ovyo sana. Sisemi maneno matupu bali nina ushahidi kuntu juu ya hili jambo.

Nimezaliwa Kenya lakini kwa bahati nzuri nimekulia jiji la Dar ambako manabii na mitume wengi huibukia na kuanza kazi yao ovu ya kuwarubuni akina mama na watoto wakiwakamua fedha bila huruma.

Mwanzoni aliibuka nabii Tito lakini huyu jamaa Mungu alimpiga kipapai na kumuondoa kwenye ushetani moja kwa moja. Baadaye alikuja Mtume na Nabii Josepahat Mwingira ambaye hadi sasa yupo na anajaribu kujitanua hadi nchi za nje ijapokuwa soko limekuwa gumu baada ya kuibuka manabii wengine. Hajakaa sana akaja mama wa upepo wa kisulisuli kutoka mlima wa moto. Naye alizipiga sana kabla ya kuitwa na Mungu wa ukweli kwenye nyumba yake ya milele.

Alifuata Nabii Lusekelo (Mzee wa Upako) akawadanganya sana akina mama kwamba atawapa upako wa kununua magari na kuwajaza mali nyingine kedekede. Pia aliwarubuni kuwa atawapa upako wa kuhamia nje ya nchi wakaishi maisha mazuri huko (kumbuka Wasabato masalia waliokusanyika uwanja wa ndege kutaka kwenda Marekani pasipokuwa na pasipoti wala nauli ya kuendea huko). Mzee wa Upako aliwapiga sana hela akina mama kabla ya Mungu wa kweli kumuumbua kwenye ulevi na huo ndio ukawa mwisho wake.

Kisha alikuja Josephat Gwajima ambaye hakudumu sana kwenye fani ya upigaji wa kimiujiza baada ya kuanza kuchanganya dini na siasa. Akaanza hadithi zake za Daudi Bashite, kitendo kilichopelekea kupoteza mvuto mbele za waumini. Baadaye aliamua kuzama jumla kwenye siasa ambapo alishiriki katika wizi wa uchaguzi kwa kushirikiana na mwendazake. Kwa sasa amepoteza kabisa mvuto wa upigaji kwenye dini amehamishia upigaji wake kwenye siasa. Amegundua upigaji wa kwenye siasa hautumii nguvu kubwa sana.

Hatimaye amekuja Nabii Mwamposa (Bulldozer); sasa hivi huyu ndiye yupo kwenye chati. Uzuri ni kwamba baada ya nabii mmoja kuwa maarufu na kuongezeka kiwango cha upigaji, Mungu humshusha ghafla na kumrudisha chini kabisa. Mungu ni mkubwa na wala hajawahi kudhihakiwa. Huyu Bulldozer sasa hivi amekuwa mwiba kwenye kuwaibia fedha akina mama. Eti anawaambia watoe pesa zote walizonazo wampe kama sadaka (kujimaliza) kisha atawaombea wapate utajiri.

Makubwa! Kama ana uwezo wa kuwabariki wenzake wapate fedha, kwanini asijibariki yeye mwenyewe apate mamilioni ya fedha badala ya kutumia ulaghai kuwauzia wafuasi wake mafuta, maji na udongo wa upako? Hana tofauti na mganga wa jadi anayekuambia umlipe pesa akupe pesa za majini. Kwanini yeye asitengeneze hizo fedha za majini badala yake anawaomba wateja fedha halali halafu anawaahidi fedha za majini? Nonsense!

Baada ya watu wengi kugundua utume na unabii ni njia ya kutoka kimaisha, kila mtu sasa anataka kukimbilia huko. Eti hadi Masanja Mkandamizaji naye kafungua kijiwe cha kupigia hela, anajiita “Askofu”. Ni askofu gani ambaye anaibuka from no where hajaenda hata bible college akasome theology anakuja hapa kuwadanganya watanzania kwamba yeye ni Askofu? Hivi hawa watu wanatuonaje?

Wanwake wengi wamewaacha waume zao baada ya kupigiwa ramli na manabii zao kwamba waume walio nao kwa sasa sio waume sahihi, hivyo kupelekea ndoa nyingi kuvunnjika na kusababisha maumivu kwa watoto wasiokuwa na hatia na wengi wao wamegeuka kuwa ombamba na watoto wa mitaani. Inauma sana.

Akina mama wapo tayari kugegedwa na manabii au kukubali kushiriki ujinga wowote ilmradi tu waahidiwe mafanikio hewa. Akina mama wasiopata mimba kwa muda mrefu ni rahisi kurubuniwa na manabii wanaojidai kuingiza upako ukeni kupitia uume. Na kwa akili zao finyu, wanawake hawakatai wala kupinga kila masharti wanayopewa na mitume na manabii hawa wa mchongo.

Mh mama Samia, wanawake wenzako na wapigakura wako wanaaangamizwa kwa kukosa maarifa. Wanapotoshwa kwa kiasi kikubwa sana na hawa manabii na mitume wa mchongo. Hakuna fedha/mafanikio yanayopatikana pasipo kufanya kazi.

Kama tukiendelea na tabia hii ya kuishi kwa kutegemea miujiza, baada ya miaka michache ijayo taifa hili litakuwa na watu wa ajabu sana, wasiopenda kufanya kazi lakini wanataka mafanikio ya haraka kupitia miujiza ya kufikirika.

Tazama hata wazungu waliotuletea hizi dini za ajabu tukasahau dini zetu za jadi wao hawashiriki kwenye miujiza hii ya kufikirika. Wachina wajapan, wahindi na makabila mengine huko Ulaya na Asia huwezi kuwaona wakiamninishwa kirahi kama sisi waswahili.

Amkeni kumekucha!
 
Hao ni wajinga wacha waliwe,hata ukiondoa manabii feki wote,tatizo la waumini wao halitakwisha,Cha kujiuliza kwanini watu wanataka miujiza sana?

Maisha yamekuwa magumu,Kodi za pango,chakula,ada,magonjwa,binadamu anatafuta faraja,na apewe matumaini,hapo ndio wapigsji hutokea,umaskini uliosababishwa na ccm ndio umeleteleza yote haya,
China,Japan,Korea(inapotoka Samsung Galaxy)hakuna "manabii"

Nchi zisizo fata huu upuuzi,zimetupa Mengi,simu,magari,tv,sie tunaokesha tumeipa Dunia nini?
 
Nafuatilia kwanza utarudi baadae🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️
 
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia huduma zinazotolewa na hawa manabii na mitume wanaoibuka kama uyoga hapa nchini.

Nimegundua serikali isipochukua maamuzi magumu kuwapiga marufuku hawa watu, miaka michache ijayo tutakuwa na taifa na kizazi zembe na ovyo sana. Sisemi maneno matupu bali nina ushahidi kuntu juu ya hili jambo.

View attachment 2411428
Nimezaliwa Kenya lakini kwa bahati nzuri nimekulia jiji la Dar ambako manabii na mitume wengi huibukia na kuanza kazi yao ovu ya kuwarubuni akina mama na watoto wakiwakamua fedha bila huruma. Mwanzoni aliibuka nabii Tito lakini huyu jamaa Mungu alimpiga kipapai na kumuondoa kwenye ushetani moja kwa moja. Baadaye alikuja Mtume na Nabii Josepahat Mwingira ambaye hadi sasa yupo na anajaribu kujitanua hadi nchi za nje ijapokuwa soko limekuwa gumu baada ya kuibuka manabii wengine. Hajakaa sana akaja mama wa upepo wa kisulisuli kutoka mlima wa moto.

Naye alizipiga sana kabla ya kuitwa na Mungu wa ukweli kwenye nyumba yake ya milele.

View attachment 2411459
Alifuata Nabii Lusekelo (Mzee wa Upako) akawadanganya sana akina mama kwamba atawapa upako wa kununua magari na kuwajaza mali nyingine kedekede. Pia aliwarubuni kuwa atawapa upako wa kuhamia nje ya nchi wakaishi maisha mazuri huko (kumbuka Wasabato masalia waliokusanyika uwanja wa ndege kutaka kwenda Marekani pasipokuwa na pasipoti wala nauli ya kuendea huko). Mzee wa Upako aliwapiga sana hela akina mama kabla ya Mungu wa kweli kumuumbua kwenye ulevi na huo ndio ukawa mwisho wake.

Hatimaye amekuja Nabii Mwamposa (Bulldozer); sasa hivi huyu ndiye yupo kwenye chati. Uzuri ni kwamba baada ya nabii mmoja kuwa maarufu na kuongezeka kiwango cha upigaji, Mungu humshusha ghafla na kumrudisha chini kabisa. Mungu ni mkubwa na wala hajawahi kudhihakiwa.

Huyu Bulldozer sasa hivi amekuwa mwiba kwenye kuwaibia fedha akina mama. Eti anawaambia watoe pesa zote walizonazo wampe kama sadaka (kujimaliza) kisha atawaombea wapate utajiri.

Makubwa! Kama ana uwezo wa kuwabariki wenzake wapate fedha, kwanini asijibariki yeye mwenyewe apate mamilioni ya fedha badala ya kutumia ulaghai kuwauzia wafuasi wake mafuta, maji na udongo wa upako? Hana tofauti na mganga wa jadi anayekuambia umlipe pesa akupe pesa za majini.

Kwanini yeye asitengeneze hizo fedha za majini badala yake anawaomba wateja fedha halali halafu anawaahidi fedha za majini? Nonsense!

Baada ya watu wengi kugundua utume na unabii ni njia ya kutoka kimaisha, kila mtu sasa anataka kukimbilia huko. Eti hadi Masanja Mkandamizaji naye kafungua kijiwe cha kupigia hela, anajiita “Askofu”. Ni askofu gani ambaye anaibuka from no where hajaenda hata bible college akasome theology anakuja hapa kuwadanganya watanzania kwamba yeye ni Askofu? Hivi hawa watu wanatuonaje?

Wanwake wengi wamewaacha waume zao baada ya kupigiwa ramli na manabii zao kwamba waume walio nao kwa sasa sio waume sahihi, hivyo kupelekea ndoa nyingi kuvunnjika na kusababisha maumivu kwa watoto wasiokuwa na hatia na wengi wao wamegeuka kuwa ombamba na watoto wa mitaani. Inauma sana.

Akina mama wapo tayari kugegedwa na manabii au kukubali kushiriki ujinga wowote ilmradi tu waahidiwe mafanikio hewa. Akina mama wasiopata mimba kwa muda mrefu ni rahisi kurubuniwa na manabii wanaojidai kuingiza upako ukeni kupitia uume. Na kwa akili zao finyu, wanawake hawakatai wala kupinga kila masharti wanayopewa na mitume na manabii hawa wa mchongo.

Mh mama Samia, wanawake wenzako na wapigakura wako wanaaangamizwa kwa kukosa maarifa. Wanapotoshwa kwa kiasi kikubwa sana na hawa manabii na mitume wa mchongo. Hakuna fedha/mafanikio yanayopatikana pasipo kufanya kazi

. Kama tukiendelea na tabia hii ya kuishi kwa kutegemea miujiza, baada ya miaka michache ijayo taifa hili litakuwa na watu wa ajabu sana, wasiopenda kufanya kazi lakini wanataka mafanikio ya haraka kupitia miujiza ya kufikirika.

Tazama hata wazungu waliotuletea hizi dini za ajabu tukasahau dini zetu za jadi wao hawashiriki kwenye miujiza hii ya kufikirika. Wachina wajapan, wahindi na makabila mengine huko Ulaya na Asia huwezi kuwaona wakiamninishwa kirahi kama sisi waswahili.

Amkeni kumekucha!
Injili lazima isonge mbele. Manabii wa uwongo wapo tangu zama za Yesu
 
Utaongea weeee hadi utachoka..dini na siasa ni mapacha wasio fanana..na wanategeneana sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Saizi wanavamia viwanja vilivyowazi ukizubaa unakuta washafungua kanisa la mabati. Kuna sehemu mbezi viwanja vitupu vimeongozana kama vinne na vyote jamaa wametia kambi wamefungua makanisa halafu maspika makubwa balaa wanapigiana kelele wao kwa wao
 
Back
Top Bottom