Sera na Ilani ya Uchaguzi ya CCM: Uwezo wa Kufikiri na Udandiaji wa Hoja

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
22,128
49,388
Wakuu Heshima.

Hapana shaka mambo kadhaa yanayolitikisa taifa kwa sasa kwa umuhimu wake kwa wananchi na taifa kwa ujumla yameasisiwa na vyama vya upinzani na baadhi ya mambo hayo yanaonekana kwenye Ilani na Sera rasmi za vyama hivyo. Ilitegemewa kabisa kwamba CCM, kama chama tawala na kilichokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi na chenye kufahamu mahitaji muhimu ya taifa kuliko chama kingine chochote, kingekuwa cha kwanza kuainisha mambo hayo kwenye sera na ilani yake lakini jambo la kushangaza hakikufanya hivyo!

Badala yake CCM imekuwa "ikidandia" hoja muhimu kutoka upinzani na kutaka kuwaaminisha wananchi kwamba ndicho kilichoasisi hoja husika. Jambo la kujiuliza hapa, je, CCM imeishiwa kiasi hicho kisera na hata kukosa muono na uwezo wa kuainisha na kutekeleza mahitaji ya msingi ya kitaifa? Hiki chama kinaelekea wapi? Hebu tuangalie baadhi ya mambo yaliyolitikisa taifa tangu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010 na ambayo sasa yamegeuzwa kuwa ya ki-CCM. Je, CCM itaweza kuyatekeleza kwa kiwango na ubora unaotakiwa? Ikishindwa itakuwaje? Haioni inazidi kujichimbia kaburi na hata kuwapa wengine hoja kwa chaguzi zijazo?

Badala ya kujenga hoja madhubuti zenye mashiko kwa wananchi imekuwa ikitumia hoja dhaifu kama kuwatia wananchi hofu kwa hoja za UDINI, UKABILA, UKANDA, AL-SHABAAB, VITA, na ku-attack PERSONALITIES kama turufu ya kisiasa. Wananchi watakaposhtuka (na wemengi tayari wameshtuka) juu ya hofu hizi zinazoingizwa kwenye jamii na CCM na vyombo vya usalama, chama hiki kinadhani bado kitaendelea kubaki salama? TUJADILI.

(i) UFISADI: Kimsingi hoja hii iliasisiwa na CHADEMA kupitia Mkutano wa Mwembeyanga, Dar hapo Septemba 15, 2007. UFISADI ni suala linalokera walio wengi lakini cha ajabu CCM, pengine kwa "ulevi tu" kupitia kwa Katibu Mkuu wake wakasema UFISADI haukuwa kwenye KAMUSI YAO! Baada ya mambo kuwa magumu, sasa "wanachezeshwa" "NGOMA YA UFISADI" hadi wameibuka na neno "jipya" - GAMBA. Kama walikuwa dhamira njema kwa nini hili halikuzungumziwa kwenye kampeni zao?

(ii) KATIBA MPYA: Hoja hii ilibebwa na CHADEMA kwenye kampeni na ipo kwenye Ilani yao. CCM wakajidai Katiba iliyopo inatosha lakini baada ya kuona moto umesambaa sasa "wameiteka" hoja! Hivi tangu mwanzo watunga sera wa Chama hawakuona hili? Je, kwa udandiaji huu, watafanikisha?

(iii) MAKAZI BORA: Hoja hii ilibebwa pia na CHADEMA wakati wa kampeni hadi kufikia mahali pa kubezwa na CCM. Jana/juzi tumemsikia Mh. January Makamba (CCM) eti "akileta" hoja binafsi Bungeni kuhusu makazi bora kwa wananchi. Walikuwa wapi hawa jamaa?

Je, kwa udandiaji huu CCM itatufikisha kunakotakiwa na yenyewe itabaki salama? Au ndio ile kauli yao maarufu kwamba eti kazi ya vyama vya upinzani ni "kuishauri serikali"? Wakuu karibuni tuongeze na mengine.
 
Back
Top Bottom