Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,444
- 9,820
Ndugu zangu watanzania,
Napenda kuwataarifu ya kuwa serikali ya Rais Samia Inatambua Umuhimu na upekee wa Bandari yetu ya Dar es salaam,Inatambua kuwa bandari hiyo ndio moyo wa uchumi wetu,ndio mboni ya Taifa letu kiuchumi,ndio Uti wa mgongo wa mapato yetu,ndio usalama wetu wa Taifa kiuchumi,ndio jeuri yetu,ndio Tamanio la mataifa jirani,ndio kila kitu kwetu watanzania Kama Taifa.
Serikali ya Rais Samia inafahamu kuwa ukiichezea na kuitelekeza bandari hiyo Ni sawa na kuuchezea uchumi wetu na Taifa letu,inafahamu ya kuwa ukiihujumu au kuitikisa au kuitoa kafara au kuishusha au kutoipa jicho la umakini Ni sawa na kuhujumu uchumi wa Taifa letu,Ni sawa na kuiangamiza nchi Na Taifa letu.
Bandari ya Dar es alaam Ni mahali ambapo vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama kuanzia JWTZ ,TISS na POLICE lazima vielekeze macho ,masikio na hisia zao zote pale Bandarini,Ni lazima pajae na Kufurika majasusi wetu kila eneo walioapa kwa viapo vikali vya kutoa jasho na Damu kuipigania na kuifia nchi na Taifa letu pale itakapo bidi katika kulitetea Taifa letu na watu wake.Ni mahali ambapo vyombo vyetu havipaswi kulala hata sekunde moja pasipo kujuwa au kuwa na taarifa juu ya Nini kimeingia nchini au kinatoka nchini kupitia bandari yetu,vyombo vyetu vya Ulinzi vinatambua bandari yetu ikihujumiwa ni sawa na kulihujumu na kuliangamiza Taifa letu kiuchumi na kuhatarisha usalama wa Taifa letu pendwa.
Vyombo vyetu vya Ulinzi vinatambua kuwa hata majirani zetu wanaitazama bandari yetu kwa jicho la wivu mkubwa Sana na la Vita ya kijasusi katika uchumi ,kwa kutambua kuwa ukiishusha bandari hiyo unakuwa umeishusha Tanzania kiuchumi na Hivyo kuidhoofisha kiuchumi na hata kiusalama.Hivyo lazima watu wetu wa vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama viwe kazini muda na wakati wote kuhakikisha kuwa Bandari yetu Ni salama na haupenyezwi mkono wowote katika kujaribu kuihujumu.
Hivyo napenda kuwaambia watanzania wenzangu kuwa zipuuzeni taarifa za upotoshaji zinazoenezwa na watu wenye maslahi yao binafsi, Rais wetu pamoja na wasaidizi wake hawawezi wakaichezea Bandari yetu.Sote tunatambua uzalendo wa Rais wetu kwa Taifa letu na nchi yetu,ndio maana mh Rais ameteua na kuwa na washauri wabobezi na nguli katika nyanja zote waliomzunguka katika kumpatia ushauri wa kitaalamu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Rai yangu kwa wateule hasa mawaziri wote,Ni kuhakikisha kuwa wanakuwa wepesi kutoa ufafanuzi hadharani pale Jambo fulani linapokuwa limeleta sintofahamu katika jamii,lazima wawe wepesi wa kutoa maelezo ya kina yasiyo acha mashimo kwa wapotoshaji,kwa kufanya hivyo itasaidia kuzuia upotoshaji unaokuwa unaendelea na kuwachanganya na kuwapa hofu watanzania.kila mmoja kwa nafasi yake anapoona Wizara Yake imeguswa Ni lazima kutoka hadharani kutoa majibu,huo ndio uongozi,huo ndio utendaji,huo ndio uungwana na hiyo ndio njia ya kuliweka Taifa katika Hali ya utulivu na Amani.
Nawaombeni Sana viongozi wa serikali kufanya hivyo Kama ambavyo mh Rais amekuwa akiwasisitiza hadharani juu ya Jambo hili,msikae tu ofisini mpaka mkumbushwe na mh Rais au mpaka mambo yawe yamepotoshwa mpaka watu waanze kuamini upotoshaji kuwa Ni ukweli,fanyeni hivi kwa mambo yote katika kutoa ufafanuzi kwa wananchi ili kuziba mianya yote ya upotoshaji.
Elezeni kwa kina ,kwa vielelezo na Nyaraka muhimu katika kuwasilisha hoja zenu za ufafanuzi ,maana Rais wetu Ni muwazi na mwenye dhamira njema katika kuliongoza Taifa letu. Taarifa Zina nguvu na ili uwe na nguvu ni lazima uwe na Taarifa muhimu, wapeni Taarifa watanzania pale panapohitajika ili wengi waisemee serikali yetu kwa kurejea ufafanuzi wa serikali zidi ya wapotoshaji wachache.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.