Serikali ifuteni Congo DRC kwenye mfumo wa Forodha (Single Custom Territory) - Nchi Inapata Hasara

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
897
715
Ni mfumo wa kiforodha unaohusisha mamlaka za kodi za nchi wanachama wa Afrika Mashariki katika usimamizi wa mizigo mbalimbali inayoingia na kutoka katika nchi wanachama ..Mfumo unahusisha waagizaji kufanya utaratibu wa utoaji mzigo ktk nchi zao na kulipia ushuru na kodi zote mzigo ukiwa bado haujatolewa ktk bandari .

Kongo DRC ni mteja mkubwa wa uagizaji na usafirishaji wa shehena kubwa za mizigo kupitia Bandari za Dar es salaam-Tanzania,Mombasa-Kenya,Beira-Msumbiji,Welvis Bay-Namibia na Durban -Afrika Kusini,Lobito-Angola kwa miaka nenda rudi ikichagizwa na mapana ya kijiografia na rasilimali

Kongo DRC amekaribishwa katika mfumo wa forodha wa SCT ili kuisaidia kusimamia mapato yake .Lakini mapana ya madhara ya kuikaribisha Kongo hayawaumizi Rwanda,Burundi,Uganda ama hata Kenya sababu ya strategic position Jimbo la Katanga lenye utajiri wa rasilimali madini na misitu.

Mamlaka ya usimamizi wa kodi na mapato ya Kongo {OFIDA} imefungua ofisi zake katika nchi wadau wa SCT ikiwamo Dar es salaam-Tanzania.Historia yaoshesha hakuna urafiki kati ya walipa kodi na wasimamia kodi hasa ktk nchi zinazoendelea sababu ya rushwa na ufisadi wa watumishi wa mamlaka za kodi na wafanyabiashara.

Madhara ya kuihusisha Kongo DRC ktk mfumo wa SCT yamepelekea ucheweleshaji wa utoaji wa mizigo ya wateja sababu ya mapungufu ya mfumo husika kiutekelezaji ,kiusimamiaji na maandalizi yenye mapungufu mtambuka hivyo kuongeza gharama maradufu katika uondoshaji wa mizigo kupitia bandari zetu hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wateja na mawakala wao.Lakini pia wateja kulazimika kulipa ushuru mkubwa tofauti na awali kwa kuepuka malumbano kikodi yanayochukua muda mrefu huku gharama mtambuka za uhifadhi mizigo yao ikiongezeka ktk hifadhi za bandari.


Hili limekuwa msingi wa wateja wengi toka Congo DRC kuanza kuikimbia kutumia milango bahari inayofungamana na nchi za Afrika mashariki {SCT} hivyo kukimbilimbilia ktk nchi zisizofungamana kiforodha na Congo DRC.

Tayari idadi ya mizigo yakiwemo magari yanayopita bandari ya Dar es salaam imepungua kwa zaidi ya asilimia 15 ktk miezi michache iliopita na uthibitisho upo kupitia kuthibitishwa na utupu ktk bandari kuu na kavu kama Farion,TALL,Chikasa,Silver,Hesu n.k

Jitihada kubwa zinazofanywa na Serikari ya JPM ktk kurestructure na ku reform bandari yetu na mamlaka za kodi matunda yake yanaweza yasiwe na tija tarajiwa kwa manufaa ya taifa.Hatua stahiki zichukuliwe kwa kuifuta Congo DRC katika mfumo husika sababu ni kikwazo kwa jitihada za kuongeza mapato kwa nchi yetu kupitia fulsa malidhawa .
 
imeandikwa kitaalamu sana ntarudi badae nikajisomee kwanza.
 
heri tumpa kagame bandari.....maana karibu watumishi wote wa umma tanzania ni wezi
 
Mkuu hueleweki,unalalamika au unatoa ushauri - wewe ni raia wa Nchi gani Afrika Mashariki na kati?

Wewe unataka kutuamanisha kwamba mfuno wa kielekitronic/digitali haufai au? Hapa unaleta vitisho baada ya kuona ujanja wenu umefikia tamati,kama unaona Badari ya Dar haikufai kwa nini uhamii Bandari nyingine kimya kimya bila ya kutuletea propaganda zako zisizo na mshiko.
 
Kwa nini wafutwe, wewe ni mpelezi wa Kagame nini? au ni Mpiganaji wa M23.

Solution si DRC ifutwe bali wapange upya viwango vya tozo. Tumekua tukisikia kua waagizaji wa kubwa wa bidha kupitia Bandari ya Dar Es Salaam ni pamoja na wa Kongomani sasa wakifutwa je inchi yako itapata wapi wateja?

Tatizo myanya ya rushwa imefungwa na JPM, sasa mnatafuta mchawi. Ni mara ngapi mumewaibia wa Kongo makontena yao? Jiulize kwa nini walikaribishwa? kama kuna ongezeko la kodi na mnahisi watu hawatumii tena bandari ya DSM kwa nini msilipeke hilo swala katika mamlaka usika?

Sasa nashindwa kuelewa, tumuamini nani kati yako na JPM. Hivi karibuni zaidi ya makontena 300 yamepita bila kulipa Kodi, PM alipofuatilia amegundua zaidi ya makontena 2000 yalipita bandari ya DSM bila kulipa kodi sasa hapo nani mchawi? wa Kongo au ni wewe ambaye unataka kutuaminisha kua wa Kongo ndo wamesababisha wateja waikimbie Bandari ya DSM.

Wafanya kazi wa bandari walikiri mbele ya PM kua mizigo inayopita hapo ni mingi sasa wewe umekuja na takwimu zako kua mizigo imepungua.

Umeanza kuisona namba nini?
 
Bandari kwa sasa wacheze mpira wao angali wakijua kabisa kwamba waliingizwa mkenge kwasasa magari wanashushia afrika ya kusini wanapakia hadi la zimbambwe chirundu wanayatembeza hadi kwao, sisi tunabakia kusema kama ujalipa kodi uko kwenu atukupatii ngari yako, kwanini wasifanye wajapan hivyo? Tufanye siye malofa? Unamnawisha wenzio uso angali wakwako ni mchafu?
 
kwa hiyo tuwatoe kongo kwenye mfumo ili wafanyabiashara wakongo iwe rahisi kukwepa kodi ya serikali yao na waje sana bandari ya dsm kupitisha magendo..

kuonesha hatutaki wezi ndio maana tumewaingiza kongo kwenye mfumo na tumeipa ofisi Revenue Authority ya congo ndani ya bandari yetu ili iwe rahisi wa kukusanya ushuru wao wa transit zao. na kuepusha dumping kwenye nchi yetu...

so ni mwendo wa kuisoma namba tu kama ulikuwa unajifanya mkongo mani unaleta kontena unazuga ni la congo then unalitoa bure unaenda lishusha kibamba na kushusha mzigo.. siku hizi hakuna hiyo.. ushuru wa kongo unakusanywa humo humo bandarini na wakongoman wenyewe wakisaidiana na Tra..

mfumo mmoja hakuna short cut
 
Ni kweli mfumo huo ulianzishwa bila kufanya utafiti wa kina hasa kwa upande wa Drc.Mifumo ya taasisi nyingi za umma nchi humo haiendani na hitaji la utaratibu huo.Kwa mfano sasa hivi mzigo ukipakiwa Dsm gari linaweza chuku zaidi ya wiki moja likisubiria karatasi zilizotumwa Congo kufanyiwa verification na mamlaka za kodi nchini humo.Tatizo hili ni kubwa hasa kwa mizigo inayopitia bandari ya Kigoma.
 
kwa hiyo tuwatoe kongo kwenye mfumo ili wafanyabiashara wakongo iwe rahisi kukwepa kodi ya serikali yao na waje sana bandari ya dsm kupitisha magendo..

kuonesha hatutaki wezi ndio maana tumewaingiza kongo kwenye mfumo na tumeipa ofisi Revenue Authority ya congo ndani ya bandari yetu ili iwe rahisi wa kukusanya ushuru wao wa transit zao. na kuepusha dumping kwenye nchi yetu...

so ni mwendo wa kuisoma namba tu kama ulikuwa unajifanya mkongo mani unaleta kontena unazuga ni la congo then unalitoa bure unaenda lishusha kibamba na kushusha mzigo.. siku hizi hakuna hiyo.. ushuru wa kongo unakusanywa humo humo bandarini na wakongoman wenyewe wakisaidiana na Tra..

mfumo mmoja hakuna short cut
Kwani hizo chek poit zimetapakaa tuka dar mpaka tunduma zinakazi ngani mpaka mzigo ushukie kibamba, watu wengine pumba kweli kweli
 
Ni kweli kuna tatizo kuhusiana na mfumo huu ambao nadhani utafiti wa kutosha haukufanyika has kwa upande wa pil.
Mfano sasa hivi gari inayopakia mzigo wa kwenda Congo inabidi isubirie karatasi zilizopelekwa nchini humo kufanyiwa verifiacation na mamlaka za kodi nchini humo.
 
Kama mfumo haufai ni kuomba mamlaka husiku ziuboreshi tu, ila haya mawazo ya kuitoa Congo kwenye SCT ni ulaghai tu, kwanza kwa nini mnang'ang'ania Congo tu na si Rwanda au Uganda ?
 
hii ni propaganda haina kichwa wala miguu mada yote utter garbage!!!
 
Wapo walioelewa na wachache wasiolewa,Nadhani mtoa hoja ana sababu za msingi zenye kuzingatia maslahi ya nchi.Mamlaka ya bandari inatumia zaidi ya bilioni 2 kila mwaka kuvutia wateja kutumia bandari za Tanzania..

Mfumo tajwa una mapungufu kwa kiwango cha kuwakwaza TPA,TRA,CFA-Tanzania,CFA-DRC,ICD's,VFS,OGEFREM,TAFFA na zaidi sana Wateja {Importers} tokea Kongo..

Kwa nini sio Rwanda,Burundi,Uganda,Kenya? Mifumo yao ya kiforodha imeboreshwa kabla ya kujiunga na SCT System,Pili Mapana ya uagizaji wa mizigo ni kwa kiwango kidogo ukilinganisha na DRC,Tatu Kuzingatia udogo wa nchi husika ni rahisi kuelimisha kwa wakati.

Mapana ya hasara japo mwenye mada hakwenda ndani zaidi yanahusisha pia vijana wetu wafanyakazi ktk makampuni ya forodha,madereva,mama lishe,na wengine toka ktk sekta tegemezi kuathirika kwa namna moja ama nyingine kutokana na kupungua kwa mizigo hususani magari na siku si nyingi makontena...Wengi kukosa ajira na kipato hivyo umaskini mpevuko.

Pia bandari kavu nyingi zitafungwa kwa sababu automatically bandari kuu itajikuta ina nafasi kubwa za kuhifadhi mizigo kwa sababu ya mizigo kupungua..

Tunawahitaji sana Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo na kuwafuta ktk mfumo husika hakumaanishi kuwafukuza bali kuwa encourage zaidi kuitumia bandari yetu na bandari zetu kwa ujumla. Nadhani mtoa hoja amemaanisha turudi kwenye mfumo wa zamani ambao kimsingi ni salama zaidi kwa nchi sababu utoaji mizigo unahusisha mawakala wa forodha kuwa responsible kuhakikisha mzigo unafika unakotakiwa kufika.

Naunga mkono hoja..mamlaka husika zifanyie kazi ushauri na ku reseach mapana yake
 
Wapo walioelewa na wachache wasiolewa,Nadhani mtoa hoja ana sababu za msingi zenye kuzingatia maslahi ya nchi.Mamlaka ya bandari inatumia zaidi ya bilioni 2 kila mwaka kuvutia wateja kutumia bandari za Tanzania..

Mfumo tajwa una mapungufu kwa kiwango cha kuwakwaza TPA,TRA,CFA-Tanzania,CFA-DRC,ICD's,VFS,OGEFREM,TAFFA na zaidi sana Wateja {Importers} tokea Kongo..

Kwa nini sio Rwanda,Burundi,Uganda,Kenya? Mifumo yao ya kiforodha imeboreshwa kabla ya kujiunga na SCT System,Pili Mapana ya uagizaji wa mizigo ni kwa kiwango kidogo ukilinganisha na DRC,Tatu Kuzingatia udogo wa nchi husika ni rahisi kuelimisha kwa wakati.

Mapana ya hasara japo mwenye mada hakwenda ndani zaidi yanahusisha pia vijana wetu wafanyakazi ktk makampuni ya forodha,madereva,mama lishe,na wengine toka ktk sekta tegemezi kuathirika kwa namna moja ama nyingine kutokana na kupungua kwa mizigo hususani magari na siku si nyingi makontena...Wengi kukosa ajira na kipato hivyo umaskini mpevuko.

Pia bandari kavu nyingi zitafungwa kwa sababu automatically bandari kuu itajikuta ina nafasi kubwa za kuhifadhi mizigo kwa sababu ya mizigo kupungua..

Tunawahitaji sana Nchi ya Kidemokrasia ya Kongo na kuwafuta ktk mfumo husika hakumaanishi kuwafukuza bali kuwa encourage zaidi kuitumia bandari yetu na bandari zetu kwa ujumla. Nadhani mtoa hoja amemaanisha turudi kwenye mfumo wa zamani ambao kimsingi ni salama zaidi kwa nchi sababu utoaji mizigo unahusisha mawakala wa forodha kuwa responsible kuhakikisha mzigo unafika unakotakiwa kufika.

Naunga mkono hoja..mamlaka husika zifanyie kazi ushauri na ku reseach mapana yake..
Wasemaji wa TAFFA,TPA na TRA wanaweza kuwa na ufafanuzi zaidi..
 
Mfumo si mbaya ikiwa nchi washiriki zitakuwa na udhati wa kusimamia,Kuutumia na kutekeleza matakwa ya mfumo husika sawa na maono,msingi,Matokeo na matalajio.Tukumbuke mfumo husika uliasisiwa mahsusi kwa ajili ya nchi zilizopo kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo kimsingi zilifanya maandalizi ya kutosha kuingia na kuutumia mfumo husika ktk kufanikisha biashara baina ya wafanyabishara wa nchi wanachama kwa kuondoa vikwazo lukuki vya kibiashara na kupunguza gharama za ufanyaji biashara katika nchi za EAC.Lakini pia mfumo husika ndio barabara ya lami kuelekea EAC Custom Union {Country intergration Highest stage}.

Sio kwamba hatupendi Serikari ya Kongo wakusanye kodi zao kupitia uagizaji unaofanywa na wafanyabiashara wao ama makapuni yao la hasha...Tunapinga ukiritimba,ubabaishaji ,ubabe na urasimu mkubwa unaofanywa na maofisa wa kodi wa kongo {OFIDA} hasa waliopo Dar es salaam kwa walipa kodi wao na kufanya bandari zetu zichukiwe na kukimbiwa zaidi Nchi yetu ichukiwe kwa kudhaniwa ndio kikwazo cha uharakishaji ktk kutoa mizigo yao.

Maofisa hawa wakiongozwa na Ndugu Peter Morisho wamekuwa kiini cha tatizo la bandari yetu ya Dar es salaam kukimbiwa ,Wamekuwa wakifanya mengi yakiwemo utengenezaji wa mazingira ya rushwa toka kwa wafanyabiashara/Mawakala wa Forodha wa Kongo na Tanzania kwa kukwamisha uhakiki nyaraka/upitishaji nyaraka za mizigo na utumaji wa taarifa za uhakiki kwa mtandao kwa wenzao Kongo ili ukamilishaji wa mchakato wa kutoa mizigo.Ucheweleshaji huu umekuwa ukifanywa mahsusi kwa manufaa yao binafsi maofisa na si serikari yao.

Mazingira ya rushwa yamekuwa yakijengwa yakihusisha maofisa wa Mamlaka ya kodi ya Kongo {OFIDA-Waliopo Dar es salaam na Kongo},mawakala wa forodha wa Kongo na baadhi ya ICD'S au Vehicle Freight Stations {Rejea faida ya biashara ya ICD'S,VFS ni storage charges} kwa kufanya mbinu nyingi kuhujumu mfumo husika na kusababisha ucheweleshaji wa uondoaji wa mizigo ya wateja husika toka bandari ya Dar es salaam licha ya wafanyabiashara kulipa kodi stahili ambazo yamkini sizo zinazofika serikarini.Moja ya mbinu inayofanywa ni kuhakikisha mizigo husika haionekani kwenye mfumo husika hivyo kutengenezewa nyaraka kama mizigo inayotekea SADC au Tanzania na si Ulaya,Asia au Amerika.

Mazingira ya urasimu na rushwa pia yamekuwa yakihusisha uthaminishaji wa thamani ya mizigo husika ili kughamua kiwango cha kodi kinachostahili kulipwa na mwagizaji.Katika mchakato huu hutokea malumbano na vuta nikuvute kati ya thamani inayowakilishwa na mwenye mzigo {Mwagizaji} dhidi ya mamlaka ya Kodi ya Kongo {OFIDA} ,zoezi hili huchukua muda kuhitimishwa ikiwa mteja atasimamia kweli anayoamini ikiwa kuna kadilio la juu {Uplift}.Ikumbukwe kuwa wakati haya yakiendelea mzigo bado upo bandarini na grace period haizidi siku 14 [kipindi cha kuutoa pasipo gharama za ziada}.Baadhi ya makampuni ya uwakala wa forodha toka Kongo yametuma wawakirishi wao mahsusi kwa ajili ya kusimamia michakato ya kodi dhidi ya mizigo ya wateja wao.

Mizigo inapochelewa kuondolewa bandarini gharama za kuiondoa huongezeka sana na maradufu kutegemeana na siku zilichochelewa kuondoshwa na gharama hizi uongezeka na kuwa kubwa kwa kiwango cha wenye mali/mizigo kushindwa kuigomboa hivyo kusababisha kupigwa minada,usumbufu mkubwa,hasara kubwa sana na chuki kubwa sana dhidi ya bandari yetu japo kuwa sababu za ucheweleshaji si za bandari yetu bali mamlaka za kodi za nchi husika.

Kwa nini wanakimbilia bandari zingine nchi nyingine,Kuepuka gharama kubwa, hasara,Ucheweleshaji mkubwa wa mizigo kufika {refer essence of time in commercial transactions} na usumbufu mkubwa wanaoupata kwa kupitisha mizigo yao ktk bandari ya Dar es salaa/Tanga/Tanganyika..Wafanyabiashara wameanza kuagiza shehena za mizigo kupia bandari zilizoko kwenye nchi zisizofungamana kiforodha na Kongo DRC mfano Msumbiji,Namibia,Angola na Afrika ya kusini.

Kwa kuzingatia ukubwa wa Kongo kijografia,mapana ya uwekezaji ktk uvunaji wa rasilimali zake na ujenzi wa miundombimu ..bado Kongo ni mteja mkubwa sana tunaemhitaji sana sasa na baadae hivyo hatupaswi kupoteza fursa za kibiashara zilizopo.Madhara ya hili zoezi ni makubwa sana kwa nchi ikiwa hatua stahiki hazitachukuliwa kwa wakati na wenye mamlaka na nia njema na Nchi yetu.

Mungu ibariki Afrika..
 
Back
Top Bottom