Sanduku la Agano yawezekana limefichwa na makundi ya siri kama Priory of Sion?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,373
Waasalam

Anaandika,
DaVinci XV,

CCF04BD2-F2F5-416D-8E95-2ABD96365EDA.jpeg


Naam
Inajulikana na kuelezwa dhahiri katika Imaani na maandiko tofauti tofauti ya kwamba miongoni mwa vitu vikubwa na vitakatifu basi huwezi kuacha kulitaja sanduku la Agano , au Sanduku la Ushuhuda kama wengine wanavyoliita.

Utakatifu wa Sanduku hili inaelezwa kuwa Makuhani walilazimika kulibeba kwa kulishika katika sehemu maalumu (-Fimbo) ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kubebea sanduku na haikupaswa kuligusa sanduku lenyewe, na sababu ni kwamba utukufu wa Mungu na uwepo wake hauwezi kuguswa na mwanadamu.
Maana sanduku lenyewe lilikuwa ni utambulisho wa uwepo wa M/mungu duniani tazama andiko la (KUTOKA 25:22)

Nadhani wengi baina yetu si wageni wa hili na wanatambua mengi kuhusu sanduku hili takatifu, sitohitaji kuingia ndani zaidi kuelezea sanduku hili , bali nitamega kidogo na kujikita zaidi katika msingi wa maada.

VILIVYOMO NDANI YA SANDUKU

6F8F8AA6-FF91-4D72-B419-B6137407740A.jpeg


Sanduku hili takatifu lilihifadhiwa vitu tofauti tofauti vitakatifu ikiwemo

1- Mawe mawili matakatifu ambayo yaliandikwa Amri kumi za Mungu katika zama za Musa

2- Fimbo ya Harouni ambayo ina muujiza wake pale ilipochipua Maua pale MwenyeziMungu alipowaonyesha waisraeli , Kuhani aliyemchagua ambaye ni Harouni (nadhani wengi wetu wanauelewa mkasa huu)

3- Na mtungi ambao ulikuwa na Chakula Manna ,
Manna ni chakula maalumu ambacho kiliweka muunganiko kati ya M/Mungu na wanaisraeli , Na katika Imani ya dini ya kiislamu inaeleza dhahiri wakati Waisrael walipoihama misri kuelekea Nchini kwao basi M/mungu Aliwarudhuku chakula kutoka katika Pepo yake ambacho ni Manna na Salwah.

CDB621BD-72D3-4322-8E32-8209E71F2E81.jpeg


Na vyote hivyo katika vitu vilivyomo kwenye Sanduku vilikuwa na Utambulisho au maana zake , Ambazo ni Sheria, ukuhani( ukuu), na utoaji wa M/mungu.
Na kama wanatheolojia wengi walivyoeleza.,
Nadhani pia umeona utakatifu wa vitu vilivyohifadhiwa katika Sanduku la M/mungu.

UPORAJI NA BAADHI YA MAENEO DHAHANIA JUU YA LILIPOFICHWA SANDUKU LA AGANO

448BA8DF-0B55-426F-B0D9-5D33AEEBD420.jpeg


Sanduku hili lilitengenezwa kwa mbao kama biblia inavyotanabahisha vyema , kisha ikafunikwa na dhahabu safi, na sanduku hili la Agano mda wote lilihifadhiwa katika hekalu

Na mara kadhaa historia imeonyesha tawala tofauti tofauti kulipora na kuondoka nalo
Mfano wafilisti walifanikiwa kuliteka na kulipeleka kwa Mungu wao lakini Athari zake lilipelekea kuzuka kwa ugonjwa wa Tauni katika jamii yao.

Sanduku hili limeonyeshwa simulizi nyingi zinazohusu kupotea kwake na kupatikana.

Lakini mara ya mwisho sanduku hilo kuonekana ni wakati wa uvamizi wa wababyloni chini ya mfalme Nebuchadnezzer kiasi cha miaka 500 (B.C)
hivi kabla hajazaliwa masihi Yesu mtoto wa maryam walipovamia Israel na kulivunja hekalu la Suleiman na huko ndio haswa kulihifadhiwa sanduku hili la Agano.


40A4A59B-F080-48BB-AF60-52200FFDE9C2.jpeg

Nebuchadnezzer

Na vivyo hivyo Hadithi nyingi zikielezea namna tofauti tofauti ambazo namna hizo hazina ithibati ya lilipofichwa sanduku hilo la Agano
Wengine husema sanduku lilifichwa Na
Mfalme Josiah baada ya kupokea Utabiri wa uvamizi wa wababyloni

Wasomi wengine hudai sanduku hili limehifadhiwa huko Makka chini ya Al-Kaaba, na haliwezi patika kwa maana waislam hawawezi kuruhusu sehemu hiyo takatifu kuchimbuliwa ili tu kutafuta Sanduku.

Na wasomi wengine wanataja sehemu tofauti tofauti ikiwepo ethiopia na Roma huko Italy.

Nadhani kwa kiasi tumejaribu kumega muktadha wa kihistoria juu ya Sanduku la Agano, ambao wengi wetu tunautambua.

4B62F905-A0A7-4851-AD72-73A3594EB21D.jpeg


JE, INAWEZEKANA SANDUKU LA AGANO LIMEFICHWA NA JAMII ZA SIRI (Kama PRIORY OF SION)

Priory of sion au Prieure de sion (au makundi mengine ya siri kama Illuminant), ni nini??? Hiyo ni mada nyingine inayohitaji nyuzi yake


0BC37797-613E-4901-B6E2-1BDD3B32B670.jpeg


Unakumbuka kuhusu Last supper ??, mlo wa mwisho wa Bwana Yesu na wanafunzi wake
Unaikumbuka vyema ile picha iliyochorwa na mchoraji na mwanasayansi hodari Leornardo Da Vinci aliezaliwa huko Vinci Italy???

Basi kama ujuavyo katika karamu yoyote , au hafla vitumikavyo ni vyombo.
Ushawahi kusikia kuhusu Holy grail kile kikombe alichotumia bwana yesu kunywea kinywaji katika mlo ule wa mwisho na wanafunzi wake.???
51CB033E-A00C-4878-9B26-4A027882798C.jpeg

Kikombe ambacho katika nyaraka tofauti tofauti zilizofichwa kimeelezwa kuwa na maajabu yaso kifani kwa yoyote aliyekitumia.

Kuna ambao , walitumia kunywa kinywaji kwa kutumia holy grail na kufanikwa kupona maradhi sugu na wasiumwe tena, kupata nguvu sisizo kifani, Kufa na kufufuka, kusafiri moja kutoka sehemu mmoja au nyingine ya umbali wa kilometa tele kwa mda mchache sana usio wa kawaida, kuwa na ufahamu mpana sana, mamlaka , na Amani ya moyo
Kuna waliotumia wakawa na ufahamu usio kifani na ujuzi wa kuvumbua mambo mengi ambayo kwa wengine si kawaida kama wanasayansi mashuhuri akiwemo Leornado Da Vinci mwenyewe ambaye baadhi ya maandiko yake ya siri yamefichua haya
Lakini ikumbukwe huyu Leornardo DaVinci ni member mkubwa sana Wa kundi la Priory of sion ambalo limehusishwa na kuwa na viongozi wengi wa kidini kama Mapapa na hata wanasayansi wakubwa na watu maarufu kama Sir Isaac Newtons , Boticelli ,na wengineo.
Na ndio kusema kwamba , wanasayansi wengi (sio wote) walikuwa katika makundi makubwa ya Siri, kutokana na uwezo uliopatikana kutoka kwao.

712F3F4A-2EB5-43AD-AFA5-19E0518EC8FD.jpeg

Sir Isaac

Cha Ajabu zaidi usichokijua ni baadhi ya nyaraka hizo zinadai kwamba Kutokana na neema na maajabu ya holy grail kikombe hiki kimehifadhiwa kusikojulikana na mhusika mkuu ni hili kundi la priory of sion kama baadhi ya nyaraka za siri za mwamba Leornardo da Vinci zinavyodai, na si tu holy grail bali vitu vingi vitakatifu vimehifadhiwa na kufichwa kusikojulikana na makundi haya siri ili viendelee kuwanufaisha na kuwapa faida.

N.B Lakini nyaraka hizi hazina ushahidi wa kutosha kuzipa nguvu ili kiwe kitu cha kuaminika
Nani anajuaye????


(Tuachane na hapo Hii mada Holy grail panapo majaliawa tutaitafutia nyuzi yake)

Wakati mmoja nilipata kupitia documentary moja ambayo muandishi wake anadai yeye ni katika member wa makundi kati ya kundi mojawapo la siri na kubwa hapa duniani.

Moja kati ya vipengele vya documdntary hiyo vinaelezea.

Dunia yetu imeaminishwa ya kwamba sanduku takatifu la Agano limepotea na yakitajwa maeneo tofauti tofauti yakwamba huenda limehifadhiwa huko

Documentary inadai makundi haya makubwa (priory of sion, Illuminati ) , au jumuiya nyingine ya siri yoyote ya siri Huenda wana uhusiano na kupotea kwa sanduku la agano.

EF4A59ED-F96E-41E7-A677-AB92A9352131.jpeg

Wasomi wale wanaijua Biblia vizuri sana, kuliko kawaida, ni miongoni mwa kitabu chao cha mwongozo.
Wanaelewa maneno ya siri na yenye faida juu ya kutawala .
Wameweza kuwafanya watu kuwa mpumbavu na wajinga juu ya maandiko na mafumbo tofauti tofauti ya dini.
Wana uelewa mkubwa sana juu ya Faida za ulimwengu wa kiroho unaopatikana kutokana na sanduku lile, na vitu vingine vitakatifu vilivyofichwa hivyo wakatengeneza nadharia nyingi sana kuaminisha ulimwengu juu ya sanduku ili kuwapoteza watu na wao kuendelea kufaidika na vilivyomo.

Sanduku halikufichwa huko Ethiopia kwa malikia wa Sheeba, wala halikufichwa kwa waarabu pale Makka wala halikufichwa kwa Wayahudi pale Israel, wala halipo kwa waitaliano pale Rome.

8FFAB4EF-8675-4A84-B809-65DFFB7F88F9.jpeg


Akili , Maarifa na Nguvu za utawala za makundi haya zinatokana na vitu kama hivyo vitakatifu ambavyo vimehifadhiwa na kutumika katika ulimwengu wa kiroho zaidi kama vilivyohifadhiwa vitu vingine
(Holy grail, Kinubi cha mfalme Daudi na hata hilo sanduku la Agano na vinginevyo)

Vitu kama hivyo (sanduku la Agano) vinawapa nguvu.
hawaogopi kifo, inawafanya wawe na nguvu Inawapa udhibiti wa akili na mwili wao na wanadamu wengine.
Inawapa mamlaka ya kutawala dunia na nguvu nyingine nyingi
Endapo vitu hivi vitarudi katika mkono sahihi basi hapo hapo ndipo nguvu itarud kama ilivyo kawaida

Na hapa ndipo kiu ya kumsubiri mwana wa Adamu (Issa au Yesu mtoto Wa marym) inapozidi kuwa kubwa ili aje kufichukua mengi msiyoyajua.

Naam nikipata wasaa nitaambatanisha jina la documentary ile

Kipindi fulani wakati najaribu kupata darasa kuhusu
Holy grail jinsi ilivyofichwa na kutumika kunufaisha watu ndipo nikajiuliza yawezekana hata sanduku la Agano ambalo sisi bado hatujui lilipo nalo limehifadhiwa na hawa mabwana wakubwa wa Dunia. Ili waendelee kunufaika na matunda ya faida zake

Wewe unadhani vipi!??

Shuqraani

DaVincii XV
 

Attachments

  • EACCDAAF-7096-4A44-90E7-2F91DBA2BC57.jpeg
    EACCDAAF-7096-4A44-90E7-2F91DBA2BC57.jpeg
    43.9 KB · Views: 42
Sanduku la agano lipo mbinguni, soma ufunuo 11:19

Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake.
Ukianzia 11: 14 au 15 unaweza pata mwanga ni kama andiko lilikuwa linaonesha liberation.
Ufalme wa Mungu utabaaki hata
Milele kutoka kwa wale waovu

Haya ni mafunuo aliyopoakea yohanna Mtoto wa zebedayo pale kisiwa cha Patmo ya mambo yajayo na siyo yaliyopo wakati ule.

Vipi , kama sanduku hili litarudishwa katika hekalu la M/Mungu wa mbinguni (na si kwamba lipo) baada ya liberation hii itakayokuja baada ya utawala usio sahihi kuenguliwa na ufalme wa M/Mungu kutokea baada ya Yohanna kufunuliwa .???
 
Sasa najiuliza iweje Mwanga na Giza vikae pamoja,Kama historia inasema hilo sanduku iliwahi kuibwa na wafilisti na likawaletea shida mpaka wakaamua kulirudisha Je leo huo utukufu uliopo kwenye sanduku umendoka sasa?

Kama haujaondoka basi sidhani kama kuna jamii yeyote ya siri inayofanya mambo ya Giza itafanikiwa kuvitumia vitu hivyo kinyume na kazi za Mungu.

Kuhusu liko wapi sanduku mpaka sasa ni kitendawili ila nilishaona documentary ya BBC wanadai lipo Ethiopia milimami huko kuna dhehebu Fulani lina hekalu na wana askari wao waumini wanavaa mavazi Fulani meupe na wana silaha na wako tayari kufa kulilinda, hawaruhusu mtu yeyote kuingia humo zaidi ya mtu mmoja tu ambaye ndiye hulinda hilo sanduku na akifa tayari kuna mwingine alishaandaliwa kufanya kazi hio,na huyo mtu huwa hatoki humo hekaluni.

Hata mwandishi aliyefika hapo hakuruhusiwa hata kuingia ndani ya uzio wa hekalu maana liko fenced,aliongea akiwa nje tu,lakini walikiri wanalo hilo sanduku la agano ila hawezi kuliona kutokana na masharti yao.
 
Ukianzia 11: 14 au 15 unaweza pata mwanga ni kama andiko lilikuwa linaonesha liberation.
Ufalme wa Mungu utabaaki hata
Milele kutoka kwa wale waovu

Haya ni mafunuo aliyopoakea yohanna Mtoto wa zebedayo pale kisiwa cha Patmo ya mambo yajayo na siyo yaliyopo wakati ule.

Vipi , kama sanduku hili litarudishwa katika hekalu la M/Mungu wa mbinguni (na si kwamba lipo) baada ya liberation hii itakayokuja baada ya utawala usio sahihi kuenguliwa na ufalme wa M/Mungu kutokea baada ya Yohanna kufunuliwa .???
Kuna namna sanduku litapatikana pale Israel kwenye true location linapotakiwa kujengwa hekalu la tatu la mfalme Suleiman. Mpaka wakati huo ni kama vile Mungu ametuficha tusijue lilipo.
 
Sasa najiuliza iweje Mwanga na Giza vikae pamoja,Kama historia inasema hilo sanduku iliwahi kuibwa na wafilisti na likawaletea shida mpaka wakaamua kulirudisha Je leo huo utukufu uliopo kwenye sanduku umendoka sasa?

Kama haujaondoka basi sidhani kama kuna jamii yeyote ya siri inayofanya mambo ya Giza itafanikiwa kuvitumia vitu hivyo kinyume na kazi za Mungu.

Kuhusu liko wapi sanduku mpaka sasa ni kitendawili ila nilishaona documentary ya BBC wanadai lipo Ethiopia milimami huko kuna dhehebu Fulani lina hekalu na wana askari wao waumini wanavaa mavazi Fulani meupe na wana silaha na wako tayari kufa kulilinda, hawaruhusu mtu yeyote kuingia humo zaidi ya mtu mmoja tu ambaye ndiye hulinda hilo sanduku na akifa tayari kuna mwingine alishaandaliwa kufanya kazi hio,na huyo mtu huwa hatoki humo hekaluni.

Hata mwandishi aliyefika hapo hakuruhusiwa hata kuingia ndani ya uzio wa hekalu maana liko fenced,aliongea akiwa nje tu,lakini walikiri wanalo hilo sanduku la agano ila hawezi kuliona kutokana na masharti yao.
Naam
Zipo tofauti tofauti hata yule myahudi msomi alidai kwamba bado liko Jerusalam
Na wengine bado wakaamini lipo Rome hivyo documentary ziko tofauti tofauti

Jambo jingine kama hawa mabwana wameweza kutumia maandiko na vitamu vitakatifu kama Biblia kuteka akili za walimwengu na mamlaka nadhani hili nalo linaleta tafakuri pana.
Kuna kifungu kimoja hapo juu kwenye kinasema
Ni wasomi sana wanajua faida zilizomo ndani ya vitu vitakatifu na namna ya kuvitumia.

Andiko la ISAYA 14:14 linaongeza nguvu zaidi juu ya point hizi

Shukraani mkuu
 
Back
Top Bottom