Spika Tulia hana imani na vyombo vya habari vya Umma na CCM

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,804
8,797
Spika wa Bunge Dkt. Tulia hivi karibuni katoa kauli ya kuvitaka vyombo vya habari kufikisha kwa usahihi habari za bunge kwa Wananchi.

Kitendo cha kuvitaja Jamii Forum na gazeti la Mwananchi, inaonyesha wazi kuwa hana imani na vyombo vya habari vya serikali na chama chake.

TBC, Daily News na Habari Leo hivi ni vyombo vya habari vya Umma vinamilikiwa na serikali. Tulia ambaye ni Mbunge kupitia CCM, huko wanamiliki gazeti la Uhuru na Mzalendo sijui kama yapo haya makaratasi. Pia wa Radio Uhuru na TV station waliyodhulumu CHANNEL 10.

Sasa hivi vyombo vya habari haviaminiki na Spika.

Kauli ya Spika, Soma: Tulia Ackson: Gazeti la mwananchi, JamiiForums tunawategemea kuwapelekea taarifa sahihi, tusipeleke za upotoshaji
 
Back
Top Bottom