PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,725
Nilipita kIWANJA CHA NDEGE aRUSHA JANA nikakuta kuna ndege (helikopta) nyingi zimepaki kama daladala zikisubiri abiria wa Samunge!
Kilichonisikitisha ni kwamba helikopta zote hizo ni za kigeni kutoka Rwanda, Burundi na Kenya, kasoro moja tu ambayo ni ya Mtanzania Ndesamburo!
Bei ya abiria mmoja kwa helikopta ni $1300 kwenda na kurudi Samunge.
Ukiacha chaji ndogondogo wanazolipa hawa wamiliki wageni zinazokaribia $500 kwa safari moja kwa ndege moja, wao wanaondoka na wastani wa $ 5000 kwa kila safari, na kuzipeleka kwao Kenya Rwanda na Burundi.
Tanzania nchi yangu utalala hata lini?