Serikali haitakwamisha wafanyabishara na wawekezaji

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
741
479
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji (Mb.) amesema Serikali ya Awamu ya Sita haiko tayari kuwakwamisha wafanyabiashara na wawekezaji kushindwa kufikia malengo yao bali itawasaidia kukua na kuendelea kibiashara, kukaa kwa pamoja na kutatua changamoto zao ili kuhakikisha ufanyaji biashara wao unakuwa na tija na manufaa kwa Taifa .

Amesema hayo Agosti 1, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vishikwambi cha Tanztech kilichopo jijini Arusha kwa lengo la kujionea uzalishaji huo na kusikiliza changamoto zao.

Aidha Dkt. Kijaji amesema ameridhishwa na uwekezaji huo ikiwa ni hatua ya kutatua changamoto ya matumizi ya Vishkwambi katika shule za awali na zile za sekondari ambapo vitasaidia kufundisha wanafunzi namna bora ya kutumia TEHAMA katika mitaala ya elimu

Naye Mkurugenzi wa Kiwanda hicho cha Tanztech Bw. Gurveer Hans amesema Kiwanda hicho kipo tayari kushirikiana na Serikali katika kutoa bidhaa hiyo mashuleni na kwa watu binafsi kwa bei nafuu.View attachment 2706154View attachment 2706153
20230802_114525.jpg
 
Back
Top Bottom