Bra-joe
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,562
- 986
Nimefanya kauchunguzi kidogo kwa ndugu na rafiki zangu waliooa/olewa. Nimegundua maisha ya ndoa yamegawanyika ktk sehemu kuu 3. Ambazo ni KIZUNGU, KICHINACHINA na KIENYEJI. 1.Kizungu huwa mara tu baada ya ndoa mpaka miezi kadhaa. Mambo yao sasa: mabusu kibao na kuambiana jinsi wanavyopendana, mume akirudi ataulizwa mambo yote ya kazini kwa upole, full out na unyumba kwa sana. 2. Kichinachina: hapa no out, unyumba kwa mbaali, mume akitoka kazini baada ya salamu anaambiwa chakula kipo mezani then no story, ugomvi huzuka mara kwa mara lkn hakuna mtu mwingine atakayejua zaidi yao, hupeana majibu ya mkato na mume huanza kuchelewa kurudi nyumbani. 3. Kienyeji: hapa ni kivumbi cha kufa mtu, ugomvi mpaka majirani wanajua, full kutupiana lawama,"ningejua nisinge kuoa" "ningeolewa na mume bora kuliko wewe", ufikia kipindi kila 1 anaomba mwenzake afe au waachane. Wana ndoa mpooo?