Serikali/CCM: Mtazikwepaje hasira zetu kwa uzembe huu!

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,409
31,393
Madarasa mawili wasomea chumba kimoja

Saturday, 05 March 2011

balaatz.jpg

Wanafunzi wa darasa la pili na tatu wa shule ya Msingi Magwalasi katika Kata ya Rujewa, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya wakiwa darasani wakiendelea na masomo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa shule hapo imewalazimu chumba kimoja kutumiwa na wanafunzi wa madarasa mawili kwa kila darasa kugeukia upande wake kama walivyokutwa na mpigapicha wetu jana. Picha na Brandy Nelson

Brandy Nelson, Mbarali

UHABA wa vyumba vya madarasa umewalazimu wanafunzi wa madarasa tofauti katika Shule ya Msingi Magwalasi iliyoko Kata ya Rujewa wilayani Mbarali, Mkoa wa Mbeya kusoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo.

Waandishi wa habari walifika hapo jana na kukuta shule hiyo yenye wanafunzi 269 na walimu saba wa kuanzia chekechekea, darasa la kwanza hadi la saba ikiwa na vyumba vinne pekee vya madarasa.

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Jonathan Chengula aliwaambia waandishi wa habari kuwa katika shule hiyo iliyoanza na kusajiliwa mwaka 2003, wanafunzi wa darasa la kwanza wanasoma chumba kimoja kwa wakati mmoja na wale wa chekechea, darasa la pili wanasoma pamoja na wenzao wa darasa la tatu, la sita na la tano, huku wale wa darasa la saba wakitumia chumba kimoja na wa darasa la nne.

"Tatizo kubwa ambalo linatusumbua katika shule yetu ni upungufu wa madarasa. Tuna madarasa manne tu hivyo imetulazimu kuweka mbao za kufundishia mbili katika chumba kimoja ili madarasa mawili yaweze kutumia kwa wakati mmoja," alisema.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu huyo, ili kukabiliana na upungufu huo wa madarasa na kutokana na mazingira ya shule hiyo, ndiyo maana wameramua wanafunzi wa madarasa mawili tofauti wasome katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo kwa maana ya kuwa wengine wanageukia upande wa kulia na wengine kushoto.

"Kama mnavyowaona hawa waliogeukia huko ni darasa la saba na hawa wengine ni darasa la nne na katika darasa hili jingine wanasoma darasa la pili na tatu ndivyo tunavyo kwenda," alisema.Alisema kuwa mwalimu wa darasa la saba anapoingia kufundisha, wa darasa la nne anasubiri mwenzake amalize huku wanafunzi hao wa darasa la nne wakiwemo humo humo ndani wakisikiliza wale wa darasa la saba wanavyofundishwa.

Alisema wakati mwingine walimu huamua kuwatoa nje na kuwaweka chini ya mti kama umefika wakati wa kusoma kitabu cha Kiswahili ili wasome wakiwa nje na wengine waendelee na masomo.

Mwalimu aliyekuwa darasani akifundisha, Shufaa Ramadhani alisema mazingira hayo ya ufundishaji ni magumu kwani kuna athari kubwa kwa wanafunzi na upande wa mwalimu kwani kufundisha wote kwa pamoja pia ni vigumu.

Alisema kuwa utaratibu huo unawaathiri watoto kisaikolojia kwani kuna uwezekano wa kusahau yale ambayo wamefundishwa na mwalimu wao na badala yake kusikia ya upande wa pili ambayo ni masomo ya darasa jingine ambalo tayari walishayapitia au bado hawajapitia.

Mwalimu Shufaa alisema walimu wanaathirika kwa kupoteza vipindi vingine kwa mujibu wa uandaaji wa masomo na vipindi kwani inamlazimu asubiri mwenzake amalize kufundisha na ndipo aingie na kufundisha somo lake.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, George Kagomba hakupatikana kuzungumzia tatizo hilo na alipotafutwa kwa simu alijibu kuwa yuko kwenye kikao cha maandalizi ya Mbio za Mwenge.

Mkurugenzi huyo aliwataka waandishi kwenda kwa Ofisa Elimu wa Wilaya ya Mbarali. Hata hivyo, aliyekuwa akikaimu ofisi hiyo hakuwepo. Ofisa elimu wa Wilaya alikuwa amesafiri kikazi

My take:
Je hivi ndivyo tunavyowaandaa watoto wetu kwa ushindani katika dunia ya leo? Je matatizo ya madarasa yamesababishwa na kupanda bei za mafuta wiki mbili zilizopita?

Chadema wanaposema hali hii haifai, wanakuwa wamechochea vurugu gani? Kama serikali ina vyombo vya kuishughulikia Chadema, kwanini nguvu hizo zisielekezwe kwenye mambo muhimu kama haya?

Kwanini serikali ipate kiwewe na mikuatano ya ''porojo'' ya Chadema na isipate kiwewe na hatari hii inayo onekana bila microscope. Hivi wananchi wenye watoto katika shule hii kwanini wasiwe na hasira na serikali yao, eti hasira inatokana na maandamano ya Chadema!!
 
Sasa kwa akili timamu eti nchi ina miaka 50 ya uhuru shule zimechoka namna hii kweli?

NYIE CCM nawauliza kweli namna hii? eti wewe JK unayelia lia na kabla dhahma haijakukuteni tuambie mmefanya nini miaka yote hii? Nchi uchumi mbovu, hebu niambieni CCM, mikoa ya kusini gridi ya taifa haijafika miaka 50 ya uhuru kweli? Mikoa ya magharibi gridi ya taifa haijafika kweli nchi hii itaendelea? sasa umeme ndo huo mmewapa mafisadi na Dowans ndo kila kitu kweli uchumi wa nchi hii utaimarika?

Wewe Pinda unajidai muungwana wakati unatetea mafisadi sitaki kukusikia ni chui ktk ngozi ya kondoo. kwa nini tupate shida kwa ajili ya kikundi cha watu wachache hawa?

Please CCM ondokeni kwa amani mmeshindwa kuongoza nchi hii, mnakashfa nyingi sana kuanzia za Loliondo, mpaka leo Dowans, hakuna mwana CCm anaytetea maslahi ya wananchi leo wanatetea mafisadi tuuu
 
Halafu ukiuliza gharama za kujenga madarasa sio kubwa hivyo basi tu watu hawataki, ila kwenye harambee za kuchangia harusi na kipaimara aah wanatoooooooa. Serikali inanunua mashangingi tu ss tunakonda.
 
Hivi zile milioni 90 za magari ya wabunge zinaweza kujenga madarasa mangapi? Kwa ufahamu wangu napata madarasa yasiyopungua 25
 
Ni lazima tujifunze kujitegemeza mawazoni mwetu......mambo mengi yanaweza kurahisishwa nasi wenyewe,lakini kwa sababu tunadhania mtu fulani ndo anawajibu wa kutuwajibikia,basi tunabakia hasira....hahah
 
Lakini si kulikuwa na uhamasishajiwa ujenzi wa madarasa, hapa haukupita?

Nakubali kuwa wananchi wana jukumu hilo pia lakini serikali izijivue wajibu wa kusimamia mambo kama haya. Kwa mamiioni ya pesa za walipa kodi zinazoptea kwa ulaji sidhani hili lingekuwa tatizo kubwa kiasi hiki.

Hoja kubwa hapa ni kuwa serikali isifuatilie mambo ya kawaida kama maandamano bali ijikite kwenye mambo muhimu ya kitaifa. Nashangaa Rais, waziri mkuu, na mawaziri wote wamekomalia Chadema, mbona hatuwaoni wakikomalia issue kama hizi.

Na mwisho kumbuka kuwa hawa ni watu wanalipa kodi kutoka katika dola moja wanayoishi nayo kwa siku, ni ajabu kuwa kodi hizo zinatumika haraka haraka kulipa Dowans bila kuwasaidia kule waliko, huoni paradox.
 
inasikitisha eti tanzania masikini sikubali mimi,rasilimali tulizonazo ulaya hakuna lakini bado masikini ? tuna mgodi na gesi,kuna pesa za watoa jasho wanazokusanya za kodi,maji tunalipia,umeme tunalipa,maisha gani haya ?

Ukiangalia barabara tunajengewa kwa misaada,elimu misaada,afya misaada,sasa nauliza pesa za uuma zinaenda wapi ? Shule miaka 47 nusu karne sasa tunasoma katika mabanda ya mbuzi ?

Mimi sikubaliani kabisaaaaaaaaaaaa kama tanzania masikini,nina hundred percent kuwa tanzania ina uwezo wa kuwalisha wananchi wake na kuwavisha na kuwapa makazi kwa uchumi tuliona na rasilimali tulizonazo,tatizo ni kwamba hili neno masikini tumeliweka katika vichwa vyetu na hatulitaki kulivua kila siku tunategemea misaada,umasikini tunaukaribisha sisi wenyewe hapa tanzania na viongozi wetu hawa wakada wa ccm ndio wanao tuletea.

Kuna mambo mengi ambayo tanznaia linawakabili moja ya hayo elimu duni,tena tunaikaribisha wenyewe,wajenzi wa mashule wanapewa ma biloni wajenge shule lakini wanajenga mabanda ya mbuzi wakati wanauwezo wakujenga shule zenye viwango vya kimataifa ikiwamo na facilities,mi naamini kama tutapata viongozi wa kweli basi ndani ya mwaka mmoja tunafanya mapinduzi ya elimu.

Lakini tuing'oe ccm ndio tutafanikisha kwani JK ameshasema kuwa tatizo la umeme,maisha kuwa magumu,elimu,na mengine hayatamaliza maisha ,,,na yeye atayaacha na wengine wanaokuja watayaacha vile vile,,,,,sasa tutarajie nini watanzania ?
 
Inaelekea kama nchi watawala wetu hawana priority wanajiendea tu.... hivi kweli serikali inashindwa kujenga vyumba vya madarasa simple kama hicho kwenye picha.....watasema wanasubiri wafadhili..... lakini wako tayari kulipa madeni hewa na kulipana posho hewa!! Shame on them!
 
Hapo kuna Afisa Elimu wa Wilaya ukimuuliza idadi ya shule katika wilaya yake na hiyo ni moja wapo!! Falsafa ya serikali ya CCM ni idadi (quantity) na sio ubora(Quality).

Hivi tunategemea ubora wa elimu upatikane katika mazingira hayo ya madarasa mawili kutumia chumba kimoja na chenye vumbi? Wakati watoto wetu wanasoma katika mazingira hayo, watoto wa mafisadi (Jakaya Kikwete and friends) wanasoma kwenye shule bora (International schools) na wengine nje ya nchi unategemea nini? Mtoto akishamaliza hapo akabahatika kuchaguliwa anakutana na shule za kata (yebo yebo) ambazo ni matatizo matupu! Unategemea nini?

CCM inabidi watambue kuwa mambo haya pamoja na mengine mengi ndio yanayo waondolea uhalali wa kuongoza nchi hii na mchawi wao ni wao wenyewe na sio CHADEMA! CHADEMA wanachofanya ni kuwaelimisha na kuwakumbusha watanzania kuwa adui yao mkubwa ni CCM pamoja na serikali yake inayoongozwa kwa remote control na Rostam Aziz (Raia wa Iran).
 
Jamani watanzania tuamke tuikomboe nchi yetu, what kind of a future are we building for these kids: can you tell me how many of those kids that you think can make up to the university?
Tuseme inatosha sasa, Tuchukue hatua.
 
Jana Rwanda wametangaza kufundishia kiingereza kama lugha kuu ya pili baada ya french sisi tunapanga kuacha kiingereza ibaki swahili tuu! Hiyo ni akili? Wananchi wakijitolea elimu CCM inasusia fisadi mkono kajenga shule huko musoma vjjn akaipa govt,govt wameitelekeza sasa anafikiria kuimiliki mwenyewe, Godbless Lema (MP wa Arusha mjini) juzi viongozi wa mkoa wamemsusia hafla ya kukubidhi msaada wakusomesha watoto 400 bure na afya! Hapo utawalaumu wananchi?
 
halafu wanapoambiwa ukweli na CDM wanakuja juu na kuanza kutoa maneno ya chuki yasiyo kuwa na maana.
Nasema kuwa hao watoto wanaosomea shule na mazingira kama hayo hawawezi kuipenda serikali yao hata siku moja.
Hilo nalisema hata kama ningekuwa ni mimi ningeichukia serikali milele kwa sababu ni kwa makusudi kabisa.
Huwezi kusema hakuna pesa za kujenga shule tena za awali kabisa ( which is very basic to all human kind) huku wenyewe wakiendesha magari ya mamilioni,
Hao ndio watakao kuwa mwiba mkubwa kwa serikali zaidi hata ya sisi.
wait and see.
 
thanks for your insight.
Hapo kuna Afisa Elimu wa Wilaya ukimuuliza idadi ya shule katika wilaya yake na hiyo ni moja wapo!! Falsafa ya serikali ya CCM ni idadi (quantity) na sio ubora(Quality).

Hivi tunategemea ubora wa elimu upatikane katika mazingira hayo ya madarasa mawili kutumia chumba kimoja na chenye vumbi? Wakati watoto wetu wanasoma katika mazingira hayo, watoto wa mafisadi (Jakaya Kikwete and friends) wanasoma kwenye shule bora (International schools) na wengine nje ya nchi unategemea nini? Mtoto akishamaliza hapo akabahatika kuchaguliwa anakutana na shule za kata (yebo yebo) ambazo ni matatizo matupu! Unategemea nini?

CCM inabidi watambue kuwa mambo haya pamoja na mengine mengi ndio yanayo waondolea uhalali wa kuongoza nchi hii na mchawi wao ni wao wenyewe na sio CHADEMA! CHADEMA wanachofanya ni kuwaelimisha na kuwakumbusha watanzania kuwa adui yao mkubwa ni CCM pamoja na serikali yake inayoongozwa kwa remote control na Rostam Aziz (Raia wa Iran).
 
Inaelekea kama nchi watawala wetu hawana priority wanajiendea tu.... hivi kweli serikali inashindwa kujenga vyumba vya madarasa simple kama hicho kwenye picha.....watasema wanasubiri wafadhili..... lakini wako tayari kulipa madeni hewa na kulipana posho hewa!! Shame on them!
their days are numbered,let them threaten us,
let them threaten CDM

but they should remember that they have already lost the creadibility for Leading this Nation.

beacuse they are no longer leaders but followers.

Eti mkurugenzi wa halmashauri anashindwa kuzungumzia suala hili nyeti kisa yuko kwenye kikao cha maandalizi ya mbio za mwenge...UPUUZI!ye anajali sana mbio za mwenge kuliko maendeleo ya elimu!Mwenge unamsaidia nini mwananchi,mlalahoi wa nchi hii zaidi ya kulazimishwa kuuchangia?AIBU HII....
 
that is not their priority at all,

Back
Top Bottom