Serikali iongeze bei ya energy drinks ili kunusuru maisha ya Watanzania

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Wasalaam wana jamiiforum

Kumekua na matumizi mabaya sana ya energy drinks Tanzania. Mbaya kuliko ni kwamba hadi watoto wadogo wa shule za msingi ni wanywaji wakubwa wa hivi vinywaji.

Na wanavichukulia powa kwamba vinawachangamsha na kuwaondolea uchovu lakini taratibu vinawamaliza.

Nimewaza bei yake madukani na vile zinazalishwa kwa wingi na makampuni tofautitofauti nikagundua soko lake ni kubwa sana nikaona ni heri serikali sasa ipandishe bei ipate mapato ya kusaidia waathirika na kupunguza matumizi yake kwa watanzania.

Bei ya chini ikiwa 5,000 kwa chupa sio mbaya kabisa

View: https://youtu.be/fHEDEy-P_xc?si=bJdgfMoKoEku53HJ

Watakaoshindwa kutumia ni vizuri warudi kwenye kutumia chai, kahawa na juice

Energy ni mbaya bora unywe beer
Kibaya zaidi hadi Kuna wamama wanawapa watoto wao under 5yrs nadhani ni elimu hawana juu ya hii kitu
 
Vitumbua +Energy .Naunga mkono hojaa

Hivi eeeh
download.jpeg
 
Ni tatizo linatengenezwa na serikali inakaa kimya kwa maana imeruhusu watu wake wawe weaknesses hapo mbeleni, yote ni serikalini kuto kuithamini kesho.

Hata wenye viwanda pamoja na kuangalia wingi wa faida leo lakini sijui kama wanapiga hesabu ya hasara kwa kesho .

Naunga mkono bidhaa hizo zipande bei au zipunguzwe uzalishaji na usambazaji ziweze kuadimika automatically bei itapanda na taratibu watu tutaacha kununua hizo energy drink mimi binafsi ni miongoni mwao wanaotumia hivyo vinywaji.
 
Nisaidie basi kufikiri Mkuu
Tufanye nini ili watoto wetu wanunue maji, maziwa na juice badala ya eneji!???
Kwani watoto wenu wanapata wapi pesa ya kununua hizo enejii?? Ni kwa nini wewe unampa mtoto wako pesa badala ya kumpa maji, maziwa na juice (hata hivyo juice sio poa kabisa kwani ni chemicals tu unamlisha mwanao). Anzia hapo kufikiri.
 
Ni tatizo linatengenezwa na serikali inakaa kimya kwa maana imeruhusu watu wake wawe weaknesses hapo mbeleni, yote ni serikalini kuto kuithamini kesho.
Hata wenye viwanda pamoja na kuangalia wingi wa faida leo lakini sijui kama wanapiga hesabu ya hasara kwa kesho .

Naunga mkono bidhaa hizo zipande bei au zipunguzwe uzalishaji na usambazaji ziweze kuadimika automatically bei itapanda na taratibu watu tutaacha kununua hizo energy drink mimi binafsi ni miongoni mwao wanaotumia hivyo vinywaji.
Unafikiri hawajui!!?
TBS wanajua ni hatari kiasi gani!

Serikali Ina tumia viwanda ku control population!!

Hiyo ninsera duniani kote!!
 
Kwani watoto wenu wanapata wapi pesa ya kununua hizo enejii?? Ni kwa nini wewe unampa mtoto wako pesa badala ya kumpa maji, maziwa na juice (hata hivyo juice sio poa kabisa kwani ni chemicals tu unamlisha mwanao). Anzia hapo kufikiri.
Sijasema mtoto wangu anakunywa
Mtoto wa mwanzio ni mwanao
 
Ni tatizo linatengenezwa na serikali inakaa kimya kwa maana imeruhusu watu wake wawe weaknesses hapo mbeleni, yote ni serikalini kuto kuithamini kesho.
Hata wenye viwanda pamoja na kuangalia wingi wa faida leo lakini sijui kama wanapiga hesabu ya hasara kwa kesho .

Naunga mkono bidhaa hizo zipande bei au zipunguzwe uzalishaji na usambazaji ziweze kuadimika automatically bei itapanda na taratibu watu tutaacha kununua hizo energy drink mimi binafsi ni miongoni mwao wanaotumia hivyo vinywaji.
Mkuu; tusiilaumu sana Serikali(Japokuwa nayo inachangia/inahusika) ila sisi walaji tunayo tabia sugu ya kutokutaka au kujisumbua kujua mambo kwa undani au kusoma maelekezo ya mtengenezaji, ni nini hasa kilichomo (ingredients)kwenye hicho kinywaji ila tunadanganyika kirahisi mno na ladha ya sukari au kupuuzia yale yanayohusu Afya zetu ni hadi litukute jambo ndo tunashtuka. Hatukubali kwamba Mwili wetu ni kile tunachokula.
Aidha wazazi esp.akina mama utamkuta mama kambeba mwanaye na chupa ya juice eti anampenda mwanaye kwa kumnunulia hiyo juice.Hajiulizi hata kidogo kwamba ni shamba gani kubwa hivyo hapa Tz linauwezo wa kuzalisha embe, machungwa n.k. kwa mwaka mzima na kutosheleza waTz zaidi ya mil. 60???
 
Hatuilaumu serikali tunaikumbusha serikali kwamba kuna chanzo kipya cha mapato
 
Back
Top Bottom