Sasa unaweza kumpa mnyama jina lako kwa Tsh Milioni 5

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) imesema gharama za kuasili wanyama ni TZS milioni 1 kila mwaka na kumpa mnyama jina lako TZS milioni 5.

----
Baada ya wanyama kupewa majina ya watu maarufu wa nje ya nchi, Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalum wa kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh5 milioni.

Utaratibu huo nakuja baada ya baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Junior, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 24, 2023 na Kamishina wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.

“Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.

Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.

Aelezea asili ya Bob Junior

Kuhusu simba aliyepewa jina la Bob Juniour, Kamishna Mwakilema amesema jina hilo alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo wakamlinganisha na Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta zake nyingi, ukubwa na kivutio kwa watalii.

“Bahati mbaya jina hilo halikutambulika hadi alipokuja kufa akaanza kuvuma kuwa Bob Junior amekufa,”amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hatua inayofuata watasema anayetaka kufunga ndoa na Mnyama ni shilingi milioni 32,470,681/-
 
Watu wanapokuwa na excess money kinachobaki ni status kwahio chochote kile uki-kibrand kwamba kina bei sana watu watatoa mfano ukisema simba mmoja kumpa jina na bilioni Hamsini alafu Diamond ukampa Hongo akajifanya kanunua usishangae Harmonize kesho akanunua na vijana wote kitaa wakanunua watoto wa huyo Simba kama bei itakuwa laki laki.....

Hii yote ni power of marketing na watu wa marketing wanacheza na na akili za watu hususan kizazi hiki materialistic...
 
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) imesema gharama za kuasili wanyama ni TZS milioni 1 kila mwaka na kumpa mnyama jina lako TZS milioni 5.

----
Baada ya wanyama kupewa majina ya watu maarufu wa nje ya nchi, Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalum wa kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh5 milioni.

Utaratibu huo nakuja baada ya baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Junior, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Julai 24, 2023 na Kamishina wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.

“Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.

Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.

Aelezea asili ya Bob Junior

Kuhusu simba aliyepewa jina la Bob Juniour, Kamishna Mwakilema amesema jina hilo alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo wakamlinganisha na Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta zake nyingi, ukubwa na kivutio kwa watalii.

“Bahati mbaya jina hilo halikutambulika hadi alipokuja kufa akaanza kuvuma kuwa Bob Junior amekufa,”amesema.

Chanzo: Mwananchi
Mwisho wa siku utasikia hata majina yetu tuyatumiayo tunatakiwa tuyalipie
 
Back
Top Bottom