Serikali haiko makini na ndio maana watu wanaendelea kuangamia kwa ajali

lengume

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
318
134
Hivi majuzi nikiwa nchini Kenya nimeshughudia magari yote ya abiria yakiwa yamefungwa speed gavana. Speed ya mwisho gari kutembea ni 80. Sasa Tanzania inaonyesha mwisho wa speed ni zote ambazo gari inazo. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali yetu isivyojali maisha ya Watu wake.

Leo hii Magari yamegongana huko Musoma na watu 36 wamepoteza maisha na wengine 79 kujeruhiwa. Cha ajabu Serikali haitachukua hatua yoyote kuhakikisha ajali zinapungua. Tunaomba Serikali iangalie tena huu usafirishaji wa abiria kwani watanzania wanaangamia na wataendelea kuangamia kama hatua sahili hazitachukuliwa. Mimi naishauri Serikali ifunge spidi Gavana kwa mabasi yote. Na kusuka upya Jeshi la polisi (Trafic) kwani wengi wao wako Barabarani kwa ajili ya kula rushwa. Serikali ikifanya hivyo tunaweza kupunguza ajli za Barabarani.

Mungu Atusaidie sana.
 
Mimi Sidhani tatizo speed mkuu, nafikiri waafrika tuna matatizo makubwa sana kichwani sijui niseme ignorance, ingekuwa speed Germany ajali zingekuwa kila siku, angalia hata barabara zetu unakuta matuta ya kufa mtu inamaanisha wanaoendesha magari wana matatizo makubwa vichwani lakini nakuunga mkono serikali pekee ndio yenye uwezo wa kuwashika adabu madereva wa hovyo.
 
Matuta ni moja ya vyanzo vya ajaili nyingi nchini, kwakuwa sehemu nyingi yamewekwa na alama za kuonesha uwepo wake zimeng'olewa. Lakini pia matuta hayo hayapo standard kwa maana ya kutotengenezwa kwa kuzingatia aina za magari yaliyopo kwa mfano kuna maeneo matuta ni makubwa sana kiasi cha magari yaliyopo chini sana kukwaruza matuta na hata kushindwa kupita kabisa (eg Nyololo Mufindi)

Shida nyingine ni rushwa imekithiri sana hasa katika kupata leseni, makosa ya barabarani ambayo imetanjwa kuwahusisha askari wa usalama barabarani mpaka maafisa wa ngazi za juu ndani ya kikosi hicho
 
ongeeeni vyote ila mjue kuna maroho ya ajali na kama watu haamini basi hapo mashetani ndipo yanapo kunywa damu
 
Hao tunawaita viongozi wapo busy kuchakachua katiba na kuwachafua wapinzani, mi nafikiri ni wakati muhafaka wa wananchi kuchua hatua kali dhidi ya madereva walio na pupa barabarani tukisema tulie na hii mijitu tunayoiita viongozi hakuna lolote bz kwanza haya mabasi mengine ni ya kwao au kama sivyo wanashare kiasi fulani, so jamani watanzania tuamkeni maneno matupu hayavunji mfupa.
 
Hivi majuzi nikiwa nchini Kenya nimeshughudia magari yote ya abiria yakiwa yamefungwa speed gavana. Speed ya mwisho gari kutembea ni 80. Sasa Tanzania inaonyesha mwisho wa speed ni zote ambazo gari inazo. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali yetu isivyojali maisha ya Watu wake.

Leo hii Magari yamegongana huko Musoma na watu 36 wamepoteza maisha na wengine 79 kujeruhiwa. Cha ajabu Serikali haitachukua hatua yoyote kuhakikisha ajali zinapungua. Tunaomba Serikali iangalie tena huu usafirishaji wa abiria kwani watanzania wanaangamia na wataendelea kuangamia kama hatua sahili hazitachukuliwa. Mimi naishauri Serikali ifunge spidi Gavana kwa mabasi yote. Na kusuka upya Jeshi la polisi (Trafic) kwani wengi wao wako Barabarani kwa ajili ya kula rushwa. Serikali ikifanya hivyo tunaweza kupunguza ajli za Barabarani.

Mungu Atusaidie sana.

Mimi naunga mkono hoja, kuwa serikalri lazima ijipange kuzibiti hizi ajali barabarani! na serikari inajukumu la kuhakisha inakomesha kabisa hizi ajali barabarani, pia tunatakakuona serikari inachukua hatua stahika ktk kukomesha ajali barabarani. Na sisi kama wananchi tuta pima na kuona ni jinsijani serikari imechukuwa hatua ya kulimaliza hili tatizo la ajari barabarani! maana inatisha sana mtu ukisikia tu swala la safari unaka roho ju kwa nini hali hi, nawakati swala hili linaweza kudhibitiwa.
 
Matuta ni moja ya vyanzo vya ajaili nyingi nchini, kwakuwa sehemu nyingi yamewekwa na alama za kuonesha uwepo wake zimeng'olewa. Lakini pia matuta hayo hayapo standard kwa maana ya kutotengenezwa kwa kuzingatia aina za magari yaliyopo kwa mfano kuna maeneo matuta ni makubwa sana kiasi cha magari yaliyopo chini sana kukwaruza matuta na hata kushindwa kupita kabisa (eg Nyololo Mufindi)

Shida nyingine ni rushwa imekithiri sana hasa katika kupata leseni, makosa ya barabarani ambayo imetanjwa kuwahusisha askari wa usalama barabarani mpaka maafisa wa ngazi za juu ndani ya kikosi hicho

Nimekuwa dereva zaidi ya miaka 30 bila ajali. Kinacho nisikitisha ni kuona jinsi serikali inavyo ruhusu maaskari wa usalama barabarani kuchukua rushwa. Ningekuwa na mamlaka katika hili taifa, kitu cha kwanza ambacho ningefanya ni kufuta kwanza kikosi cha usalama barabarani na kukiunda upya. Nimeona mara nyingi mkuu wa usalama barabarani amekuwa mwanasiasa kuliko utendaji. Vyombo vingine vya usalama navyo vinafumbia macho matendo ya trafic. Ninasikitika nguvu ya Taifa inateketea na watawala wanajitahidi kutuma salam za rambirambi badala ya kuchukua maamuzi. Shaaaame.
 
[QU OTE=LESIRIAMU;10525902]Nimekuwa dereva zaidi ya miaka 30 bila ajali. Kinacho nisikitisha ni kuona jinsi serikali inavyo ruhusu maaskari wa usalama barabarani kuchukua rushwa. Ningekuwa na mamlaka katika hili taifa, kitu cha kwanza ambacho ningefanya ni kufuta kwanza kikosi cha usalama barabarani na kukiunda upya. Nimeona mara nyingi mkuu wa usalama barabarani amekuwa mwanasiasa kuliko utendaji. Vyombo vingine vya usalama navyo vinafumbia macho matendo ya trafic. Ninasikitika nguvu ya Taifa inateketea na watawala wanajitahidi kutuma salam za rambirambi badala ya kuchukua maamuzi. Shaaaame.[/QUOTE]

Utawala mbovu kuanzia juu mpaka chini hakuna afadhali mkuu, hao polisi wenyewe wanapeleka hesabu kwa wakuu wao! Sasa unategemea nidhamu kivipi?
 
Inashangaza kuwa mpaka sasa Serikali haijazungumza lolote . Ingekuwa ni tukio la katiba mpya ungesikia kelele kwani umegusa maslahi yao.
 
Tuko busy tunashugulikia mambo ya kanzu kulowana kwa wale watuhumiwa ugaidi wafuasi wa mudi..haya ya ajali yasubiri
 
Ukichukua takwimu za ajali kwa vigezo muhimu kwa dereva yeyote pamoja na taarifa binafsi za madereva kwa kipindi cha miaka 10 tu utajua tatizo liko wapi,wanasiasa wanapiga porojo tu sijui kwa sababu wanamiliki hivi vyombo vya usafiri!
 
[QU OTE=LESIRIAMU;10525902]Nimekuwa dereva zaidi ya miaka 30 bila ajali. Kinacho nisikitisha ni kuona jinsi serikali inavyo ruhusu maaskari wa usalama barabarani kuchukua rushwa. Ningekuwa na mamlaka katika hili taifa, kitu cha kwanza ambacho ningefanya ni kufuta kwanza kikosi cha usalama barabarani na kukiunda upya. Nimeona mara nyingi mkuu wa usalama barabarani amekuwa mwanasiasa kuliko utendaji. Vyombo vingine vya usalama navyo vinafumbia macho matendo ya trafic. Ninasikitika nguvu ya Taifa inateketea na watawala wanajitahidi kutuma salam za rambirambi badala ya kuchukua maamuzi. Shaaaame.

Utawala mbovu kuanzia juu mpaka chini hakuna afadhali mkuu, hao polisi wenyewe wanapeleka hesabu kwa wakuu wao! Sasa unategemea nidhamu kivipi?[/QUOTE]
 
Ni vizuri Serikali ikaangalia Upya hivi Vyombo vya Abiria hususani Mabasi yote ya Abiria yawekewe Vidhibiti Mwendo na Mikanda ya Usalama na Tochi Ziongezwe Barabarani Watakaokiuka Hatua Kali zichukuliwe dhidi yao.
 
Tuwe na madereva makini tu ila ata ufunge izo speed governor ado kazi bure pia elimu itolewe na imani za kishirikina zikatazwe

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hivi majuzi nikiwa nchini Kenya nimeshughudia magari yote ya abiria yakiwa yamefungwa speed gavana. Speed ya mwisho gari kutembea ni 80. Sasa Tanzania inaonyesha mwisho wa speed ni zote ambazo gari inazo. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali yetu isivyojali maisha ya Watu wake.

Leo hii Magari yamegongana huko Musoma na watu 36 wamepoteza maisha na wengine 79 kujeruhiwa. Cha ajabu Serikali haitachukua hatua yoyote kuhakikisha ajali zinapungua. Tunaomba Serikali iangalie tena huu usafirishaji wa abiria kwani watanzania wanaangamia na wataendelea kuangamia kama hatua sahili hazitachukuliwa. Mimi naishauri Serikali ifunge spidi Gavana kwa mabasi yote. Na kusuka upya Jeshi la polisi (Trafic) kwani wengi wao wako Barabarani kwa ajili ya kula rushwa. Serikali ikifanya hivyo tunaweza kupunguza ajli za Barabarani.

Mungu Atusaidie sana.

...mkuu' siku za nyumba hii kitu (speed gavana) ilikuwepo na ikalalamikiwa sana na wamiliki wa mabasi....,

" Wamiliki wa mabasi
wagoma kufunga Speed
gavana

WAMILIKI wa Mabasi yaendayo
mikoani (TABOA) wamesema
hawatafunga vithibiti mwendo
kwenye mabasi yao kama
walivyotakiwa kufanya na serikali
kwani kifaa hicho kimeshindwa
kufanya kazi iliyokusudiwa ya
kupunguza ajali.
Pia wameitaka serikali kuwafutia
leseni za udereva, na kuwafunga
kifungo cha miaka mitano pamoja na
kulipa faini madereva wote watakao
bainika kusababisha ajali, pamoja
na kutokuwalaumu wamiliki hao
kwani wamekuwa hawahusiki na
ajali hizo pindi zinapotokea.
Akitoa tamko lao la pamoja jana
jijini Dar es salaam, kabla ya
kumaliza mkutano wa wamiliki hao,
Mwenyekiti wa TABOA, Mohamed
Abdula, alisema hadi sasa hakuna
basi lenye vidhibiti mwendo kwani
wamebaini kuwa chombo hicho
kinauzwa fedha nyingi na hakina
kazi, licha ya kuwa kinaharibika
haraka na kutokuzuia ajali.
“Tumekubaliana kwa pamoja kuwa
kifaa hiki hakifai na hakina kazi,
hatutakifunga kwenye magari yetu
tena, tumekuwa tukimnufaisha mtu
mmoja kibiashara tu, lakini hiki si
sababu ya kuzuia ajali. unafunga
ukifika hapo Kimara
kinaharibika,”alisema
Alisema kifaa hicho kinafungwa
kwenye gari ili lisiende mwendo wa
zaidi ya kilomita 80 kwa saa lakini
baadhi ya sehemu magari yamekuwa
yakipata ajali yakiwa kwenye
mwendo wa chini ya Kilomita 60.
“Hiki ni chombo ambacho
wamekianzisha na sasa
kimeshindwa kazi, hakitufai na
hakikidhi haja, tumekifunga miaka
15 iliyopita lakini bado
tunazungumzia ajali zilezile huku ni
kupoteza fedha na muda tutafute
dawa ya ajali,” alisema Abdula.
Pia wamiliki hao wa mabasi ambao
kwa pamoja walikataa wawakilishi
wa baadhi ya wamiliki kushiriki
katika kikao hicho, walisema serikali
ifuatilie kwa umakini dereva
anayedhibitika kusababisha ajaili
ashitakiwe kutumikia kifu ngo
kisichopungua miaka mitano, na
alipe faini kubwa ili kuwakomesha.
Alisema Dereva atakayesababisha
ajali afutiwe leseni na kutoajiriwa
tena katika kampuni yoyote nchini
ili iwe fundisho na asiende
kusababisha ajali mahali pengine.
Kwa upande mwingine wamiliki hao
walikubalina kuwa serikali kupitia
Mamlaka ya usimamizi wa barabara
(Tanroads) iondoe matuta yaliyopo
barabarani na mabasi yote ya abiria
yaondolewe kwenye utaratibu wa
kupitia kwenye mizani kupima kwani
leseni inatolewa kwa kuzingatia
idadi ya abiria na siyo uzito.
“Tunaiomba serikali iyatoe mabasi
katika orodha ya magari yanayopita
kwenye mizani, mizani
zinasababisha foleni, magari
yanarundikana hapo baadaye
yakiachiwa yanaanza kukimbizana,
Mizani zinasababisha rushwa sizizo
na lazima, tunataka
tuziondoe,”alisema
Pia walitaka ratiba ya kuanza safari
ya mabasi katika vituo vya mabasi
nchini ibadilike iwe kwa magari yote
kuondoka kwa muda unaotofautiana
tofauti na sasa ambapo hutofautiana
kidogo na kusababisha kusindana
njiani.
“ Tunaiomba ratiba ya safari
ibadilike mabasi yaruhusiwe
kutembea usiku ili kupungusa
kufukuzana, leo hii ratiba
inamalizika saa 5 asubuhi wakati
wakiruhusu hadi jioni, tutaiona
madereva wakiendesha polepole
wakijua kuwa hawatazuiwa njiani”
alisema
Kuhusu kutolewa leseni kiholela
bila kuzingatia vigezo, TABOA
walisema serikali idhibiti utoaji wa
leseni na kama kuna askari wa
usalama barabarani wanaohusika
kuzitoa wadhibitiwe.
Kuhusu askari wanaosimamisha
mabasi ghafla barabarani walisema
hilo ni la kudhibiti kwani askari
wamekuwa na tabia ya kujitokeza
kutoka vichakani ghafla na
kusimamisha mabasi na
kusababisha magari kuanguka kwa
kushika breki gafla.
 
Nimekuwa dereva zaidi ya miaka 30 bila ajali. Kinacho nisikitisha ni kuona jinsi serikali inavyo ruhusu maaskari wa usalama barabarani kuchukua rushwa. Ningekuwa na mamlaka katika hili taifa, kitu cha kwanza ambacho ningefanya ni kufuta kwanza kikosi cha usalama barabarani na kukiunda upya. Nimeona mara nyingi mkuu wa usalama barabarani amekuwa mwanasiasa kuliko utendaji. Vyombo vingine vya usalama navyo vinafumbia macho matendo ya trafic. Ninasikitika nguvu ya Taifa inateketea na watawala wanajitahidi kutuma salam za rambirambi badala ya kuchukua maamuzi. Shaaaame.

Tuko busy tunashugulikia mambo ya kanzu kulowana kwa wale watuhumiwa ugaidi wafuasi wa mudi..haya ya ajali yasubiri
Acha upuuzi,watu wamekufa,kuna msiba mkubwa,wewe waleta utani.
 
Hivi majuzi nikiwa nchini Kenya nimeshughudia magari yote ya abiria yakiwa yamefungwa speed gavana. Speed ya mwisho gari kutembea ni 80. Sasa Tanzania inaonyesha mwisho wa speed ni zote ambazo gari inazo. Hii inaonyesha ni kwa jinsi gani Serikali yetu isivyojali maisha ya Watu wake.

Leo hii Magari yamegongana huko Musoma na watu 36 wamepoteza maisha na wengine 79 kujeruhiwa. Cha ajabu Serikali haitachukua hatua yoyote kuhakikisha ajali zinapungua. Tunaomba Serikali iangalie tena huu usafirishaji wa abiria kwani watanzania wanaangamia na wataendelea kuangamia kama hatua sahili hazitachukuliwa. Mimi naishauri Serikali ifunge spidi Gavana kwa mabasi yote. Na kusuka upya Jeshi la polisi (Trafic) kwani wengi wao wako Barabarani kwa ajili ya kula rushwa. Serikali ikifanya hivyo tunaweza kupunguza ajli za Barabarani.

Mungu Atusaidie sana.

Kwanza naomba ujue Mungu hasaidii watu wazembe na wavivu. Akishatupa akili na maarifa ya kupambana na mambo ya kimaisha. Back to the topic. Pamoja na uzembe wa barabarani lakini mimi nadhani body za mabasi ya abiria hazina ubora. Utengenezaji wake unaonekana ni wa kubana matumizi (kama kwenye ghorofa za matope) hivyo uimara wake si wa kiwango kinachokubalika!
 
Back
Top Bottom