Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya kuanza rasmi zoezi la sensa ya watu na makazi, kumeibuka changamoto mbalimbali ikiwemo watu kusambaza vipeperushi vinavyozuia wananchi kushiriki sensa na katika baadhi ya maeneo makarani wakigoma kula kiapo kwa kuwa hawajalipwa posho ya kufanyakazi hiyo.
Hii ni kwa mujibu wa uchunguzi wa NIPASHE katika mikoa mbalimbali nchini uliofanyika jana.
Mkoani Tanga, kundi la watu wasiofahamika limesambaza vitabu na vipeperushi vinavyowataka wananchi kutoshiriki zoezi hilo.
Mratibu wa sensa mkoa wa Tanga, Toni Mwanjota, aliiambia NIPASHE kwamba vitabu na vipeperushi hivyo vimekuwa vikitolewa kwa siri kubwa.
"Tumesikia kuwa vipo vitabu na vipeperushi ambavyo vinatolewa na watu wasiopenda maendeleo ila vinatolewa kwa siri sana lakini tunavifanyia kazi," alisema.
Hata hivyo, aliwataka wananchi kutambua kuwa ni kosa kisheria kufanya hujuma yeyote inayolenga kukwamisha sensa.
Visiwani Zanzibar, Jumuiya za Kiislam Zanzibar zimetoa masharti kadhaa ambayo kama hayatatekelezwa, taasisi hizo zitaendelea kuwashawishi wafuasi wake kususia zoezi la sensa visiwani humo.
Tamko hilo lilitolewa na kiongozi wa jumuiya hizo, Sheikh Mselem Ali Mselem, katika mkutano na waandishi wa habari uliotishwa kutoa msimamo juu ya ushiriki wa wananchi wa Zanzibar katika zoezi la sensa itakayofanyika nchini kuanzia Jumapili ijayo.
Sheikh Mselem ambaye ni Amir wa mwavuli uitwao Umoja wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Zanzibar, alisema taasisi hizo zinataka serikali itekeleze haki ya kisheria kwa wananchi kupewa vitambulisho vya Uzanzibari.
Alisema pamoja na kuwapatia vitambulisho wote wanaostahili, serikali pia iwaamuru wote waliopewa vitambulisho hivyo kwa utashi wa kisiasa kuvirejesha.
Sheikh Mselem alitaja sharti lingine ambalo taasisi hizo zinataka litekelezwe ni kuingizwa kwa kipengele cha dini katika dodoso za sensa hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, amesema zoezi la sensa limekumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa
kikundi cha watu wachache ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu waliokuwa wakipinga zoezi hilo.
"Hiki ni kikundi cha watu wachache wenye dhamira chafu ya kutaka kukwamisha zoezi hili, watu hao wanapatikana katika wilaya za Same, Mwanga, Hai na Moshi Manispaa, walikuwa wanajipatia kazi zisizo na mshahara kwa kupita na kuwahamasisha wananchi ili waweze kupinga zoezi la hilo," alisema.