Sensa na vitambulisho vya urai

DCM

Senior Member
Apr 13, 2012
163
98
Hivi kupitia vitambulisho vya urai huwezi kujua idadi ya watu wako katika nchi? Kuna sababu gani ya vyote kufanyika ktk mwaka mmoja?
 
Mimi kama mimi siono sababu ya kutumia pesa nyingi kwenye sensa, wakati kwa kupitia vitambulisho vya urai,serikali inaweza kujua idadi ya watanzania kwa ujumla.

Wakati hiyo pesa ingewezakutumika kwenye idara nyingine kwa maendeleo ya taifa.
 
Huenda kuna namna walivyotathmini na kuona vifanyike vyote. Binafsi sioni haja ya kufanya hayo yote!
 
Hilo ni wazo zuri mkuu, ingawa maswali au taarifa zinazo hitajika katika sensa zinaweza kuwa tofauti na zile za vitambulisho vya taifa.
 
Kama hela zipo, acheni vyote vifanyike separately tuliosoma tupate allowance kujazia salary
 
Jamaa karudi home usiku wa manane. Moja kwa moja akazama chumbani, akafunua blanketi, akaiona miguu minne badala ya miwili aliyozoea.

Jamaa akafunika blanketi taaratibu, akachukua bonge la rungu, akaitwanga ile miguu kwa nguvu zote halafu
akaelekea sebuleni kutuliza hasira.

Kutahamaki akamkuta mkewe amejipumzisha sebuleni. Mkewe
akamwambia: Wazazi wako wamekuja leo kututembelea, nimewaachia chumba chetu walale, sisi tutafanya maarifa mengine."
 
hakuna kitu kinacho fanywa na serikali ya ccm perfect. Mda si mrefu tutaanza kukusanya kero za vitambulisho. mia
 
Jamaa karudi home usiku wa manane.Moja kwa
moja akazama chumbani,akafunua blanketi,akaiona
miguu minne badala ya miwili aliyozoea.Jamaa
akafunika blanketi taaratibu,akachukua bonge la
rungu,akaitwanga ile miguu kwa nguvu zote halafu
akaelekea sebuleni kutuliza hasira.Kutahamaki
akamkuta mkewe amejipumzisha sebuleni.Mkewe
akamwambia:Wazazi wako wamekuja leo
kututembelea,nimewaachia chumba chetu
walale,sisi tutafanya maarifa mengine."

Hahahahaaaaaaaa u made ma evening.
 
Ni kweli vitambulisho ni kuanzia 18ers kupanda lakini sensa ni kwa watu wote.

Pia sensa inakusanya takwimu nyingi zaid mfano idadi ya vifo within five yrs and twelve months. Isitoshe takwimu nyingine kama shughuli za uchumi, takwimu za uzazi, kiwango cha elimu na takwimu nyingi zaidi ambazo hazipatikani kwny national IDs.
 
Nadhani ipo haja vyote kufanyika kama wachangiaji wengine walivyosema hapo juu. Tatizo nadhani ni mfumo unaotumika katika kufanikisha vyote viwili.

Mfano vitambulisho vua utaifa ni adhabu kuamka saa 9 usiku kama kile kipindi cha maduka ya ushirika kuwahi foleni.
 
Back
Top Bottom