Serikali ianzishe somo la Mahusiano na mapenzi shuleni

MWALIMU DAIMA

Senior Member
Mar 4, 2023
130
263
Habari za usiku Wana Jf hope wote ni wazima poleni na majukumu ya kujitafutia riziki,

Niende kwenye lengo la Uzi,

Napenda kushauri serikali yangu na wadau mbalimbali kuwa ni Wakati sasa sahihi kuanzishwe na somo la mahusiano na mapenzi katika mfumo wetu wa elimu, kuanzia level ya primary hadi vyuo vikuu, tena somo hili litiwe mkazo mkubwa sana na liwe somo la lazima.

Kwanini nasema hivi Wana jukwaa
Kwasasa Jamii ya TANZANIA inapita katika mkwamo mkubwa katika eneo hili la mapenzi na mahusiano, vijana wengi walio opo vyuo vikuu wanasumbuliwa na mapenzi, wafanyakazi maofisin kuanzia walimu, madaktari na kadharika wanakubwa na mateso makubwa katika eneo la mahusiano na mapenzi, wenye ndoa na wasio na ndoa Yan kiufup hili suala limekuwa ni janga,

Afya za vijana Wengi sana hasa afya akili zinadhoofika Kila siku moja ya chanzo ni mahusiano na mapenzi, vijana Wana ingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya wengine pombe, wengine wanaacha masomo, wengine wanafikia hatua ya kuuaana, moja ya SABABU ni mapenzi.

Ombi langu serikali itazame hili suala kwa upana mkubwa ili tuokoea taifa letu na vijana wetu katika janga Hili,
Na silaha kubwa ni kuanzishwe somo la mapenzi na mahusiano kwan mapenzi na mahusiano yanagusa sehemu kubwa sana na ni topic ndefu mno. Vijana wajua how to handle heart break na vitu kama hivyo.

Samahani wakuu mm sio mzuri kwenye uandishi mtanisamehe,

Ni Mimi mwalimu mtarajiwa
@ mwalimu daima
 
Hivi kwa mindset kama hii kwa nini mpwayungu village asiwakosoe,

Kuna vipaumbele vingapi ambavyo vingeweza kutoa taifa sehemu moja kwenda nyingine. Aisee! Ndio nyie mnaotuharibia vijana wetu sio bure!!

Na hivi ni kwanini muafrika akili yako imelala kwenye mapenzi sana kuliko kitu kingine chochote. Kwa taarifa yako ukiona mtu mweupe kitu chochote hakipi kipaumbele basi ni bora uachane nacho maana alishakifikiria na akaona hakina faida.

Halafu na wewe unajiita msomi humu JF kweli?

This nonsense ondoa haraka sana broh!
 
Umewaza mbali sana bro,,, Log,
nusu mara kimo mara kitako,
umri wa juma ni mara nne ya Asha,
charles Darwin,
Vasco Da Gama
havina umuhimu mkubwa sana kwenye maisha ya msukuma na mnyakyusa

Mitaala ya elimu iwasaidie watu kujikomboa kutoka kwenye shida tulizonazo sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom