Sanaa za msafara wa Magufuli kuzuiwa na wananchi

Wewe umeshakuwa mtu mzima!
Wanaposema msafara umezuiwa haiwezakani watu wakawa wamepambana magogo barabarani, hao watakuwa wameomba asipite hapo bila ya kuzungumza nao, haukuwa planned na hivyo raisi amelazimika kusimama kuongea na wananchi! Inawezekana umepangwa leo, au Jana au hata wiki iliyopita Ila point ni kuwa alilazimika kusimama eneo ambalo halikuwa ktk ratiba yaake!
Vinginevyo ktk nchi hii hakuna hata mtu mmoja anaweza kuzuia TINGATINGA likitaka kupita!
wameomba wapi na kutoka kwa nani protocol zinasemaje usanii mkubwa huyu raisi wa ajabu sana ataendeleza propaganda kama watu tumekinai
 
Kweli watanzania wengine ndo maana tuliitwa malofa ukweli hakuna mtu anayeweza fanya mambo kama JMP maana anaonyesha kitu toka moyoni yani angekuwa huyo fisadi mmmh
Jipu la zanzibar halioni, mbna yupo kimya kama anaweza kuingilia maamuzi ya mahakama anashindwaa nn hili la zbar, na suala la bunge kuoneshwa live ili tuone HAPA KAZI TU, hv kodi wanazokatwa watumishi kwa mishahara zimeshuka? Nakumbuka kama alisema hichi kitu kwa kampen zake au niliota?


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
msafala wa raisi unasimamishwaje na nani kwa kua njiani wanakua wao peke yao na kiusalama wanakua na mwendo kasi na mbele kunakua na escot kali sana nyuma gari za polisi nani anaweza simamisha na anadimamishaje na je kiusalama inakubalika msafala kusimamishwa na watu wasiopangwa wala sehemu isiyokaguliwa
 
Na nyinyi muwe mnasema kuwa lowasa kaandaliwa watu wa kuhutubia !
Magufuli sio level ya lowass manake anachokifanya una maana anakifuatisha ndio maana aliambiwabado hajakomaa kuongoza nchi unaona unavyotoa ushuhuda
 
Kuna retired jounalist alijiuzia mgodi wa makaa ya mawe kwa bei ya kununulia gari million 70 ndo maana anasema watanzania ni malofa kwel ss ni malofa nimeamini

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Ndo hao hao.
 
Kwa mfano wale Bodaboda walioenda kumuona lowasa pale Dodoma si mlituambia wameenda wenyewe bila kuitwa? Je ulimuona mwana ccm yeyote kaanzisha Uzi kuonesha kuwa Yale yalikuwa ni maigizo a Mzee?

Mbona ninyi ukawa roho zina wauma sana mafanikio ya Magu? Ninyi ni watu wa aina gani hata hamtaki rais wa nchi yako afanye kazi vizuri ili kila mtu akiwemo bibi yako kule kijijini awe na maisha mazuri kama ya Lowassa?

Hivi unafikiri Magufuli akishindwa kuongza nchi vizuri maisha magumu yatamwangukia nani? Si ni we we na ndgu zako ndio watakiona cha moto? Mna akili gani ninyi UKAWA?

JE, kuna mwanasanaa zaidi ya yule aliebeba wapiga Picha akaenda kuswaga ng'ombe akisema kule ndo kuchunga ng'ombe?

Mtakubali lin ninyi kwamba si kila MTU lazima awe shabiki wa chadema /ukawa?
 
Ni busara Rais abainishe wazi kuwa hatasimama tu kusema na wananchi kisa wamemsimamisha. Huu si utamaduni mzuri kabisa.
kwa vyovyote rais huenda kwa ratiba na muda. huu muda anaupataje au uko kwenye ratiba zake tuambiwe.
Ni kama mwalimu anaenda darasani kufundisha lakini hapa katikati anasimamishwa na wanafunzi wengine
 
hawa jamaa huwa wanasiasa flani hivi yaan
wanajua hawapendwi na majority so wanafanya hivyo kuwahadaa watu
waone wanapendwa na wananchii
mimi leo hata nimuone magu kaja kwetu sitompapatikia YAN kama edward lowasa
 
Lowassa alikusanya Wamasai wenzie njiani Morogoro akielekea Dodoma hukumuona?
Taifa hili lilimhitaji Magufuli kuwa Rais kabla hajazaliwa!

Mahakama ya Wanamtandao Mafisad itaanzishwa bila ya kupitia Bungeni kuepusha Genge la Fisadi Mkuu kuipinga!
Mahakama ya mafisadi??? Kwikiiiiii kwiiii hao waliofungwa wanatolewa waje kula bata mtaani na bilioni 3 zetu sasa iyo mahakama ya kazi gani acheni siasa.
 
Kwani mkisema Magufuli ameomba kuhutubia wananchi,maandalizi yakafanyika na mkusanyiko ukapatikani itaonekanaje?jamani kampeni zimeisha,sioni tatizo kama mtakuwa wakweli.Hapa ITV nashuhudia habari kuwa Magufuli kazuiwa na wananchi ili ahutubie.Ukitazama mazingira huoni dalili hizo.isipokuwa ni mkusanyiko ulioandaliwa kwa shughuli maalimu

Kwani wananchi wakiandaliwa kumsikiliza mkombozi wao kuna shida gani. Mbona yule mgonjwa alipokuwa anatoka dodoma alipita pale kibaigwa akaongea na primitives wenzake. Usijitoe ufahamu
 
Rais anauhuru wakuhutubia sehemu yoyote anayotaka kwan ni njia mojawapo ya kuwasiliana na wananchi. Nadhan mtoa mada anahoji kitendo cha kusema wananchi wamezuia msafara wa rais ili awahutubie. Ukitaka kujua rais analindwa vipi hebu jikusanyeni barabarani ili mzuie huo msafara muone nini kitatokea. Ni vizuri kuwa wakweli kwa kusema rais amesimama kuwahutubia wananchi na si wananchi wamezuia msafara wa rais ili awahutubie. Mbona wananchi wakitaka kwenda kumuona rais ili awahutubie polisi wanazuia?
 
wameomba wapi na kutoka kwa nani protocol zinasemaje usanii mkubwa huyu raisi wa ajabu sana ataendeleza propaganda kama watu tumekinai
Dada usuchokujuwa usishupaze mishipa nakushaur endelea kulinda ndoa yako mengine waachie wanaume
 
wameomba wapi na kutoka kwa nani protocol zinasemaje usanii mkubwa huyu raisi wa ajabu sana ataendeleza propaganda kama watu tumekinai
Hakuna protocol inayomkataza raisi kuongea na watu wake!
Wameomba wapi na kwanani hilo nadhani sina uwezo wa kujibu, lkn simply wanaweza hata kuomba kwa ccm mkoa, Mkuu wa wilaya au mkoa, au just kutime msafara na kutengeneza kundi kubwa kando ya barabarà ili kumfanya raisi aone kuna tija ya kuongea nao! Sababu zote hizo zinatosha kuwafanya wao ndio wawe wamezuia msafara!
Halafu sijaelewa wewe unachukia nini? Kuna vitu vya kuchukiza unavichekelea halafu vyenye kufurahisha wewe unachukia!
ie. Umechukizwa na raisi kusimamisha msafara na kuongea na wananchi, lkn unafurahishwa na ukawa kuvuruga bunge kwa kuwa haliko live! Huchukizwi na Lowasa kutembelea mikoa na kuanza kampeni za 2020 huku akishutumu kuwa ameibiwa kura!
Watanzania ni watu wa ajabu kwelikweli
 
Back
Top Bottom