Sengerema: Kikongwe wa Miaka 102 Afunga Ndoa na Mkewe Mwenye Miaka 90

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,210
50,000
Hongera kwao ila mwenye miaka 90 anaonekana Mzee Kupitia wa miaka 102.

=====

Masasila Kibuta (102) mkazi wa kijiji cha Nyamazugo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza ameshangaza umati wa waumini wa Kanisa Katoliki Kigango cha Nyamazungo baada ya kufunga pingu za maisha na mkewe Chem Mayala (90) kanisani hapo.

Ndoa hiyo imefungishwa na Padri wa Parokia ya Ngomamtimba Padri Julian Mondula jana Jumamosi Juni 17, 2023 huku Padri Mondula akiwataka vijana kuiga mfano bora wa wazee hao wa kufunga ndoa katika mazingira yoyote.

Kwa upande wake Mzee Kibuta amesema Chem Mayala ni mke wake wa pili kufunga naye ndoa baada ya mke wa kwanza kufariki dunia ambaye aliishi naye upendo mkubwa na walijaliwa kupata watoto 12.

Mzee Kibuta amesema aliishi na Chemi bila kufunga ndoa takatifu hivyo walishauriana na kukubaliana kwenda kubarikia ndoa yao kanisani ili kuwa wasafi mbele za mungu.

"Nimefunga ndoa hii kanisani ili nikifa nikaonane na Mungu kwa kutimiza agano la ndoa takatifu kama maandiko yanavyosema,” amesema Mzee Kibuta.

Amesema njia pekee na kuduma katika ndoa nikuwa na uaminifu, upendo, uvumilivu wakati wa shida na raha sambamba na kusameheana wakati wanandoa wanapokoseana.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom