SoC02 Sera ya Elimu imesimama imara, makandokando katika elimu yetu yanatoka wapi?

Stories of Change - 2022 Competition

Nyarubakula-Nabo

New Member
Aug 15, 2022
1
0
SERA YA ELIMU IMESIMAMA IMARA, MAKANDOKANDO KATIKA ELIMU YETU YANATOKA WAPI?

Kuna mambo kadhaa ambayo yanatakiwa kuangaliwa kwa macho matatu na wizara ya elimu, sayansi na teknolojia. Mwaka 1961 baada ya Waingereze kutukabidhi nchi yetu tulirithi karibia kila kitu ambacho walikuwa wakifanya wakoloni, kadri miaka ilivyosogea baadhi ya mambo tulianza kuyabadilisha ikiwemo falsafa ya elimu. Mwaka 1967 chini ya Baba wa Taifa, Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius K. Nyerere ilianzishwa sera ya "Elimu ya kujitegemea" ikiwa ni sehemu ya kufanya marekebisho ya elimu ili kusudi elimu iendane na mahitaji ya Watanzania na iwakomboe kutoka katika umasikini uliokuwa umekisiri ulisababishwa na wakoloni.

Pamoja na marekebisho ya sera yaliyofanyika bado elimu yetu, kuna maeneo yamekuwa sugu kufanyiwa marekebisho ambayo yamkini ndo yanayofanya elimu yetu tuioneka kama ambavyo inaokana ikilinganishwa na mifumo ya elimu ya nchi nyingine Duniani. Kwa mtazamo wangu kuna mambo kadhaa nayoyaona kama yangefanyiwa marekebisho yamkini elimu yetu ingekuwa bora zaidi kuliko hapa ilipo. Baadhi ya mambo hayo ni

Mosi, Lugha ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu iwe kiswahili.
Ngazi ya elimu ya msingi katika shule za umma kiswahili kinatumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia huku kiingereza kikifundishwa kama somo. Kuanzia ngazi ya sekondari hadi elimu ya juu lugha ya kufundishia ni kingereza. Lugha ya kiswahili wanafunzi wanaouwezo mkubwa wa kuimudu wakiwa darasani, hii inatokana na kiswahili kutumika katika mazingira yao ya kila siku wakiwa nyumbani na sehemu nyingne kama sokoni.

Wanafunzi wanapojiunga na elimu ya sekondari huwa tofauti, hukutana na lugha mpya ya kingereza ambayo hutumika kama lugha ya kufundishia na kijifunzia. Mwanafunzi anakatishwa mwendelezo aliokuwa ameanza nao darasa la kwanza hadi la saba ambapo anakuwa ameshazoea kiswahili.

Lugha ya kingereza ni changamoto kwa wanafunzi, hii ni kwa sababu kingereza ni lugha ambayo hawaitumii katika shughuli za kila siku, lugha ya kingereza hutumika wakati wa kujifunza darasni tu na hata wanafunzi wanapofanya mawasiliano wao kwa wao darasani hutumia kiswahili walichozoea.

Wanafunzi wengi katika mitihani yao ya mwisho wakati wa kujibu maswali hujikuta wakichanganya misamiatia ya kiswahili na kiingereza kwa wakati mmoja. Suala hili linaifanya elimu yetu iendelee kuwa duni kwani wanafunzi hujikita kwenye kukariri baadala ya kuelewa maudhui yanayofundishwa, hali ambayo huwafanya wanafunzi kukosa ubunifu katika maisha yao ya kila siku baada ya kuhitimu katika ngazi mbalimbali za elimu.

Wahitimu wanashindwa kuiweka elimu yao waliyoipata katika vitendo ili iwasaidie kujikwamua katika tatizo la ajira, wanashindwa kufanaya hivyo kwa sababu wakati wakiwa shule walikuwa wanakariri kwa ajili ya kujibia mtihani tu. Ili tuweze kuwasaidia wanafunzia kujifunza kwa uhuru, kiswahili kinatakiwa kutumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia kwa ngazi zote za elimu kama ilivokuwa kwa nchi nyingine Duniani wanaotumia lugha zao za asili katika ufundishaji na ujifunzaji mfano mzuri wa mataifa hayo ni Uchina , Ujerumani na Korea.

Kuna watu huleta hoja kuwa kama Tanzania tukiamua kutumia kiswahili kama lugha ya kufundishia tutashindwa kushindana katika masoko ya ajira Duniani, hii sio kweli kwa sababu tumeshuhudia wachina wakichukua mikataba mbalimbali ya kufanya kazi hapa Tanzania, na wao ni miongoni mwa nchi hapa Duniani wanaotumia lugha ya asili kufundishia na kujifunzia katika ngazi zote za elimu.

Wengine hutumia hoja ya kiswahili hakina msamiati wa kutosha katika kutafsiri maneno ya kisayansi na maneno mapya yanayogunduliwa kulingana na sayansi na teknolojia, hoja hii nayo sio kweli, kiswahili tumeshudia kikitumika katika mikutano mikubwa na katika vyombo vya habari hapa Duniani.

Pili, Maudhui katika mada/ moduli yaendane na mazingira
Kuna mada nyingine zipo katika baadhi ya masomo hazilengi kuwasaidia wanafunzi moja kwa moja wanapokuwa wamehitimu, ukichunguza vizuri katika somo la historia limejukita katika historia ya watu wengine.Ili kuweza kwenda sawa kuna haja ya kuiweka historia ya nchi yetu katika vitabu ili isomwe vizuri lakini vile vile mila, desturi na utamaduni wa watanzania kwa ujumla.

Sehemu kubwa ya madhui ya katika somo la historia inaelezea mambo ya ukoloni na kuhitimisha kwa kuonesha kuwa hali ya umasikini tulionayo imetokana na ukoloni bila kutoa suluhisho nini sasa kifanyike ili kuondokane na hicho kilicho sababishwa na wakoloni.

Baadala ya kuweka mada hizo ambazo baada ya kujifunza, wanafunzi hujenga chuki dhidi ya watu wenye rangi nyeupe ziwekwe mada zinazohusiana na "maendeleo" ili kuweza kukata huu mnyonyoro wa umasikini na kuwajengea wanafunzi uzalendo kwa nchi yao na kuachana na fikra za ukoloni na kutawaliwa na hasira walizonazo juu ya watu wa ulaya wazielekeze katika kazi.

Tatu na mwisho, Elimu kuifanya kuwa kipaumbele cha kwanza kwaTaifa letu,
Karika bajeti ya serikali kwa kila mwaka, fedha zinazoelekezwa wizara ya elimu hazitosherezi mahitaji ya wizara. Ili elimu iwe na uhalisia serikali haina budi kuwekeza katika elimu kwa kupanga bajeti inayoeleweka kwa wizara ya elimu.

Kumekuwa na propagada kuwa uduni wa elimu yetu unatokana na "sera ya elimu" sio kweli tatizo ni bajeti, kutokana na bajeti kutotoshereza baadhi ya vipengele katika sera huachwa bila kutekelezwa, kwa mfano ukiiangalia sera ya elimu ya 2014 (ETP 20114) inaonesha kuwa elimu ya lazima kuwa miaka 10 yaani msingi miaka 6 na miaka minne sekondari lakini kutokana na ufinyu wa bajeti kipengele hiki kimebaki katika maandishi. kwahiyo shida ipo kwenye utekelezaji wala sio sera, bajeti ndio inayoangusha utekelezaji wa mambo ambayo yapo katika sera yetu ya elimu.

Kwa maelezo mafupi ya kuhitimisha nasisitiza matumizi ya lugha ya kiswahili katika ngazi zote za elimu kama lugha ya kufundishia na kujifunzia hii itatoa mawanda mapana kwa walimu na wanafunzi wakati wa kujifunza na kufundisha hii itatupeleka katika nchi tunayoitaka ambayo sio tegemezi kukoka nchi nyngne kwani elimu yetu itakuwa na uwezo wa kuzalisha watalaam wengi makini na mahiri katika taaluma zao, wahitimu katika ngazi mbalimbali watakuwa na uwezo wa kufanya gunduzi nyingi ambazo zitakuwa na tija kwa taifa letu hapana shaka utakubalina na mimi kuwa lugha ya kingereza kutumika kama lugha ya kufundishia na kujifunzia imewafanya vijana wa kitanzania kuonekana hovyo pamoja na elimu walizona kwani wamekuwa wakishindwa kutatua matatizo yanayowakabili kama vile janga ukosefu wa ajira ambalo limekuwa tatizo kubwa kwa vijana wengi wa kitanazania.
 
Back
Top Bottom