Serikali ikae na viongozi wa waalimu kujadili matatizo yao,vitisho si suluhu. .

Tikerra

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
1,702
146
Mawaziri wa elimu Ndg.Jumanne Maghembe na Utumishi Hawa Ghasia wametoa tamko la pamoja wakisema kwamba mgomo wa waalimu ambao utafanyika takriban wiki mbili zijazo si halali,kwa vile matatizo mengi ya waalimu yameshatatuliwa. Kwanza kwa kusema 'mengi' ina maana mengine bado hayajatatuliwa,kwa hiyo waalimu bado wana haki ya kugoma kama wakitaka kufanya hivyo,kwa vile kugoma ni haki yao ya msingi ili mradi wafuate sheria.Jambo la kwanza la msingi ni kwamba serikali ikumbuke ina wajibu katika mambo mengi yawahusuyo wafanyakazi wake wote,wala sio waalimu peke yao.Linalo onekana sasa ni wafanyakazi kugawanywa katika makundi, waalimu na wasio waalimu,hii ni makosa kabisa.Hao wengine wasio na mtetezi awatetee nani? Au serikali sasa inaanza kutumia ule mkakati unaotumiwa na watu waliofirisika kimawazo wa 'divide and rule'.Kama sivyo basi tunaiomba serikali ihudumie wafanyakazi wake wote 'equally.' Kama wote wana madai basi walipwe wote vinginevyo tutaanza kuleta hisia mbaya kwa wafanyakazi wetu.La pili ni kwamba, kuwatishia waalimu haitasaidia sana.La msingi hapa ni kwamba serikali itekeleze wajibu wake kwa wafanyakazi wote.Wafanyakazi wana matatizo mengi,huduma duni za afya,maslahi duni,ukosefu wa vitendea kazi,makazi duni,mazingira mabovu ya kufanyia kazi nakadhalika.Sasa bila serikali kutatua matatizo haya isidhani iko salama.Sawa inaweza ikafanikiwa kwa kutumia nguvu za dola kuzima huo mgomo,lakini haitafanikiwa kuzima migomo baridi.Na hii ni mibaya zaidi kwa vile italimaliza taifa polepole.Ni vema basi serikali ikakaa na viongozi wote wa wafanyakazi ili kupata 'plan of action' ambayo itakubalika na pande zote mbili.
 
Back
Top Bottom