Sasa ni Dhahiri: Bandari yakumbwa na Uhaba wa Mizigo

Endelea kulia lia tuu maana zama zenu za kuinyonya hii nchi zimeshakwisha. Jipange kivingine bro, kulalama lalama huku jamii forum hakutokusaidia, Utaumbuka mjini mzazi. Kaanzishe mashamba ya matikiti kimbiji, yanalipa sana pia.
Unajiita 'seal team six' afu unakuwa na upeo wa ajabu namna hii!!
 
Nani amekwambia tunahitaji mizigo mingi isiyo na tija kwa taifa?

bagamoyo.png
 
Nisaidieni kufahamu...
Kwani sababu ya kupungua mizigo ni nini?

Kama ni kodi, imepanda kwa asilimia ngapi kulinganisha na awamu iliyopita?

Msaada plz
 
Sababu kubwa ni uchumi wa China kupungua, kwakua Wazungu wameuathiri sana mpaka huku kwetu, na yale magari mengi ya kijapani yameingia chumvi kwaiyo wafanyabishara wamepungua kununua magari kutoka Japan.
 
Kitu cha Muhimu ni kuwa mapato yameongezeka...
Hatuhitaji mizigo mingi isiyokuwa na tija kwa taifa
Tija kwa taifa aiamuliwi kwa maneno ya kisiasa. Mapato yanaongezeka for how long? Impact ya ajira za waliokuwa wakiwajibika huko? Au hizo kodi utawagawia wagawane ili watunze familia zao?

Mimi sipingi ukusanyaji kodi...tatizo approach. Jambo lolote likifanywa kwa mwendokasi huishia kutafutiwa excuses ili mradi kujustify crisis.
 
poleni sana wale vijana na wasichana mliozoea kunywa heinken, windhoek na savanah, sasa hamieni kwenye mwanmke nyonga (safari lager ndogo) au ukawa/lowasa (pilisner lager)
 
Bora kuwa na mizigo michache inayoingia kihalali na kulipiwa kodi kuliko kuwa na mizigo mingi ya magendo na ambayo haina tija kwa taifa zaidi ya kunufaisha wachache wezi
 
Mh! kuishi kwingi ni kuhatarisha afya tu, sasa hali hii ni kutiana msongo wa mawazo na kufa gafla. Sasa kuna haja ya kuendelea na ujenzi wa ile ya bagamoyo kweli?
Bagamoyo Ni Bandari Maalum Ya Kufuga Konokono Tu
 
Habari ya kusikitisha na kuhudhunisha kwa siku ya leo. Hii ina maana ajira kibao zimeota mbawa, Madereva wa shunting toka bandari mpaka ICDs,makarani wa ICDs,wafanyakazi wa kampuni za uagent(clearing and fowarding),usisahau watu wa plate namba,mawakala wa kampuni za meli,madereva wasafirishaji (IT),mama ntilie,madereva mitaani n,k . Jamani kuweni waungwana tusifurahie shida na machungu ya wengine kwa kujipa faraja kwamba sisi tunapokea mshahara au tuna hela hatuathiriki,ipo siku huu mzunguko utakufikia tu! direct au indirect
 
Hizo Icd zilikuwa vichaka vya kukwepa kodi tu
Ni heri tupate container 100,lakini kodi yote tuipate,kuliko kungiza container 3000 hazilipiwi ushuru.
Wakwepa kodi,wanajipanga ku adjust cashflow,baadae mizigo itajaa tu hakuna jinsi
 
Hauko sawa kwatika hili. Ukweli ni kwamba kulikuwa na deal pale bandarini kuwa hata kama TPA yard ziko tupu jamaa walikuwa wanapeleka mzigo kwenye hizo ICD kwa maslahi yao binafsi ( Chanzo Jamhuri). alipokua DG mpaya Jamhuri wakalipua akafuatilia na kutoa maelekezo kuwa hakuna mzigo kwenda ICD mpaka capcity ya TPA imetumika hadi kwisha ndipo wapeleke ICDs. Sasa hapo ndio inapokuwa kazi kwa sababu jamaa hawapati biashars na wengine ndio wameanza anza tu biashara baada yakuona wenzao wanapiga. wameinvest big tyime biashara hamana pengine wapo waliokopa na benki kila leo wanapiga hodi!

Kitu cha Muhimu ni kuwa mapato yameongezeka...
Hatuhitaji mizigo mingi isiyokuwa na tija kwa taifa
 
Kitu cha Muhimu ni kuwa mapato yameongezeka...
Hatuhitaji mizigo mingi isiyokuwa na tija kwa taifa

Hakuna ongezeko la pato bali ni makusanyo ya arias. Huwezi kuadhiri ajira ukapunguza wigo wa kodi na kazi kwa watu wako then ukanadi kutetea wananchi wako maskini ambao watoto wao ndiyo wahanga wa hayo.
 
Tutawatoza VAT tu, asiyetaka kulipa VAT asije. Afadhali kupata VAT kidgogo kuliko mizigo mingi. Na hata nyie watalii mtalipa VAT tu, asiyetaka kulipa VAT asije. Heri kuwa na watalii kidogo wanaolipa VAT kuliko watalii wengi bila VAT. Sie uchumi tunaujua bwana, tumesoma sana sayansi. Msitubabaishe.
 
Hivi mwezi uliopita mmekusanya shiling ngapi vile??
Kama uko hapa kutukejeli, endelea na kejeli zako. Ssi tunasonga mbele.

Ukiangalia hizo icd's ndo baadhi zilikamatwa kwa kutokulipa kodi stahiki. Hivyo as longer as the port can receive and distribute the cargo efficiently, without the help of those exploiters, its fine to us
 
Habari ya kusikitisha na kuhudhunisha kwa siku ya leo. Hii ina maana ajira kibao zimeota mbawa, Madereva wa shunting toka bandari mpaka ICDs,makarani wa ICDs,wafanyakazi wa kampuni za uagent(clearing and fowarding),usisahau watu wa plate namba,mawakala wa kampuni za meli,madereva wasafirishaji (IT),mama ntilie,madereva mitaani n,k . Jamani kuweni waungwana tusifurahie shida na machungu ya wengine kwa kujipa faraja kwamba sisi tunapokea mshahara au tuna hela hatuathiriki,ipo siku huu mzunguko utakufikia tu! direct au indirect
Hao si ndo walikuwa majizi wa accessories kwenye magali? Wacha waisome namba
 
Kitu cha Muhimu ni kuwa mapato yameongezeka...
Hatuhitaji mizigo mingi isiyokuwa na tija kwa taifa
Yameongezeka baada ya kupungua mizigo?? Hahahahaha hii kali sana kama ni hivyo basi tuzifunge kabisa ICDs na Bandari ili mapato yaongezeke zaidi na zaidi
 
Kama uko hapa kutukejeli, endelea na kejeli zako. Ssi tunasonga mbele.

Ukiangalia hizo icd's ndo baadhi zilikamatwa kwa kutokulipa kodi stahiki. Hivyo as longer as the port can receive and distribute the cargo efficiently, without the help of those exploiters, its fine to us
Nani aliwaweka hao unaowaita Exploiters??
 
Back
Top Bottom