Semina elekezi za ngurdoto

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,581
1,069
Wana JF naomba kuuliza;

-Malengo/shabaha za semina elekezi kwa watumishi wa serikali kule Ngurdoto zilikuwa nini?
-Mpaka sasa tunaweza kufanya tathmini yoyote kupima kama malengo hayo yamefikiwa au la? Na kama hayajafikiwa ni kwa nini?
 
Mimi nadhani hututendei haki kutuuliza silly questions like what you have asked. Kwa kukusaidia naomba nikushauri hivi:-

Kamuulize Vasco Da Gama aka Mzee wa Kujibu Mapigo aka Mzee wa Kubembea aka Mzee wa Kuuza Sura aka Mzee wa Kuchekacheka.

Yupo jirani kabisa na iliko wizara inayoongozwa na Profesa lakini ina madudu kuliko wizara ya SHETANI wenyewe wanaiita wizara ya Elimu
 
Kikwete anasitahili ashitakiwe kwa ubadhirifu wa fedha za umma kwa kuendesha semina elekezi zisizo kuwa na tija.
 
Wana JF naomba kuuliza;

-Malengo/shabaha za semina elekezi kwa watumishi wa serikali kule Ngurdoto zilikuwa nini?
-Mpaka sasa tunaweza kufanya tathmini yoyote kupima kama malengo hayo yamefikiwa au la? Na kama hayajafikiwa ni kwa nini?
Matokeo yapo wazi, Muulize waziri Sophia Simba atakupa tathmini!
 
Malengo yamefikiwa ndugu yangu.Lengo lao kubwa wala halikuwa ni kuelekezana ila ilikua ni kupeana ulaji na kufanya anasa.Hiki ndicho ninachokijua mimi.
 
Ni AIBU kwa viongozi wote waliohudhuria hizi semina. Inaonekana hawakuwa wanasikiliza na kujifunza bali walikuwa wanajinafasi kwa starehe wakishangaa mazingira ya Ngurdoto kwa gharama za wavuja jasho walipa kodi!
SHAME!
 
Walikuwa wanaelekezana namna ya kula pesa ya mlipa kodio na kuficha siri zote zina expose ulaji wao wa pesa za Umma . Wamefanikiwa kiasi fulani maana ambao hawakula wanatoa info kwa kuwa hawakupata lolote .
 
Back
Top Bottom