SERIKALI imeahirisha ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam hadi Chalinze yenye urefu wa kilometa 144 ya Expressway hadi miradi mingine ikamilike

Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Izack Kamwelwe amelieleza bunge kuwa Serikali imeahirisha ujenzi wa barabara kutoka DSM hadi Chalinze yenye urefu wa kilometa 144 hadi miradi mingine inayoendelea itakapokamilika. Barabara hiyo ilikuwa inajengwa kwa kiwango cha expressway #KwanzaHabari
D6M-1oEXoAAKvVN.jpg
Kwa hiyo ile haraka ya kuwabomolea watu ilikuwa ni chuki tu dhidi ya wachaga?
 
Sio kweli, tatizo sio fidia na wala haikua inapita huko unakosema, hiyo unayosema itakua kwenye miradi unayoisema wewe na sio ya serikali.

Ilikua ianzie mbezi hadi chalinze na Rais alilisema mara nyingi tu hata alipokua anazindua ujenzi wa flyover Ubungo.

Tatizo ni kua ilikha inatakiwa ifadhiliwe na benki ya Dunia, baada ya serikali ya wanyonge kujifanya wanajua Benki ya Dunia imejitoa, hakuna hela ndio serikali imejitutumua itajenga hadi kibaha.

Hizo stori za fidia kawape mataahira wenzako wasuojua.
Mbezi -Chalinze ni 144kms ? uwe unapitia maandiko ya budget za wizara kila mwaka ndio ungeelewa.
 
Kamandapole sana...bara bara unayo ongelewa siyo hiyo uliyoweka kwenye picha... hiii ya kwenye picha ni ya kimara-kibaha na inayo ongelewa ilikuwa inaanzia katikati ya jiji..
Ya kwenye picha sio express way ni ya kawaida na ni kilometa 19...
Pole kamanda kwa kuingia chaka kutokana na kutokujua kusoma vizuri...

Spin doctors at work!! Hiyo project ya kuanzia katikaji ya jiji ni wewe tu ndio unayeijua. Angalia hata husemi inatoka katikati ya jiji kwenda wapi. Come on, man - nilitaraji useme hakuna project inasimama. Point here is - kuna plans au project zinahirishwa. Period. Sasa tuambie hata hiyo yako inaahirishwa kwa sababu zipi!
 
Mda c mrefu ile stiglaz goji, na standadi goji zinaelekea kufa , hela imekata, chezea majizi wewe....Nyie wanyonge tulieni hivyohivyo....Hela Zenu zinaliwa na kina makondakta....ndo tunanunulia magari ya kifahari.....
 
Miaka ya 80 wakati barabara ya Morogoro kipande cha Magomeni hadi Fire inajengwa na Kajima daraja lilisombwa na maji. Walikaa almost two weeks bila kuendelea na ujenzi. Hakuna tangazo la kuahirishwa ujenzi lililotolewa.
Miaka 90 El-nino iliharibu barabara nyingi tu na ujenzi wake ulikuwa interrupted mara nyingi tu; hakukuwa na matangazo ya kuahirisha ujenzi.
Majuzi tu hapa daraja la Njiro kwenye barabara ya Afrika Mashariki Arusha lilisombwa na maji na ujenzi ukasimama siku kadhaa; hakukuwa na tangazo la kuahirisha ujenzi.
What is so special kwa ujenzi wa barabara hiyo hadi kutangazwe kuahirishwa ujenzi wake kwa sababu ya mvua?
Mbona kunamkandalas mbeya alijarbu kutoa utetez wa mvua mheshimiwa akasema barabara ikijengwa na mvua ndy inakua bora
 
Unanikumbusha event ya walokole waliokusanyia kiwanja cha ndege cha Dar es salaam wakiwa na Biblia kama passports na tickets zao, ungewauliza tu wanakwambia usidharau imani yetu maana Mungu atatenda!

Mkuu has walikuwa wasabato masalia..
 
Johana-mbatizaji muda mwingine unapenda kukurupuka na taarifa nusunusu....
Ujenzi umeahirishwa Kwa ajili ya mvua na si vinginevyo kutokana na mamlaka ya hali ya hewa walivyosema kuhusu mvua ndio maana ujenzi umesimama Kwa muda Tu Hadi pale mvua zitakapokoma.

Asanteniii
kwa sasa ujenzi unafanyika mpaka mailimoja[kibaha] mpango wa kwenda mpaka chalinze kwa sasa amna kutokana na uhaba wa fedha,
 
Johana-mbatizaji muda mwingine unapenda kukurupuka na taarifa nusunusu....
Ujenzi umeahirishwa Kwa ajili ya mvua na si vinginevyo kutokana na mamlaka ya hali ya hewa walivyosema kuhusu mvua ndio maana ujenzi umesimama Kwa muda Tu Hadi pale mvua zitakapokoma.

Asanteniii


acha upotoshaji.

mradi umesitishwa mpaka miradi mingine ikamilike ndo huo uendelee inshort fedha hakuna za kumalizia.
 
Alikuwa anaongeza praise team
Rudini mkasujudu kwa mabeberu..... Inasikitisha sana chicken head anapokuwa Ndiyo mwenye maamuzi.
Hivi unaanzaje mradi ambao hauwezi kuufanikisha?
Una buku jero halafu unataka kwenda Australia, kudadadeki
 
Back
Top Bottom