GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Akiwa katika kipindi leo katika T.V ya taifa TBC naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara ambaye pia ni mbuge wa Ukonga kupitia chama cha mapinduzi( ccm) amewapa onyo na tahadhali wamiliki wote wa shule za binafsi ambayo hawafuati utaratibu uliowekwa na serikali na kuanzisha sheria zao binafsi.
Akifafanua zaidi kiongozi huyo ametoa onyo kali kwa mmiliki yoyote wa shule binafsi atayepanga wastani wake kwa wanafunzi tofauti na ule wa serikali.
Nikimnukuu alisema " serikali peke yake ndiyo yenye mamlaka ya kuwapangia watoto wastani wa kutoka darasa moja kwenda darasa lingine sasa wewe mmiliki wa shule mamlaka hayo umeyapata wapi mpaka umfukuze mtoto shule eti kisa kashindwa kufikia wastani wako wa ajabu ajabu"
Mwita alienda mbali zaidi kiasi kwamba alitoa namba zake hadharani ili kama kuna mzazi yoyote atasumbuliwa na shule binafsi basi ampigie haraka iwezekanavyo ili aende kuwaonesha cha mtema kuni.
Pia mwita amepiga marufuku wamiliki wa shule binafsi kupandisha ada hovyo hovyo na kumrudisha mtoto nyumbani eti kisa ada.
Mwita amewataka wamiliki wote wasipandishe ada zao kipindi hiki mpaka hapo serikali itakapotoa ada elekezi kwa shule binafsi na ole wake mmiliki yoyote wa shule binafsi atakayekiuka agizo hili la serikali kwani hato sita kuifungia shule hiyo Mara moja bila kujali shule hiyo inamilikiwa na nani.
Akifafanua kuhusu kutatua uhaba wa madarasa kiongozi huyo ameeleza kwamba serikali imeamua kuanzisha utaratibu wa wanafunzi kuingia kwa zamu mashuleni kwa mtindo wa kupokezana madarasa yaani kuna wale watakaoingia asubuhi na wengine wataingia mchana. Na ili kuweza suala hili serikali imetenga zaidi ya bilioni 400 ili kusaidia utaratibu huo.
Ndugu mtanzania kama mwanao atarudishwa darasa au kufukuzwa shule kwa ajili ya ada. Au kama utapata usumbufu wowote kutoka kwenye shule binafsi na uliiokosa namba ya Naibu waziri ambaye ameitoa hadharani Leo asubuhi basi chukua namba hii 0767221344.
Kweli serikali hii ni sikivu sana na ipo kwa ajili ya wanyonge. Hongera Mwita waitara
=====
UPDATES; 10 Jan 2019
Dar es Salaam. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amepiga marufuku wanafunzi wa shule binafsi ambao hawajamaliza ada kusimamishwa au kufukuzwa shule.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Alhamisi Januari 10, 2019, jijini Dar es Salaam, Waitara amesema kuanzia kesho Ijumaa ataanza kupokea taarifa kutoka kwa katibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa halmashauri na wadhibiti ubora wa shule ambazo zimewafukuza au kuwarudisha wanafunzi.
Amesema ni marufuku mwanafunzi kusimamishwa au kufukuzwa shule kwa sababu ya kutolipa ada bila kujali anasoma shule ya umma au binafsi.
Waitara amesema jambo jingine ambalo Serikali haikubaliani nalo ni la wazazi kulazimishwa kulipa ada kwa mkupuo na iwapo hawajafanya hivyo wanafunzi hawataendelea na masomo hata kama mwaka uliopita walifanya hivyo.
"Nina sms (ujumbe mfupi wa maandishi) nilizotumiwa na wazazi wa shule ambazo zimerudisha wanafunzi nyumbani kwa kukosa ada na malipo mengine ya kiholela kama vile kulazimishwa kununua sare za shule shuleni, for figer, rim na madaftari ya ganda gumu (counter book),” amesema Waitara.
“Nataka maofisa elimu, wakurugenzi na makatibu tarafa kwenda kwenye hizi shule (anazitaja shule) hadi kufikia kesho niwe na majibu yanayoonyesha kupatikana ufumbuzi."
Waitara pia amewataka wazazi ambao watoto wao wamerudishwa kwa ajili ya kutolipa au kukamilisha ada wafike kwenye ofisi alizozitaja au Tamisemi kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Naibu waziri huyo amesema kuna haja ya kurudisha mjadala wa ada elekezi.
"Nafanya utaratibu kurudisha mjadala wa kuangalia namna ambavyo Serikali itatoa msimamo wa ada elekezi kwa sababu kuna shule zinatoza kuanzia Sh1.5 milioni hadi Sh6 milioni na zinasema zinatoa huduma," amesema Waitara.
Waitara amefafanua kama mazazi anaweza kulipa fedha yote hiyo kuna haja gani ya kupata mkopo chuo kikuu.
"Hili limekuwa changamoto kwa wanafunzi wengine wanaishi kwa ndugu wanaporudishwa inazua taharuki kwa wanafunzi na wazazi" amesema.
"Mtoto amesoma shule kwa miaka mitatu na kukamilisha michango yote, anaposhindwa haongezewi hata wiki moja badala yake anafukuzwa shule na mzazi hataki kukanyaga kabisa shule bila kuwa na risiti ya malipo," amesema
"Hili halivumiliki hata kidogo, wakibainika wanaofanya hivyo tutawachukulia hatua kwa sababu wao wanatoa huduma na hawalipi kodi na ninawakumbusha elimu inasimamiwa na Serikali" amesema Waitara