Sasa naamini kabisa CUF ni CCM 'B'

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Kutokana na jitihada za kupunguza nguvu za Chadema Bungeni ili kuikweza CUF kuwa na sauti kubwa katika upinzani -- sauti ambayo inaanza kupotea kama ilivyojionyesha katika uchaguzi ulopita, sasa naamini kabisa kwamba CUF ni CCM B -- na ni maswahiba wakubwa wa chama tawala -- CCM.

Na pia inaonysha jinsi CCM inavyoiogopa Chadema hasa katika kutoyumba kwao katika kusimamia masilahi ya wananchi.

Naona kwa hili hakuna ubishi. Asanta Spika makinda kwa kutudhihishia hilo -- lakini angalia usiwe unawafanyia wananchi maandalizi ya yaliyotokea Tuniusia au Misri, kwani nchi hii kama tulivyoiona hivi karibuni, Tanzania siyo tofauti (unique) na hivyo hayo yanaweza kabisa kutokea. Tatizo ni time muafaka na wewe Makinda utahesabiwa katika historia kuwa ni mmojawapo aliyechangia vurugu.

Ukae ukijua hilo kutokana na maamuzi yoyote utakayokuwa unafanya katika Bunge hili katika kulinda masilahi ya mafisadi wachache, na siyo ya wananchi wengi walio masikini.

Nakuomba usikubali kuambukizwa ule ugonjwa wa kuona mwisho wa pua tu, jaribu kuona mbali sana.
 
Hii imetulia -- ona nimekugongea. Hakuna tena uthibitisho zaidi ya hatua hiyo ya Spika kwamba CUF ni CCM B. mimi nadhani ingekuwa ni kinyume chake, kwamba Chadema -- katika suala lolote lile kuhusu shughuli za Bunge -- ndiyo wangeomba kanuni zibadilishwe ili kukipa nafuu chama hicho, Makinda angelitupilia mbali ombi hilo.

Kweli Chadema ni tishiuo kwa CCM!!!! na uzuri ni kwamba CCM wenyewe wanaionyesha hofu hiyo!!!
 
umechelewa kugundua tu mkuu,hilo tatizo mbona lipo siku nyingi sana !!
 
View attachment 22409 CHADEMA.gif

Peoples Power, wanasema sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na Nguvu ya waengi pia ni nguvu ya Mungu. Tunaamini nguvu ya CHADEMA ni nguvu ya Mungu. Makamanda msife moyo
 
Mi naona kama kuwaita CUF CCM B sio sahihi kwangu, CUF ni CCM uchwara...
 
Jamani tumeona. Twende kwa wananchi tuwaeleze watuelewe ili tusipate shida 2015. Tukizungumza humu JF tu hakuna cha zaidi ni kuzungusha habari inayojulikana toka zamani. CUF na CCM walionekana wakati wa uchaguzi wa Spika na bunge la SADC. Hakuna maswali tena!!! Tushirikiane kuhakikisha kuwa kila mtu anapata watu laki moja walioelezwa na kuelewa bila shaka njama za CCM na CUF za kuipunguzia nguvu CHADEMA.
 
Hii wengine tuliisha iona tokea zamani! Kilichobakia ni CUF kubadili bendera yao kuweka jembe na nyundo! CUF ni historia
 
hivi kuna haja ya kuishi kwenye nchi kama hii? si bora tufe. mimi naomba nchi iuzwe tugawane hiyo ela.
 
Mheshimiwa Tundu Lisu amewaambia kabisa CUF na CCM kwamba sheria zinaruhusu polygamy and not bigamy yaani ndoa ya wake wengi nasiyo ya wamewawili kwani wameshafunga ndoa na ccm Zanzibar sasa bara hawatakiwi
 
Hivi seif bado mpinzani wa ccm au ndiyo yale mambo yetu ya atafutae hachoki akichoka ujue keshapata?
 
Ndugu zangu mimi nimehudhuria kikao cha leo cha Bunge. Nilichokiona na kushuhudia ni maafa kwa democrasia ya nchi hii. CUF, NCCR, UDP, CCM na TLP wanapoungana dhidi ya Chadema ujue Chadema is becoming a threat to their personal gains and their political survial . Chadema are truly fighting for the welfare of the public but the rest of the parties are there to safeguard their personal interest. However, I am prety sure Chadema will emerge victors.

When you start losing the fear of death life begins
 
Ndugu zangu mimi nimehudhuria kikao cha leo cha Bunge. Nilichokiona na kushuhudia ni maafa kwa democrasia ya nchi hii. CUF, NCCR, UDP, CCM na TLP wanapoungana dhidi ya Chadema ujue Chadema is becoming a threat to their personal gains and their political survial . Chadema are truly fighting for the welfare of the public but the rest of the parties are there to safeguard their national interest. However, I prety sure Chadema will emerge victors.

When you start losing the fear of death life begins

Another wishifull thinking!

Eti chadema pekee ndio wapinzani...wa kweli

Endeleeni kujifaraji maana ndio mwisho wa uwezo wenu wa kufikiri..

CUF, NCCR, TLP ni wanasiasa hawawezi kunyamazishwa na chadema lazima watafute uhalali wa kuheshimiwa..
 
Another wishifull thinking!

Eti chadema pekee ndio wapinzani...wa kweli

Endeleeni kujifaraji maana ndio mwisho wa uwezo wenu wa kufikiri..

CUF, NCCR, TLP ni wanasiasa hawawezi kunyamazishwa na chadema lazima watafute uhalali wa kuheshimiwa..
Hivi huwa wanasemaje tena? Adui wa adui yako ni rafiki yako? Au rafiki wa adui yako in adui yako? Hii misemo huwa haina maana inakuja kwa wanasiasa wa Tanzania? Au haina maana kiujumla.
 
Back
Top Bottom