Sekondari Makurunge yakaidi amri ya serikali

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Sekondari Makurunge yakaidi amri ya serikali

na Abdallah Khamis

amka2.gif
WAKATI serikali ikipiga marufuku shule kuwarudisha nyumbani kwa kukosa ada ama kulipa michango mbalimbali, shule ya sekondari Makurunge iliyoko wilayani Kisarawe, Pwani, imepinga hatua hiyo kwa kuwarudisha baadhi ya wanafunzi wake kwa kushindwa kulipa michango shuleni hapo.
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, mwalimu mwandamizi wa taaluma shuleni hapo, aliyefahamika kwa jina moja la Mende, alikiri kurudishwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule hiyo kwa ukosefu wa ada na michango kwa muda wa miaka mitatu sasa.
Alisema walikubaliana na wazazi na bodi ya shule kwamba ifikapo Januari 17 mwaka huu wawe wameshalipa madeni yote waliyokuwa wanawadai wanafunzi hao, na kubainisha kuwa madeni hayo yanatokana na michango ya rimu, madawati na ada.
“Ninachoweza kukuambia hao wanafunzi tunawadai fedha za michango mbalimbali na kama serikali inasema tusichangishe wajue kwamba haya ni madeni ya miaka mitatu nyuma,” alisema mwalimu Mende.
Alisema kuwa wao wanaendesha shule kwa michango ya wanafunzi na kwamba suala la kuzuia michango hiyo liko kisiasa zaidi kwa kuwa wasemaji wa kauli hizo huzitoa kwa dhamira za kisiasa na si kuangalia taaluma inataka nini.
Aliongeza kwamba sio wanafunzi wote waliorudishwa majumbani bali ni baadhi yao ambao alishindwa kukumbuka idadi yao na kumtaka mwandishi asiandike chochote vinginevyo angeshtakiwa.
“Ninachoweza kukwambia ni kwamba usiandike hizi habari kwani kuna baadhi ya wanafunzi ni waropokaji wa mitaani, kama unaweza njoo tuonane, vinginevyo nitakushtaki kama utaandika habari hizi,” alisema mwalimu Mende.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Hajjat Amina Saidi alipoulizwa juu ya kadhia hiyo alisema hazijamfikia na ndio kwanza anapata taarifa hizo kutoka kwa mwandishi wa habari hizi.
 
PHP:
WAKATI serikali ikipiga marufuku shule kuwarudisha nyumbani kwa kukosa ada ama kulipa michango mbalimbali, shule ya sekondari Makurunge iliyoko wilayani Kisarawe, Pwani, imepinga hatua hiyo kwa kuwarudisha baadhi ya wanafunzi wake kwa kushindwa kulipa michango shuleni hapo.
  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, mwalimu mwandamizi wa taaluma shuleni hapo, aliyefahamika kwa jina moja la Mende, alikiri kurudishwa kwa baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu wa shule hiyo kwa ukosefu wa ada na michango kwa muda wa miaka mitatu sasa.

Tusishangae kwa sababu nchi hii hivi sasa ni kichwa cha mwenda wazimu kila mmoja aweza kujifunzia kunyoa tu bila ya zengwe lolote lile,..............................
 
Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, mwalimu mwandamizi wa taaluma shuleni hapo, aliyefahamika kwa jina moja la Mende

Haya majina mengine ni balaa.....Mende
 
Back
Top Bottom