Serikali fungieni vyombo vya habari pamoja na watangazaji wanaoendesha vipindi vyenye vinasaba vya upotoshaji

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,229
3,525
Uhuru umezidi, vyombo vya habari vimekosa uadilifu, vyombo vya habari vimekosa uzingatizi wa sheria na kanuni za kiutangazaji, Vyombo vya habari vimekosa uweledi wa udurusu wa maudhui kabla ya kurusha kipindi hewani,

Zipo baadhi vya online tv zinahamasisha vipindi vya mapenzi ya kinyume na maumbile kwa kuwahoji machangudoa, Zipo online Tv zinapromote uongo kwa masrahi binafsi ya kutangaza utapeli,

Lakini zaidi na zaidi lengo langu naiomba Serikali Ichunguze kipindi alichokifanya Mtangazaji maarufu MILLAD AYO na huyu anaejiita Mfalme zumaridi, kwani kuna maneno ya upotoshaji na uongo, ambao licha mtangazaji huu kutambua kuwa ni vitu haviwezekaniki kibinadamu na kikawaida lakini bado mtangazaji huyu ameamua kufanya maksudi kwa kurusha hewani kipindi hiki kupitia TV yake ya AYO TV,

Baadhi ya maneno yenye uongo wa kuaminika ni haya hapa :"nilitokewa na mungu usiku alikuja na jua' kikawaida na kibinadam jua haliwezi kusogea jirani na uso wa dunia lisilete maafa, ila mama huyu anadanganya umma kuwa jua lulimwingia mwilini,

Ningeomba kijana huyu afungiwe ili liwe fundisho kwa wandishi wengine ambao wanafanya vipindi vyenye content za upotoshaji kwa lengo la kujiingizia kipato kwa taarifa zenye lengo la kuwahadaa wasikilizaji na kupotosha jamii, pia kuleta taharuki miongoni mwa wanajamii.

---
Pia soma
- Clouds TV imeanza kuwa kituo cha kutetea wauza madawa ya kulevya
 
Back
Top Bottom