Seminari Kipalala wavamiwa - in progress!!

Wakishakamatwa wafanyiwe utafiti ni kwanini wavamie sehemu hiyo. Yawezekana ni matatizo ya kijamii yamewasababisha kufanya vitu vya namna hiyo.

Hii serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ndo wawe proactive au unazungumzia nini? Wao shida ni kukamata watu nyang'anya pesa/simu zao waachiwe wengine na wengine mahakamani.
 
Jamani Jamani.... Mbona wanawatia hasara watu wa Mungu hawaaa.. Hawajui Kwa mwaka huu wa fedha 2009/10 wamefutiwa msamaha wa kodi hawa, sijui watafidia vipi mali zilizoibiwa??? We acha tu.....

POLENI SANA MAPADRE NA MAFRATERI WA KIPALAPALA
 
Poleni sana wana Kipalapala. Inawezekana ni njaa tu za majambazi uchwara.Tunasubiri kujua zaidi kulikoni
 
Inasikitisha sana! majambazi wamefanikiwa kuchukua kiasi kikubwa cha fedha, pamoja na zawadi za padri mpya ikiwa ni pamoja na fedha za padri huyo zisizopungua M1, baadhi walipigwa pigwa mapanga akiwemo Fr Kibobera ambaye hadi sasa amelazwa hospitali ya mkoa ya Kitete-Tabora
 
Sasa si wataiba biblia,misale na divai tuu bila shaka.Labda na mifugo
Sasa tuendako siko kabsaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nimeitafakari sana thread hii na posts zilizochangiwa lakini nimeshindwa kabisa kuelewa mantiki ya kuwekwa kwake. Tutaweka thread ngapi kuhusu matukio ya ujambazi hapa nchini1 Mzee MK what is happening? tunataka mada za kuwabana mafisadi na wapambe wao.
 
Poleni sana jamani ssijui kama wamepata msaada kwa muda muafaka....maana ni mbali sana toka police kama 9kms hadi ufike kule......sijui poleni sana
 
Umejuaje? Wee wtoka huku? Nafikiri ukweli utajulikana soon.
Pole Mapadre wetu wa Kipalapala.
Kwani Sikonge ulikuwa wapi siku zote? Mpaka ulivyosikia seminary ya Kipalapala imevamiwa lakini mtoa habari alikosea akasema Kipalalala badala ya Kipalapala. Hata hivyo nikupongeze kwa kupenda kwenu maana waswahili husema msahau kwao ni mtumwa
 
Nimeitafakari sana thread hii na posts zilizochangiwa lakini nimeshindwa kabisa kuelewa mantiki ya kuwekwa kwake. Tutaweka thread ngapi kuhusu matukio ya ujambazi hapa nchini1 Mzee MK what is happening? tunataka mada za kuwabana mafisadi na wapambe wao.
Zak Malang naona una matatizo watu wanavamiwa na majambazi wewe unasema mada hiyo haina mantiki watu wanaweza kuwa wamekufa kule wewe unataka mafisadi tu sikuelewi una maana gani
 
Nimezipata, japo kwa ufupi kutoka kwa mmoja anayeishi hapo.
Kisa chenyewe kimetokea katika parokia ya Kipalapala iliyopo karibu kabisa na seminari. Hapo parokiani alikuwepo padre mpya, siku chache tu toka apadirishwe. Majambazi hao walitaka kupora vijizawadi alivyozawadiwa kijana huyu na waamini katika kumpongeza kwa kuupata upadre. Kwa kweli, kadiri ya mzungumzaji, hapakuwa na vitu vya thamani kiasi cha kuwafanya majambazi wurushiane risasi na walinzi wa seminari! Wanasema majambazi walifaulu kuchukua vitambaa vya kushonea nguo na zawadi nyinginezo na pia kiasi fulani cha pesa.
Padre mhusika hakupigwa kwani alitulia humo ndani mwake, wavamizi hawakumwona. Padre mwingine ndiye aliyeteswa sana na kujeruhiwa, akishurutishwa kutoa chochote hasa hizo zawadi alizopewa padre mpya.
Kilio kiliposikika wanakijiji waliizingira parokia, ndipo wavamizi waliaanza kurusha risasi hewani. Wanakijiji walijitahidi kutumia zana walizokuwanazo kama vile mawe, na wavamizi walianza kutafuta mpenyo kutoroka. Njia waliyopitia ndio hapo seminarini, ambapo walipita huku wakirusha risasi. Walinzi wa seminari walianza kujibu mapigo na wanachuo/waseminari walipasika kujificha kwa muda. Mambo yaya yalidumu kwa muda wa nusu saa hivi, na Polisi walifika eneo la tukio baada ya majambazi kukimbia, bila shaka watawasaka ili sheria ichukue mkondo wake.
Basi hivyo ndivyo nilivyozipata, nimeandika kwa ufupi.
Ninatoa pole nyingi sana kwa wanajumuia wote wa Kipalapala. kwa namna ya pekee, huyo padre majeruhi, na wote walioathirika kwa namna moja au nyingine. Ni kitu cha kushangaza kidogo, zawadi za upadirisho tu ndizo zinasababisha yote haya!
 
Back
Top Bottom