Secret admirer; hii ipo jamani?

Mimi simlaumu sana huyo dada... hiyo ipo sana, kwani si kila mtu ana ujasiri kama mnavyofikiri, wengi wetu tupo hivyo kwa namna moja ama nyingine...
 
hiyo ipo sana jamani nimewai kupata mdada wa ivyo yalipomchinda alinieleza bayana na wakati huo nilikuwa nimependa mahali kupitiliza nikamwambia nipo engage aliumia sana na sikumwona tena na kanisa akahama
 
NAANZA KUONA OPPERTUNITIES ZA KIJASIRIAMALI HAPA KWENYE JUKWAA LA MAPENZI..FL- mwambie huyo binti asipate taaabu..mie najitolea kum-imbishia mpaka mshkaji aingie laini..sema issue ni pale mshkaji atapo hit n run...naona huyo rafikiyo ATAJIUA MAANA ATAKUWA AMEMWAGWA na mnavyojua kulia eti mmechezewa basi ni balaa tupu...mwambie anipatie particularz za muhusika nianze kumlia mingo za kufa mtu...ndani ya 2weeks lazma wapate dinner pamoja... ila atalipia gharama zangu za hiyo consultancy nitayomfanyia.
hahahahaah ngoja nikutumie PM contact zote labda unaweza kumsaidia
 
mie nimeolewa mpendwa nakaribia kupata wajukuu.

Haijalishi best. Wazee wanatamani kweli kweli. Ukitaka nenda Mombasa au Arusha uone wenye vitukuu wanavyokimbilia Virasta vichafuchafu . Feelings hazina cha uzee wala nini.
 
mie nimeolewa mpendwa nakaribia kupata wajukuu.

Halafu haka 'kaugonjwa' ukikapata wakati umeolewa/umeowa ndio kanasumbua zaidi! Huyo dada anashangaza kweli yaani analilia 'mali' ya watu!
 
Haijalishi best. Wazee wanatamani kweli kweli. Ukitaka nenda Mombasa au Arusha uone wenye vitukuu wanavyokimbilia Virasta vichafuchafu . Feelings hazina cha uzee wala nini.

Am committed bwana nikiwa na feelings za hivyo itabidi nijitahidi ku-ignore
 
Hili ni jambo la kawaida kwa madada walio wengi. Kwa tamaduni za kiafrika inakuwa ni vigumu kwa mwanamke kumuapproach mwanaume na akijilengesha sana anaweza kuonekana hajatulia. I have similar experience, kuna mwalimu mmoja aliyekuwa jirani yetu alitokea kunizimia sana. Kwa kuwa tuliheshimiana kama majirani sikuwahi kuhisi kama alinimind alipokuja kunitazama nilipougua akaniletea juice, alipokuja ofisini kuomba msaada wa usafiri nikamwambia dereva ampeleke akasema angependa nimpeleke mimi, nk nk. Mpaka siku alipoamua kumueleza ukweli rafiki yangu wa karibu ambaye walikuwa wamezoeana. Kumbe mtu unaweza kupitwa na riziki hivi hivi........!!
 
Kuna Binti hapa kaniacha hoi mie labda na nyie atawashangaza
Huu ni mwaka wa pili sasa yuko kwenye hiyo secret admirer na kaka mmoja ,
Kila siku binti anategeshea amuone huyu kaka ndo apande gari aliyopo,Lunch time anategea mida ya huyo kaka kwenda lunch ndiona yeye anaenda amekuwa kama mtumwa wa penzi na kusema hawezi.
Cha kushangaza jana tumeenda kwenye Party moja,,,,Binti akiwa anaenda Toilet kamkuta huyo secret admirer wake amekumbatiana na mdada mmoja wa haja wanakiss
Kaja kuniaga huku anabubujikwa chozi eti anaenda home hawezi kuendelea na partyl,leo hajafika kazini namuuliza kulikoni kanipa mkasa kamili...
Kumwambia amesema hawezi tena sasa anauguza majeraha ya mapenzi
Hii imekaaje wadau?:A S 39::A S 39:
hehehe hii stori yote ni kitu cha kawaida, kitu ambacho si cha kawaida ni hapo mdada alipoanza kulia na kutokuja kazini . mshauri ajiunge JF halaf amPM da sophy apate ile mikoba ya kuteka nyara waliomilikiwa.:bathbaby:
 
Msaidie wewe FL1 .nenda kamwambie huyo kaka kuhusu huyo dada anayempenda.Ili ajue moja kama Gender Sensistive
 
halafu haka 'kaugonjwa' ukikapata wakati umeolewa/umeowa ndio kanasumbua zaidi! Huyo dada anashangaza kweli yaani analilia 'mali' ya watu!

smu katakusumbuaje wakati tayari una mali yako binafsi ?????
Kaugonjwa mpaka unaugua ..no no no....
 
Msaidie wewe FL1 .nenda kamwambie huyo kaka kuhusu huyo dada anayempenda.Ili ajue moja kama Gender Sensistive
hehehe ukiisoma vizuri hii habari, ni kwamba huyo mdada alikuwa anamtuma FL1 akamwambie huyo mkaka (body lengueji), lakini FL1 ndo kwanza anatafuta ushauri JF. dah! sasa hapa mdada inabidi abadilishe lawyer tu kama FL1 hawezi.
 
Hili ni jambo la kawaida kwa madada walio wengi. Kwa tamaduni za kiafrika inakuwa ni vigumu kwa mwanamke kumuapproach mwanaume na akijilengesha sana anaweza kuonekana hajatulia. I have similar experience, kuna mwalimu mmoja aliyekuwa jirani yetu alitokea kunizimia sana. Kwa kuwa tuliheshimiana kama majirani sikuwahi kuhisi kama alinimind alipokuja kunitazama nilipougua akaniletea juice, alipokuja ofisini kuomba msaada wa usafiri nikamwambia dereva ampeleke akasema angependa nimpeleke mimi, nk nk. Mpaka siku alipoamua kumueleza ukweli rafiki yangu wa karibu ambaye walikuwa wamezoeana. Kumbe mtu unaweza kupitwa na riziki hivi hivi........!!

Ambassador baada ya kuambiwa ukweli na huyo dada ulidumisha mila ama ikawaje hapo hujamaliza habari kamili??
 
Ambassador baada ya kuambiwa ukweli na huyo dada ulidumisha mila ama ikawaje hapo hujamaliza habari kamili??

Teh teh teh teh! Uchokozi huo sasa FL1. Ndo maana nikasema saa nyingine unaweza kupitwa hivi hivi kwa kuzubaa kwako. Anyway, sikupenda kumtesa mtoto wa watu bure na ku-misuse resource, kwa kuwa nilikuwa free na mtoto mwenyewe alikuwa analipa ilibidi nidumishe mila.
 
hehehe hii stori yote ni kitu cha kawaida, kitu ambacho si cha kawaida ni hapo mdada alipoanza kulia na kutokuja kazini . mshauri ajiunge JF halaf amPM da sophy apate ile mikoba ya kuteka nyara waliomilikiwa.:bathbaby:

hhahaha ndo hapo mie nikajiuliza hivi mapenzi ni ugonjwa ???
 
FirstLady1 unaweza kumsaidia mwenzako kwa kufikisha ujumbe kwa huyo bwana anayekuwa dmired.

By chance unaweza kukuta wote wawili ni secret admirers wa each other na wanaogopana tu, ukitekenya tu mambo msweno.

Kiranga du naona kama mtihani mgumu mie ...hebu ngoja na mie nijipe muda wa kufikiri nyie wanaume hamtabiliki kabisa niko na huyu binti hapa namchukua maelezo..
 
Msaidie wewe FL1 .nenda kamwambie huyo kaka kuhusu huyo dada anayempenda.Ili ajue moja kama Gender Sensistive

Mpendwa katika bwana itabidi unipe mbinu mbadala hivi akikataliwa si ndo atakufa huyu dada ..mapenzi gani haya ya kuuguzana .??
 
Back
Top Bottom