Sera za muungano za chama cha CHADEMA hizi hapa

Nitaandika katika sentensi moja, kama utashindwa kuona hiyo MANTIKI basi huwezi ku pass hata course ya LLB 101.

Mantiki yake iko kwenye HAKI ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi.

The Oparating word here is HAKI. I rest my case.

Inawezekana kabisa kwamba you have a very high level of intelligence than I, ndio maana sikuelewi, ila nitaendelea kuwa wa kiwango hicho kwani vijisababu unavyotoa kwangu still they are very superficial na za kutumia tu loopholes za sheria, haki, ili kufanikisha malengo fulani fulani ya kisiasa; Vinginevyo kama wewe ni msomi kama unavyojidai, bila ya kupoteza muda ungeshatumia utaalam wako wa sheria to come up with a reasonable argument why the candidacy age should be harmonized with the voting age in our context; Lakini naamini wapo wengine humu ambao wataniokoa kutoka katika hali hii duni ya ubongo ili na mimi pia niwe mwelewa kama wewe; Vinginevyo tuombee uzima kushuhudia content ya katiba mpya in that regard itasema nini; Kila la kheri;
 
Mbona Nchi nyingi sana zinatumia Umri wa 18 lakini hakuna hata mmoja ilio wahi kuongozwa na mtu wa Umri huo? Ulaya nchi nyingi wanatumia umri huo, wa miaka 18
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Vyama vimeonesha bado havijatambua Mtanzania wa sasa anataka nini na anategemea vyama vifanye nini.

Ama kweli, kama vyama mbadala ndiyo vinakuwa na mapendekezo kama haya, Tanzania bado tuko mbali sana katika demokrasia ya kweli na maendeleo.

Is this April foul's day or I'm just in dream.

Bahati mbaya Tume ya Katiba imetunyima haki ya kusikiliza maoni ya vyama vyote. CCM wanasemaje kuhusu hili.
 
Ndio maana nikauliza kigezo kwetu ni nini, je ni miongoni mwa vile nilivyotaja? au ni kwa sababu wengine wanafanya hayo kwa mfano ufaransa? Katika muktadha wetu, kigezo cha miaka 18 ni kipi hasa.

Unayo haki ya kuhoji lakini tujiulize kuweka umri Kama kigezo inasaidia nini? Je ukichagua kwamba umri wa chini wa mtu kuwa Rais ni miaka 35 ni kigezo kipi ulichotumia kuona kuwa umri huo ndio sahihi? Ninaunga mkono ukweli kwamba ikiwa tumekubaliana umri wa mtu 'mzima' anayeweza kuchagua kiongozi basi hiki ndio kiwe kigezo pia cha kuchaguliwa. Kinyume chake ni kuweka kigezo ambacho hakina hakina mshiko na kinaminya haki ya mtu binafsi.
 
Hoja ya CUF kuwa kusiwe na chaguzi ndogo mi naipinga. Naipinga kama itakuwa kama inavyosemwa kwamba mbunge akifa bac yule aliyeshika nafasi ya pili apewe Ubunge aendeleze mchakato. Hii naona itatuletea adha ya kuuwana. Watu watalogana au hata kusababishoana ajali kwavile tu mtu anajua yule akifa kiti kile anakalia yeye. Hiyo ni possible kwakuwa gharama za kumtoa mtu roho ni ndogo ukilinganisha na zile hela wanazolipwa wabunge.
 
CDM wamepoteza golden opportunity kwenye suala la MUUNGANO. This is a BOLD TRUTH. CDM huko ZNZ hawana wafuasi wengi hili lazima walitambue. Majority ya wafuasi wa CDM wako Tanganyika. Baada ya kuweka facts hizi wazi, kwanini CDM wamepoteza golden opportunity??

Baada ya chokochoko za mda mrefu za Wazanzibari kuhusu Muungano, Watanganyika wengi wanaona dawa/suluhisho la malalamiko hayo ya Wazanzibari wakati wanachangia ZERO SHILINGI kwenye Muungano, ni kuwa na nchi moja, serikali moja, rais mmoja. Huu ndiyo ungepaswa kuwa msimamo wa CDM.

Kama CDM wangekuja na msimamo huu wange score points huku Tanganyika ambako ndiko base yao ilipo. Lakini pia msimamo huu ungewa udhi wazanzibari WOTE. Lakini CDM they have nothing to loose in Zanzibar. Lakini huo msimamo wa serikali tatu, halafu URAIS wa Muungano uwe wa kupokezana vijiti kati ya Tanganyika na Zanzibar, they have shoot themselves on their feet.

Mkuu mimi siwezi nikakupinga mawazo yako lakini kwa muda huu tulionao na kama unafuatilia siasa za zanzibar na tanganyika nahisi kwa hayo maneno uliyoyasema hutanipinga iwapo nikwambia umezungumza mumbo jumbo or nonesense.labda nikukumbushe tu labda umesahau.jee umesikia mtanganyika kuelezea kero za muungano?kama wapo ni wachache lakini unapomwambia mtanganyika akuwekee angalau kero tatu,atakwambia zanzibar tunawapa umeme,tunawapelekea chakula,tunawaajiri etc.hizo ndo kero kuu za watanganyika.kama mtu anafikira na mawazo yajuu kabisa,atajiuliza hawa wazanzibar tunawapa huduma hizi kwanini,mwisho utagundua kupata huduma na nafasi ni haki yao kwasababu hakuna nchi tanganyika bali iliopo ni jmt na zanzibar imo ndani ya jmt.lakini ndugu zetu wazanzibar unapo muuliza kero za muungano kwa haraka haraka atakupa kumi na tano na nizamsingi kabisa.kwa hiyo mdogo wangu kuifanya nchi moja kwa wazanzibaq ni sawa na kuput all eggs into one basket so haiwezekani.na ukikomaa kutaka nchi ndo wazanzibar watakuja juu mara mbili zaidi na kupinga serikali moja.kwa mfumo wa serikali tatu nawapongeza chadema na cuf,hapo kila nchi itajitegemea.je wewe hupendi kila nchi ijitegemee?kama hupendi unataka serikali moja malumbano mengine yataibuka.wapo ambao watasema zanzibar wanatengwa kimaendelea kwasababu ni mkoa wa kusini,ama waislamu ni wengi,ama waarabu,ama uamsho,wazanzibar kwao na watanganyika kwao.
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Vyama vimeonesha bado havijatambua Mtanzania wa sasa anataka nini na anategemea vyama vifanye nini.

Ama kweli, kama vyama mbadala ndiyo vinakuwa na mapendekezo kama haya, Tanzania bado tuko mbali sana katika demokrasia ya kweli na maendeleo.

Is this April foul's day or I'm just in dream.

Duuu yani yote then HAMNA HATA MOJA???
 
Well said Chadema, ila hoja juu ya umri wa miaka 18 kama sifa na kigezo (kikatiba) ya mtanzania - hasa haki ya kuchaguliwa nafasi ya Urais kidogo haijaeleweka vizuri, je ni kwa hoja kwamba if you are old enough to vote then you are old enough to run for any political office? Au hoja hii ipo based on median age in Tanzania? Au kwamba majority of Tanzanians are under the age of 30? Au kwa sababu nyingine zozote...?

Mtanzania husika anatarajiwa atakuwa amefikia kiwango gani cha elimu na anatakiwa awe na uzoefu kiasi gani katika masuala ya public leadership? In other words, je kuna requirements pia za minimum qualifications (experience ya uongozi) na pia minimum level of education? Is it degree ya kwanza? It is miaka kadhaa ya uzoefu fulani? At what age mtanzania husika anatarajiwa kupata hiyo degree au kukusanya the relevant experience? Au elimu na experience sio vigezo vya msingi?

Chadema needs to approach suala hili la umri na kugombea urais holistically, not in an atomistic manner; Otherwise the age of 35 is more ideal;
kaka kama umeamua kuandika kwa kiswahili basi iwe kiswahili na kama ni kiingereza basi iwe kiingereza,sasa huu mchanganyo wa lugha na maneno ya kiingereza na kiswahili unaondoa utamu wa hoja,na kuifanya ionekane iko bias kwa wasomi tu na wasiojua kiingereza ndio hoi kabisa.Ni hayo tu,ila wazo lako zuri!
 
Umri wa miaka 18 nakuendelea ni pendekezo murua kwa maana ya kuondoa UBAGUZI,pili kuzingatia HAKI YA KIKATIBA.Kama wa miaka 18 ANAYO AKILI YA KUTOSHA KUCHAGUA ambayo hamna mpinzani viweje akose haki ya kuchaguliwa?
Serikali TATU/MOJA AMA MBILI ingefaa referendum ifanyike kwa hatua TATU:
1.Iwapo wazANZIBARI/BARA wanaukubali Muungano
2.Iwapo Watanganyika wanaukubali Muungano
3.Aina ya Muungano inayokubalika na kundin zima IWAPO WALIO WENGI wataukubali Muungano
VINGINEVYO KUNA HISIA SAHIHI kuwa JK na WARIOBA&team tayari wana KATIBA YAO MFUKONI wanachofanya wanahalalisha ULAJI wa Fedha NA NOTES kuwa walipokea maoni
 
Kwani mtu akigombea lazma achuguliwe?me nadhani hakuna makosa katika hili ni uvivu tu wa baadhi ya watu kuelewa au kutotaka kuelewa au hulka ya kupinga kila kitu kwa sabu tu anayependekeza si wa chama chake.
Well done chadema,tungeona na mapendekezo ya ccm ingekuwa bora zaidi tulinganishe.
 
Hoja ya umri wa miaka 18 nafikiri kuwa gazeti la habari leo , liliamua kufanya Spinning kwa malengo ya kuwafurahisha watawala, ila hoja ya Cdm ni kuwa kama una haki ya kuchagua kwanini usichaguliwe? Mbona ubunge ni miaka 21 , ni kigezo gani kiliangaliwa? Kwanini hata kuwa mwenyekiti wa kijiji lazima uwe na miaka 21? Ni kigezo gani kilitumika? Mbona umri huu unakuwa centred kwa urais tuuu? Je? Watanzania wakiamua kumchagua rais wa miaka 18 nani mwenye haki ya kusema kuwa huo sio uamuzi sahihi?

Aidha, ijulikane kuwa katiba inaweka misingi tuu na taratibu za kusimamia hiyo misingi zinatengenezwa na sheria zitakazotungwa........
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Vyama vimeonesha bado havijatambua Mtanzania wa sasa anataka nini na anategemea vyama vifanye nini.

Ama kweli, kama vyama mbadala ndiyo vinakuwa na mapendekezo kama haya, Tanzania bado tuko mbali sana katika demokrasia ya kweli na maendeleo.

Is this April foul's day or I'm just in dream.
mawazo ya vyama vyote viwili yanakubalika hasa kuhusu muungano kwamba kuwe na serikali Tatu, ngoja tuone maoni ya wanamagamba
 
Mapendekezo ya CHADEMA yanaacha maswali mengi zaidi ya majibu huku mapendekezo ya CUF yakiwa kama yameandikwa na kikundi cha UAMSHO.

Hapo yameandikwa na kikundi cha UAMSHO. Hebu fafanua kidogo. Itasaidia sana wanaJF kupata elimu zaidi
 
Proscovia Alengot Oromait has become Africa's youngest Member of Paliament (MP) at the age of 19, after she won the Usuk county election with 11,059 votes. The outspoken youngster replaces her father who died earlier this year.
Z

Alengot is a member of National Resistance Movement, headed by President Yoweri Museveni. Other people who stood for the post included, Charles Ojok Oleny with 5,329 votes, Charles Okure from FDC with 2,725 votes and Cecilia Anyakoit of UPC with 554 votes

Many people have come out to congratulate her, whilst some are saying she will not survive her term in parliament because of her age and limited experience. Some people believe this is the beginning of change in Africa and its time to get rid of the overly old leaders and allow young people to take the continent forward.
Hon. Alengot's area faces challenges of clean water, electricity and poor roads among others. For now the people of Usuk have their hopes pinned on the 19 year-old MP. Hopefully, she will be in position to represent her area and develop it.

alengot-1-375x252.jpg
0.jpg


 
Ndio maana nikauliza kigezo kwetu ni nini, je ni miongoni mwa vile nilivyotaja? au ni kwa sababu wengine wanafanya hayo kwa mfano ufaransa? Katika muktadha wetu, kigezo cha miaka 18 ni kipi hasa.

Kigezo ni uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa mtu kuupata kwa wakati mmoja, sio kumpata mtu uhuru wa kuchagua halafu wa kuchaguliwa unampa baadaye.
 
Kigezo ni uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa mtu kuupata kwa wakati mmoja, sio kumpata mtu uhuru wa kuchagua halafu wa kuchaguliwa unampa baadaye.

Mbona sioni kama kuna shida ya msingi katika hili? Kaka Mchambuzi labda hata kabla CHADEMA wenyewe hawajapatikana kufafanua tungeiweka hivi: Ili kuondoa fallacy katika mlinganyo ni SALAMA zaidi kuweka umri wa miaka 18.
Kimahesabu tukisema Z= Y/X huwa tunakua salama zaidi (hasa pale kanuni inapokua inahusu ujumla(general) zaidi kuliko kitu mahsusi(specific)) kutanabaisha kuwa "endapo tu X si sawa na sufuri". Inawezekana kabisa kuwa haitotokea thamani ya X kuwa sufuri lakini ili tu kuondoa fallacy, just in case ikatokea mtu akachomeka X=0 akapata infinity.
Nimejaribu kutumia kiswahili kadri nilivyoweza.
 
Last edited by a moderator:
Kigezo ni uhuru wa kuchagua au kuchaguliwa mtu kuupata kwa wakati mmoja, sio kumpata mtu uhuru wa kuchagua halafu wa kuchaguliwa unampa baadaye.

Kwamba haki ya kuchaguliwa ina mipaka pia au sio, kwamba una haki ya kuchaguliwa lakini hapo hapo wenzako wana haki zaidi kwa sababu kuna vigezo ambavyo wewe mwenye miaka 18 haujavitimiza kama vile minimum education and experience, au sio...
 
Kimsingi ninakubaliana na muhtasari wa mawasilisho ya maoni ya vyama hivi viwili vya kisiasa, lakini na tofautiana na hoja ya CUF kuwa usiwepo na uchaguzi wa marudio punde mgombea aliyeshinda uchaguzi anapokuwa amefariki.

Kwa kutenguliwa na mahakama ni sahihi aliyekuwa mshindi wa pili atangazwe ndiye mshindi hilo ni sawa kwani litakuwa linapunguza vitendo vya ukiukwaji wa sheria za uchaguzi na gharama zisikuwa za ulazima.

Lakini kwa suala la kifo kwa mshindi, uchaguzi urudiwe ilikupunguza vifo ambayo vitakuwa vinatengenezwa kisiasa ili aliyekuwa mshindi wa pili kuwa ndiye anayejaza nafasi.

Hasa hii itakuwa inakibeba chama kinachokuwa kinaongoza serikali kwa kuwa kinasimamia taasisi zote za usalama wa nchi na wananchi wake, tumeyaona ya akina Dkt. Ulimboka usalama unavyoshutumiwa kila kona kwa madai ya kuhusika kwake kwa manufaa ya wanasiasa walipo madarakani.
 
Kwamba haki ya kuchaguliwa ina mipaka pia au sio, kwamba una haki ya kuchaguliwa lakini hapo hapo wenzako wana haki zaidi kwa sababu kuna vigezo ambavyo wewe mwenye miaka 18 haujavitimiza kama vile minimum education and experience, au sio...

Vyema kabisa Mkuu wangu!
Wanachosahau wadau ni kuwa KATIBA ipo juu zaidi ya hicho wakiitacho HAKI. Na HAKI nayo haipatikani pasi kuwa utekelezaji WAJIBU. WAJIBU wetu uzaao Haki unatokana na Nyakati(mahusiano yetu) na Mazingira yetu. Tukishapima huko kote ndio tuje kwenye MAAFIKIANO-KATIBA. Labda kwa umri huu tunadhani huyu anaweza kupewa dhamana hii na hii kwani mazingira na nyakati zetu zinaruhusu, lakini dhamana hii na hii asipewe kwani nyakati na mazingira yetu hayaruhusu! KATIBA NDIYO IWEKAYO MIPAKA YA HAKI, TUKISHAKUBALIANA KWA VIGEZO VYENYE MANTIKI KWETU (yaani vinavyoendana na nyakati na mazingira yetu) kuwa hii ni haki lakini mpaka wake ni huu, IMETOSHA. Ndio maana leo kuna nchi zimeruhusu ushoga wengine hawaruhusu, na zote ni nchi za kidemokrasia zinazotambua Bill Of Rights ambako ushoga ni HAKI!
KATIBA IPO JUU YA HAKI. Nilisema hapa kuwa, vyama vyetu vinahangaikia HISIA za watu sio AKILI zao! Matokeo yake ndio hayo! Mara Serikali tatu au 2, Muungano wa mkataba, Serikali ya majimbo, Uraia wa nchi mbili, Raisi kupewa mamlaka makubwa, n.k ni upuuzi tupu! Laiti tungekuwa na ITIKADI YA TAIFA, iliyotokana na MAZINGIRA na NYAKATI ZETU, basi haya yote yasingekuwepo kwani tungehoji tu ITIKADI inasemaje!
Mungu wetu anaita sasa!
 
sera ya majimbo nimeipenda sana!! binafsi kwa chuki ambayo inaonekana kwa wazanzibari dhidi ya wabara busara kwanza nadhan ni tuvunje muungano alafu ndio tuojadiliane tuone kama kila upande unaitaji muungano na uwe wa aina gani kuliko kuanza kubadili bila kwanza kuuvunja huwezi jua pengine kwa kutumia njia ya "huwezi jua umuhimu wa kitu mapaka ukikipoteza" inaweza saidia kila upande uje na reasonable demands so kwa mimi mtanganyika nadhan kuhusu muungano sera iwe kwanza serikali moja au kuvunja muungano!!!!
 
Back
Top Bottom