Serikali iko taabani kifedha

chishango

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
852
350
Wadau wakati huu halmashauri zote nchini zipo Dar es salaam kuwasilisha mipango ya bajeti ya 2013/14 lakini cha ajabu ni kwamba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2012/13 hazijaletwa wilayani hata senti moja yaani tunaandaa bajeti mpya wakati iliyopita haijatekelezwa na hii ni robo ya tatu ya mwaka wa fedha nashangaa sana alafu waziri wa fedha anajinadi bungeni kuwa uchumi unakwenda vizuri......kwa kweli tunaelekea kubaya wananchi wenzangu
 
Sijui lini serikali itapona kwa sababu kila siku tunaambiwa iko hoi
 
Sio siri tena kwani watumishi wa umma huwa wanalipwa mishahara tarehe arobaini na ngapi? waulize then utajua au kama vipi piga story za kitaa na jamaa wa hazina, hakuna cha epicol wala makolombwezo
 
CCM oyeee!!!!!

hoyeeeeee........or sorry njaa tu hiyo so nilikuwa napiga mwayo wakati nataka kucomment ndo ikanitoka hiyo salaamu.but usijali,only three years remaining.after then hii njaa itapungua.sio kwa sababu watakaokuja watanigawia chakula bure,no but ni kwa sababu ninaamini watajenga mazingira ya haki kwa sisi watz kugawana haka kakeki chetu bila upendeleo tofauti na sasa inavyoneemesha watu wachache wanaonunuliwa kukandamiza walahoi na maskini wa nchi hii.
 
wiki iliyopita imepelekwa barua kwenye taasisi zote za serikali kukatwa hela kwenye bajeti zao kusaidia gharama za tanesco na sensa,jumla ya fedha iliyochukuliwa na hazina ni bilioni 100,..nikajiuliza hizi fedha kweli ni za shuguli hizo au kuilipa dowans na shughuli za ccm za juzi?dah,nchi inaliwa na haya maccm vibaya sana
 
Sikuizi mishahara wanalipa tarehe 37 kila mwezi huu ni utaratibu mpya kutoka kijiji cha Msoga Bagamoyo.
 
Pesa zinatumika kuzidi bajeti halafu serikali inapeleka bungeni kuhalilisha matumizi kumbe pesa zimeshaliwa.
Watanzania hawajui kuwa bado Bunge ni rebber stamp CCM ojee.................
 
Sio siri tena kwani watumishi wa umma huwa wanalipwa mishahara tarehe arobaini na ngapi? waulize then utajua au kama vipi piga story za kitaa na jamaa wa hazina, hakuna cha epicol wala makolombwezo
Serikali gani mnayoizungumzia hapa?Nijuavyo mimi Tanzania hakuna serikali ila genge la walanguzi wa madaraka na waamrisha polisi kuua ili kuwazima watu midomo!Kuna serikali yoyote Duniani inayoweza kuwa haina mitaala ya Elimu?Inaibia pesa za watu wake yenyewe?Inaibiwa wanyama hai mbugani?ooh Mjomba nhaule kanhyi vyono ukubwabwa nkhani swanuswanu ntavivyo!!!Kaah unamahala mzelelo..Mbukwenyi alee????
 
Wadau wakati huu halmashauri zote nchini zipo Dar es salaam kuwasilisha mipango ya bajeti ya 2013/14 lakini cha ajabu ni kwamba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2012/13 hazijaletwa wilayani hata senti moja yaani tunaandaa bajeti mpya wakati iliyopita haijatekelezwa na hii ni robo ya tatu ya mwaka wa fedha nashangaa sana alafu waziri wa fedha anajinadi bungeni kuwa uchumi unakwenda vizuri......kwa kweli tunaelekea kubaya wananchi wenzangu
priority -- tunajenga mji mpya wa kisasa Kigamboni 12trilion.
 
kwasababu katiba haitamki sasa hii ijayo basi iseme mishahara iwe ni ndani ya siku30 ..kama ni tar26jan na fbr isizid26
 
kwasababu katiba haitamki sasa hii ijayo basi iseme mishahara iwe ni ndani ya siku30 ..kama ni tar25jan na fbr isizid25
 
kwasababu katiba haitamki sasa hii ijayo basi iseme mishahara iwe ni ndani ya siku30 ..kama ni tar26jan na fbr isizid26

Naunga mkono na kama itachelewa zaidi ya tarehe 28/30/31 kutegemea na mwezi husika, Wafanyakazi waitoze serikali riba ya 2% kwa kila siku iliyocheleweshwa, labda hii serikali SIKIVU itapata masikiao ya KUSIKIA!
 
Bora akina Mkwawa ambao hawakawa wamesoma elimu ya darasani kuliko hawa wanaopenda kujiita Dkt.
 
Wadau wakati huu halmashauri zote nchini zipo Dar es salaam kuwasilisha mipango ya bajeti ya 2013/14 lakini cha ajabu ni kwamba fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka 2012/13 hazijaletwa wilayani hata senti moja yaani tunaandaa bajeti mpya wakati iliyopita haijatekelezwa na hii ni robo ya tatu ya mwaka wa fedha nashangaa sana alafu waziri wa fedha anajinadi bungeni kuwa uchumi unakwenda vizuri......kwa kweli tunaelekea kubaya wananchi wenzangu

.
Hii nchi inaendeshwa kisanii. Sasa umefika wakati wa Mungu kuanika maovu yao yote yajulikane mpaka kwa ma-house girl. Wizi wao umefika kikomo na walichoiba hawatakuwa na mahali pa kukila. Ni full hofu mpaka kaburini, watakimbia wasijapofukuzwa na tamaa yao itakuwa ni kutoa roho.
.
 
Budget ya mwaka 2012/2013 wameshindwa kutekeleza tasisi nyingi na halmashauri ziko hoi kifedha,bungeni wanacheza tu nchi inaaangamia.
 
Back
Top Bottom