Sawa, Hussein Bashe SIO Mtanzania: Na hawa JE?

Kuna maswali mengi ambayo hatupati majibu-:
1.Je Bashe ni raia watanzania au Somalia na Somalia ipi?
2. Je Bashe alivyotimiza miaka kumi na nane aliukana uraia wa Tanzania?
3.Je Bashe anayo hati ya kusafiria yaani passport ya Tanzania?
4.Kama anayo passport nani wa kulaumiwa Uhamiaji au CCM au yeye?
5.Je Bashe ni Tishio kwa usalama wa Tanzania na CCM au ni chuki binafsi?
 
mkianza kutafutana uchawi nani raia na nani sio mtaishia kuuwana tuu...civil war nyingi zinatokana na tabia kama hizi za baadhi ya watu kwenye society kujiona wao ndio wenye nchi kuliko wengine,nawashauri acheni tabia za kishenzi kama hizi hazitawasaidia kitu
 
Kwenye red - my answer: We have in this country sheep for humans!

You are a genius. Ushishangae wafanyakazi wa umma wakampigia kura kwa kishindo huyu mheshimiwa pamoja na kusema hadharani kuwa hahitaji kura zao. Reason? because workers in Tanzania are sheeps.
 
Nataka kujua siri ya hizi nguvu za ajabu za Bw. Ridhiwan Kikwete

- Kumuangusha Masauni kutoka kwenye Uenyekiti wa UVCCM kwa kashfa ya kughushi umri
- Kumuangusha hasimu wake mkubwa Bw. Bashe kwenye ubunge kupitia Kamati kuu kwa zengwe la uraia
- Kumuangusha Kifukwe kutoka kwenye Uongozi wa Yanga
- Kuongoza kundi la vijana kutafuta wadhamini wa Mgombea Urais kupitia CCM ambae ni baba yake.

Huyu dogo naanza kumtizama kwa jicho la Tahadhari...!

..bora umeona hilo,hii inaweza kuwa hatari kubwa baadaye
 
mkianza kutafutana uchawi nani raia na nani sio mtaishia kuuwana tuu...civil war nyingi zinatokana na tabia kama hizi za baadhi ya watu kwenye society kujiona wao ndio wenye nchi kuliko wengine,nawashauri acheni tabia za kishenzi kama hizi hazitawasaidia kitu

Hakuna nchi duniani ambapo unaweza kuwa kiongozi wa kuchaguliwa bila ya kuhojiwa uraia wako. Sasa unataka kusema kuwa nchi zote duniani zina tabia za kishenzi kwa kuhoji uraia wa viongozi wao?

Je unadhani ni sahihi kuruhusu wageni waje kututawala kwa sababu tu tunapenda kuonekana ni wastaarabu? Kama kuhoji uraia wa viongozi wetu ni tabia ya kishenzi nadhani ushenzi utakuwa umepata maana nyingine nzuri kuliko ile tunayoifahamu.
 
Hakuna nchi duniani ambapo unaweza kuwa kiongozi wa kuchaguliwa bila ya kuhojiwa uraia wako. Sasa unataka kusema kuwa nchi zote duniani zina tabia za kishenzi kwa kuhoji uraia wa viongozi wao?

Je unadhani ni sahihi kuruhusu wageni waje kututawala kwa sababu tu tunapenda kuonekana ni wastaarabu? Kama kuhoji uraia wa viongozi wetu ni tabia ya kishenzi nadhani ushenzi utakuwa umepata maana nyingine nzuri kuliko ile tunayoifahamu.

Huu una kuwa ushenzi pale ambapo kuhoji uraia kunachagua nani wa kuhojiwa ili hali wageni wengine wakiwemo wairani wakiachwa waivuruge nchi kwa mali zetu walizotufisadi!
Ingekuwa kila mwenye uraia wa utata anahojiwa hiyo ingeitwa hekima!.
 
yote haya ni mazingaombwe ya ccm na siasa zake. vinginevyo

- ni vyema ccm wakaujulisha umma ni lini uhamiaji ilifafanua kwamba bashe
si raia wa tanzania.

- aidha inabidi uhamiaji ieleze kwa kigezo gani wameamua kumuachia
mtu ambaye si raia wa tanzania kuendelea kuishi hapa nchini bila
kibali halali na ni hatua gani kisheria ambazo watachukua kwa bashe
iwapo kijana huyu alipatiwa pasi ya kusafiria ya kitanzania (hii ikimaanisha
alitoa taarifa za uongo zilizopelekea yeye kupatiwa pasi)

- je ccm watachukuliwa hatua gani kwa kuendelea kumuachia bashe kushika
madaraka ya chama wakati tayari wamekwishataarifiwa na vyombo husika
kwamba si raia wa tanzania (wamesubiri mpaka kura za maoni)

- je bashe ana haki zipi mbele za sheria hususan ukizingatia ccm walimwachia
aendelee na kupata gharama za uchaguzi wakati wakijua kwamba hatimaye
watamtosa kutokana na kutokuwa raia wa tanzania,
 
Nadhani Bashe wanamshika hapa kwenye kipengele hiki hapo chini: Sasa, according to recent reports zinasema aliomba uraia na kuupata 2009 kama sikosei, na uthibitisho anao na wizara ya mambo ya ndani-uhamiaji wamethibitisha hivyo.

Folks, kama haya yote yanacheck out then Bashe ni mTanzania, period!!
5. Persons born in the United Republic on after Union Day

(1)Subject to the provisions of subsection (2), every person born in the United Republic on or after Union Day shall be deemed to have become and to have continued to be a citizen of the United Republic with effect from the date of his birth, and with effect from the commencement of this Act shall become and continue to be a citizen of the United Republic, subject to the provisions of section 30.
(2)A person shall not be deemed to be or to have become a citizen of the United Republic by virtue of this section if at the time of his birth-
(a)neither of his parents is or was a citizen of the United Republic and his father possesses the immunity from suit and legal process which is accorded to an envoy of a foreign sovereign power accredited to the United Republic
; or
(b)any of his parents is an enemy and the birth occurs in a place then under occupation by the enemy.

 
Watanzania Bwana,
Basi majina yote yamesahaulika, limebaki la mwakalebela na Base tu.
Kama tunataka kuwa objective, tunatakiwa kupitia majina yote, na kukosoa jina kwa jina, si yale tu yanayowekwa kimtego tusahau ukweli na umakini.
Wengi wamepita kimizengwe lakini kimya kimya kwa ajili ya JF kukomalia swala la Bashe na mwakalebela, hamuoni mnafungwa macho?
au ni mchezo wa mdomo?
yani kila gazeti, bashe bashe.....
jamani ina maana kazi yetu ni kudandia kesi na issue za waandishi tu?
 
Sala yangu ya leo.

Ee Mungu, Iokoe Tanzania kutoka katika fikra za kina Chiligati, Makamba, NEC na bosi wao Kikwete. Amsha fikra za watanzania na boresha mboni zao, waone walikotoka, walipo na wanakoelekezwa, Nakemea nguvu za fitna majungu na ubaya unaoelekezwa na CCM dhidi ya Dr. Slaa. Amen.
 
Nadhani tunakosea sana hapa!!
Kama kweli ni nguvu ya Mtoto wa Rais basi mvumilieni tu maana ni nguvu yenye ukomo na inaishia mwaka 2015.
Kama ni kweli, basi Yote yana mwisho!! So it is just a matter of time.
 
Makamba ateta sakata la Bashe


NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yussuf Makamba, amesema kabla ya vikao vya Chama kutamka kwamba aliyekuwa anawania ubunge katika jimbo na Nzega, Hussein Bashe si raia, vilijiridhisha
pasipo shaka. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba mjini Dar es Salaam, Makamba alisema taarifa zilizochapishwa katika magazeti juzi, zikisema CCM imemnyang'anya uraia Bashe si sahihi. Makamba alisema vikao vya Chama havina mamlaka ya kumnyang'anya uraia mtu yoyote, na suala la Bashe ni kwamba, haiwezekani kunyang'anywa uraia mtu ambaye si raia. Alisema wajumbe wa Halmashauri Kuu hawakumnyang'anya uraia kwa sababu hawana mamlaka hayo, na kuna ushahidi usio acha shaka kwamba, Bashe si raia. Alisema kwamba, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuziona nyaraka ambazo zilichapishwa katika gazeti la Tanzania Daima zikidai Bashe ni raia wa Tanzania. "Nyaraka hizo na mimi nimezisoma, lakini kuna mengi zaidi ya nyaraka hizo kuthibitisha kwamba sio raia," alisema Makamba. Katibu Mkuu alisema kwamba vikao vya Chama haviwezi kumuonea mtu na kufafanua kwamba, wazazi wa Bashe walikuwa ni raia wa Somalia, baadaye baba yake aliukana uraia wa nchi hiyo na kuwa Mtanzania, jambo ambalo Bashe naye kwa mujibu wa sheria alipaswa kulifanya kwa sababu alizaliwa na wazazi wasio raia. Kuhusu hatua ya NEC kumteua aliyeshika nafasi tatu katika kura za maoni kugombea ubunge ambaye ni Dk. Hamis Kigwangala badala ya mshindi wa pili Lucas Selelii aliyekuwa akitetea ubunge wake, Makamba alisema Chama kinawajua wanachama wake na kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha mtu asiteuliwe. Katika kura za maoni zilizopigwa nchini kote Agosti mosi, mwaka huu, katika jimbo la Nzega, Bashe alioongoza kwa kura 14,466 akifuatiwa na Selelii mbunge aliyemaliza muda wake kwa kura 2,706 na watatu ambaye ndiye aliyeteuliwa na NEC kugombea ni Dk. Kigwangala aliyepata kura 1,566. Makamba alimsifu Bashe kwamba ni kijana mzuri ambaye alioongoza katika kura hizo, na kuwaomba viongozi wa Chama na wana-CCM kuelewa uamuzi uliofikiwa na NEC. Akijibu swali kwamba aliyekuwa mbunge wa Maswa na ambaye alishindwa katika kura za maoni John Shibuda amekuwa akiilaumu CCM kwamba imejaa rushwa, Makamba alihoji kama
Shibuda angeshinda, angesema hivyo. "Angeshinda angesema hayo? Bwana we! Mbaazi ikikosa maua
husingizia jua, na yeye mwenyewe katika kura za maoni amefanya makubwa zaidi kuliko wenzake, "alisema Makamba na kuongeza: "Tunamwambia nenda salama, asitupake matope."
Makamba ateta sakata la Bashe
 
Hapa issue sio Riz, ila Mama wa kwanza.

Aliyeshika nafasi ya tatu na kupitishwa na nec ni mshauri wa mama wa kwanza. Hivyo mama alimwambia mzee piga ua lazima jamaa apite

Na Mzee aliridhia?...Kha ingekuwa mimi ningekuja juu kujua nini kiko kati yao nisijekuwa nafanywa Babu jinga
 
Nadhani safari nyingine watasema hata Pape si mtanzania!
Hapo hapatakalika! Sigh!:confused2:
 
Lakini kwa nini tunaumiza vichwa juu ya suala la Bashe? Tunapaswa kurejea jinsi maamuzi na uteuzi umekuwa ukifanywa katika serekali ya JK kwa style ya " technique know who". Huyu Mrundi aliyeteuliwa na JK kwa kusema kuwa Selelii amepoteza mvuto (rejea tanzania daima la jana), ni mfanyakazi katika ofisi ya WAMA chini ya Mke wa JK. It is simple pia kuwa, ukaribu huo umemuweka karibu na JK na Ridhiwani. JK kamteua kwa kuwa ni swahiba wa mwane na kwa kuwa mkewe alishampigia ndogondogo.

Lakini pia cha kuijuliza, kwa nini huyu Dr Mrundi hakufanya intern yake tulipomaliza shule? yeye ni Dr (kwa kumaliza course work) na sio kwa kufaya practice. Therefore tunaweza kuona kuwa KUWA WAMA kumemsaidia kumuwekea kivuli ili madhambi yasigundulike. Namshauri arudi kwake Burundi, they might need him!
 
acheni ubaguzi nyie.....hao WA-ASIA mnaowasema nyie ndo mlowakumbatia....mmewapa madaraka wenyewe. suala la uraia si la rangi, ni mkataba wa kisheria baina ya mtu na katiba ya nchi. wa-ASIA waliingia nchi hii kabla hata ya Mjerumani kuweka mipaka ya Tanganyika...Mwingereza akaja, akawapa uraia wake uliojulikana kama 'British Protected People', baada ya Mzee Mchonga kupewa nchi akawakubali kuwa na wao ni raia wa Tanganyika, vivyo hivyo mpka Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nayo iliwakubali. suala la Rostam kuhusishwa na Ufisadi ni suala la mtu mmoja isichukuliwe kuwa SAMAKI MMOJA AKIOZA WOTE.....SOMENI SHERIA ZA URAIA KWANZA ndio muanze kuleta URANGIRANGI (RACISM)...
 
mtanzania sio lazima uwe mweusi kama mimi.....na obama sio mmarekani imekuaje amekuwa rais??????you guys are bullshiters!shame on u!kama Nyerere alivyosema.....KABURU SIO LAZIMA AWE MZUNGU,HATA HAPA TANZANIA KUNA MAKABURU WEUSI WENGI TU!......By pb
 
Back
Top Bottom