Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Aisee wewe ni mtu hatari sana na natumaini haupo katika nafasi yoyote ya kuweza kutunga sheria ama sera unazozipigia debe hapa maana tutadumbukia katika shimo la chuki na ubaguzi usio na nafasi katika jamii yoyote ile iliyostaarabika!!
Nyani,
Hebu nikuulize na watu wote wa upande huo. Hivi ile sheria ya Marekani inayosema kuwa "Wahandisi wawili wakiomba kazi, wote wana pass karibu sawa, mmoja mweusi na mwingine mweupe, basi kazi apewe mweusi..." ni ya kibaguzi? Hata kwenye pass, weusi wanapendelewa. Tumesikia kuwa hata Tanzania kuna makabila kibao yamependelewa shuleni. Hii si kuleta ubaguzi. Hii kitu inatakiwa kufunguliwa na kulindwa kwa sheria kali. Wewe Nyani, Mwana kijiji, FM, Fundi Mchundo, Mkandara na wengine wengi haturuhusiwi kuwa kwenye listi ya watakaofaidika kwa kipesa, ila labda kimawazo.
Hivi usingelifanyika upendeleo KUTUSOMESHA sisi Lami, wengi humu tungelikuwamo? Mwaka Nyerere ametangaza shule zote bure, Mzee wangu aliyekuwa Mkulima, aliamua kuwachukua mabinti zake (dada zangu) warudi nyumbani waolewe. Hapo mmoja alikuwa aende form 5, mmoja form 1, mwingine darasa la tano. Kwa kuruhusiwa kusoma bure, dada yangu mkubwa alisoma hadi akawa Mhanidisi mwenye masters. Ilikuwa furaha kuona picha yake kwenye gazeti la Daily News akimuonyesha Nyerere (kama mfanyakazi wa Costech) matanki ya Biogas huko Dodoma.
Kumbe basi, kama serikali ikifanya sisi tunachokiita Upendeleo au wewe wakiita SERA ya kuwaendeleza Weusi katika biashara, kesho kutwa kuna vijana watamuonyesha Kikwete Biashara zao za kutisha, kama alivyofanya marehemu dada yangu. Halafu lazima mkumbuke ule msemo niliouona hapa kuwa "kwenye msafara wa Mamba na Kenge wamo". Hivyo katika kufaidisha weusi walio wengi, wahindi, Wazungu, Wachina, Waarabu, Wayahudi basi nao wao wata-tumbukiaMO.