Serikali imeshindwa kuzuia upandishaji nauli holela wakati wa sikukuu?

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Imekuwa ni kawaida kuona taarifa za ongezeko la nauli za usafiri hasa mabasi yanayosafiri mikoani, lakini Serikali mara zote imekuwa ikitoa matamko kadhaa lakini kiuhalisia hakuna mafanikio kivitendo.

Mfano ukienda Kituo cha Magufuli vilio vya nauli kupanda vipi tena kwa wingi, ninachojiuliza haya matamko ya Serikali inakuwa ni kutimiza wajibu tu kuwa nao wamezungumza au wanamaanisha kweli? Mbona kila mwaka mambo ni yaleyale yanajirudia?

Nimesoma sehemu leo kuwa miongoni mwa mabasi yaliyozidisha nauli ni kampuni ya Nazareti linalokwenda Iringa ambapo abiria wametozwa Sh35, 000 badala ya Sh 28,000.

Abiria mwingine Happy Muhagama amesema yeye amelipa Sh 40,000 kwenda Iringa badala ya Sh28,000 ambayo ni bei elekezi.
 
Achaa kuilaumu Serekali kwa vitu vya kijinga! Kwani mmelazimishwa wote msafiri December!!? Demand ikiwa kubwa,na bei lazima ipande!!
 
Serikali ni watu, na makampuni ya usafirishaji yanamilikiwa na viongozi au viongozi wa serikali wana maslahi yao kwenye hizo kampuni.
 
Back
Top Bottom