Sasa tunakwenda kushuhudia tofauti ya UKAWA kushika dola na CCM kurudi madarakani

Hapo umeeeleweka vizuri
Acha kupotosha, hadi sasa hii ni kazi ya Magufuli tuliyemwamini na siyo CCM. Kwa Taarifa yako hadi January ndiyo CCM wataingia kama mawaziri na watakuta Action Plan kwa makatibu wakuu. Mmezoea kutuharibia nchi kwa sifa za kijinga na kupiga deal. Mbaki na NEC/Kamati kuu yenu pembeni tujenge nchi, kama chama hata kipya kitaanzishwa
 
Tutakachoshuhudia katika awamu hii ni kuibuliwa kwa madudu makubwa huku wakuu wa mashirika ya umma wakiwajibishwa kama mbuzi wa kafara lakini vigogo walioko kwenye system wakipeta au wakikamatwa wale dagaa tu.

Inawezekana kabisa,hawa wakuu wa mashirika haya ya umma walikuwa wanafanya kazi tu ya kulinda maslahi ya wakubwa na huenda wao wakawajibishwa huku vigogo hawa wakiachwa jambo ambalo serikali ya UKAWA isingelifanya.

Kumekuwepo na madai/tuhuma za vigogo kutumia majina ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuendesha biashara zao kitu ambacho sidhani kama serikali ya Magufuli itathubutu kukufanyia uchunguzi-UKAWA wangethubutu.

Hivi biashara ya madawa ya kulevya, magogo,meno ya tembo na hata hii ya kupitisha makontena kiholela bandarini haina baraka za wakubwa?Magufuli ataweza kuwawajibishi vigogo hawa pindi wakibainika?

Fukuafukua hii ya serikali ya Magufuli huenda ikawa "counter-productive" kwa CCM na serikali yake na jambo hili likiwa handled vibaya, huenda likafanya watu waichukie zaidi CCM badala ya kuipenda kama wengi wanavyodhani.

Anachokifanya hivi sasa Magufuli ni sawa kuwadhihirishia watanzani,tena kwa ushahidi, ni kwanini CCM haikupaswa kuchaguliwa kurudi madarakani na akishindwa kuwawajibisha vigogo watakaobainika atakuwa anajimaliza mwenyewe.

Hivi sasa UKAWA wamerahisishiwa kazi kwani karibu kila kitu kinaibuliwa na serikali yenyewe na wao kama wapinzani watakuwa na kazi ya kushinikiza hatua zichukuliwe jambo ambalo nina mashaka kama litatekelezwa kwa uaminifu hata kama itaundwa hiyo Mahakama ya Mafisadi.

Bungeni ndio kutakwenda kuchafuka na hapa ndio mtihani wa Magufuli na serikali yake kuchukua hatua utakuwa mgumu zaidi maana ndani ya bunge huenda yakaibuliwa mengi ambayo hatukuyatarajia.

Kwa mfano, yanayosemwa na watu na kuandikwa mitandaoni kuhusu kampuni ya Home Shopping Center huenda yakaibukia Bungeni na wabunge wa UKAWA wakadai uchunguzi ufanyike kuhusu kampuni hii.

Kufichua tuhuma na watuhumiwa ni jambo moja, na kushughulikia tuhuma na watuhumiwa ni jambo lingine.

Kwenye orodha hakuna wafadhili?

Tusubiri.

Mkuu mbona una papara?huyo ndo JPM the man of his words-anatenda anayosema na kuahidi,la msingi ni kumuombea afya njema na kuweka politics pembeni na kumpa support kwa umoja wetu kama watanzania.wale waliokuwa wanasema "mwenye ushahidi aende mahakamani" sidhani kama utawasikia wakirudia ngonjera zao hizo,kwa sasa WATU WAKO KAZINI.
 
Subiri uone ndio mtajua kama Magufuli anairudisha CCM kwenye ramani au ndio anaifuta.

Hayo maneno ya subiri utaona nimeaanza kuyasikia siku nyingi mpaka yameshakinahi, kwa maana nilianza kuyasikia 2000 ikaja 2010 mpaka 2015 sasa bado tu tunaambiwa subiri mtaona kuna lipi jipya mtalifanya ambalo mmeshindwa kulifanya miaka 20 iliyopita?

WatanZania wanataka maendeleo na hawako kwenye mambo ya siasa
!
Raisi Magufuli atahukumiwa hapo kama watu wakiona huduma za Afya zimeboreka hali ambayo inaelekea kutokea, Maji masafi yanapatikana, Umeme wa uhakika upo, Chakula cha uhakika kipo, Wanafunzi wanasoma baada ya mazingira kuboreshwa ninakuhakikishia Raisi Magufuli hatakuwa na shida yoyote kwenye kukubalika na WatanZania hilo kaa ukijua, na hayo yote yako ndani ya uwezo wa Raisi Magufuli na atayafanya!
 
Mkuu mbona una papara?huyo ndo JPM the man of his words-anatenda anayosema na kuahidi,la msingi ni kumuombea afya njema na kuweka politics pembeni na kumpa support kwa umoja wetu kama watanzania.wale waliokuwa wanasema "mwenye ushahidi aende mahakamani" sidhani kama utawasikia wakirudia ngonjera zao hizo,kwa sasa WATU WAKO KAZINI.

Hawa watu ndio misukule ya kina MBOWE kilajema kupinga hawana nafasi tena
 
Mkuu mbona una papara?huyo ndo JPM the man of his words-anatenda anayosema na kuahidi,la msingi ni kumuombea afya njema na kuweka politics pembeni na kumpa support kwa umoja wetu kama watanzania.wale waliokuwa wanasema "mwenye ushahidi aende mahakamani" sidhani kama utawasikia wakirudia ngonjera zao hizo,kwa sasa WATU WAKO KAZINI.

Akiweza tutamshukuru.
 
Makala yako imetukuka umefikiri kwa kina sana. Wa kuisoma namba muda si muda wataeleweka
 
Bahati mbaya mkuu waraka wako umejaa hisia,tetesi za mitaani na habari za kudhaniadhania kiasi kwamba hata msomaji anaona hauna mantiki!
 
Hivi kuna nembo ya ufisadi nchi hii Kuzidi lowassa?
Hapa ukitaja ufisadi akili za watz zote zinapata picha ya lowassa kichwani,
Halafu eti lowassa angesimamia kukamatwa kwa mafisadi!!!??? Usichekeshe wewe, sema angeshinda basi mpaka sasa mafisadi wangeshakuwa wamegawana nchi nzima vipande vipande,

Mleta mada anatumia formula ya kua kwa vile Lowassa ni Mwizi basi ingekua rahisi kujua wezi wenzake walipo na kuwakamata! Mleta mada hakujua kama Magufuli hana mchezo na wezi wote
 
Mleta mada anatumia formula ya kua kwa vile Lowassa ni Mwizi basi ingekua rahisi kujua wezi wenzake walipo na kuwakamata! Mleta mada hakujua kama Magufuli hana mchezo na wezi wote
Ngoja kubenea atapowataja watuhumiwa wa Escrow Bungeni ndio utanielewa vizuri na utaelewa ni kwanini Magufuli alisema tumuombe na ndio itakuwa fursa nzuri ya kupima ujasiri wa Magufuli.
 
Mleta mada, wataje hao vigogo au peleka taarifa zao kwa raisi au pm uone kama hawajashughulikiwa. Kama unawafahamu halafu unalalamika tu haikusaidii wala haitusaidii Watanzania. Pia tuwe na shukrani awamu hii japo ni mwanzo bado lakini wamethubutu, hata hao unaowaita vigogo lazima watetemeke. MUNGU amlinde raisi wetu.
 
Salalei Stupid, mbona unataka chai inipalie? CCM haijarudi madarakani, kilichotokea ni kwamba CCM na UKAWA wote wamepigwa chini na sasa nchi inaongozwa na Rais.

Ukitaka kujua CCM haipo madarakani, angalia jinsi makada wake wanavyopata hasara na Hawana cha kufanya sbb serikali sio yao. Kuna mtu atakuwa alishaagiza T-shirt za kuvaa watoto wa halaiki kwenye gwaride, sasa subiri utaziona zinauzwa mitaani kwa bei ya hasara.

Asante sana. Watu wanaleta uchama na ukada. Sisi tunajua tuna raisi na serikali.
 
Tutakachoshuhudia katika awamu hii ni kuibuliwa kwa madudu makubwa huku wakuu wa mashirika ya umma wakiwajibishwa kama mbuzi wa kafara lakini vigogo walioko kwenye system wakipeta au wakikamatwa wale dagaa tu.

Inawezekana kabisa,hawa wakuu wa mashirika haya ya umma walikuwa wanafanya kazi tu ya kulinda maslahi ya wakubwa na huenda wao wakawajibishwa huku vigogo hawa wakiachwa jambo ambalo serikali ya UKAWA isingelifanya.

Kumekuwepo na madai/tuhuma za vigogo kutumia majina ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuendesha biashara zao kitu ambacho sidhani kama serikali ya Magufuli itathubutu kukufanyia uchunguzi-UKAWA wangethubutu.

...........................................................................................................................................
..........................................

Kwa mfano, yanayosemwa na watu na kuandikwa mitandaoni kuhusu kampuni ya Home Shopping Center huenda yakaibukia Bungeni na wabunge wa UKAWA wakadai uchunguzi ufanyike kuhusu kampuni hii.

Kufichua tuhuma na watuhumiwa ni jambo moja, na kushughulikia tuhuma na watuhumiwa ni jambo lingine.

Kwenye orodha hakuna wafadhili?

Tusubiri.

Serikali ya UKAWA isingezunguka mbuyu. Mfano sakata la TRA, tungemkamata waziri na katibu husika pamoja na huyo kamishina wa TRA. Tungewadandia woote walionufaika na misamaha ya kodi pia.

Juu ya yote tungemwajibisha pia IGP kwa kushindwa kuzuia uharifu huu.
 
Those who think it can't be done,shouldn't interrupt the one doing it.Hata huyo Rished Bade ni kigogo or who is kigogo to you?
 
A world class stupid article, eti serikali ya ukawa, wtf! Unataka kuniambia lowassa angekuwa na balls hata za kusimamisha watu kazi wakati yeye ndo angekuwa LE MAFIA namba moja?? Ni mipango ya Mungu ukawa hawatashika dola!
Zitto Kabwe has a better chance kuwa rais kuliko chadema kutoa rais siku zijazo! Eti serikali ya ukawa, itabaki kusema kichwani hivyo hivyo serikali ya ukawa isingefanya, haitatokea miaka 40.

Mh!! mmeshaanza kuchemka! Hapo bado madudu yenu mengi hayajaanikwa hadharani. Ingefaa mtulie tu muangalie upepo unavyovuma. Ni ujinga kututaka tusilinganishe yanayofanyika leo na kama upande wa pili wa mlengo wa siasa zetu ungeshinda ingekuwaje. Ujinga huo wanao wajinga tu!
 
Back
Top Bottom