Samunge Bado Ni Tishio!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,725
IMAG0710.JPG
Nilipita kIWANJA CHA NDEGE aRUSHA JANA nikakuta kuna ndege (helikopta) nyingi zimepaki kama daladala zikisubiri abiria wa Samunge!

Kilichonisikitisha ni kwamba helikopta zote hizo ni za kigeni kutoka Rwanda, Burundi na Kenya, kasoro moja tu ambayo ni ya Mtanzania Ndesamburo!

Bei ya abiria mmoja kwa helikopta ni $1300 kwenda na kurudi Samunge.

Ukiacha chaji ndogondogo wanazolipa hawa wamiliki wageni zinazokaribia $500 kwa safari moja kwa ndege moja, wao wanaondoka na wastani wa $ 5000 kwa kila safari, na kuzipeleka kwao Kenya Rwanda na Burundi.
Tanzania nchi yangu utalala hata lini?
 

Attachments

  • IMAG0712.JPG
    IMAG0712.JPG
    389.4 KB · Views: 68
  • IMAG0715.JPG
    IMAG0715.JPG
    395.4 KB · Views: 66
  • IMAG0719.JPG
    IMAG0719.JPG
    429.6 KB · Views: 68
Mkuu PJ, kama hatuna uwezo wa kuzimiliki ina maana tukatae hata kushirikiana na wageni wanapoleta za kwao ili tuzitumie?

Nijakupata vyema bandugu :thinking:
 
Mkuu PJ, kama hatuna uwezo wa kuzimiliki ina maana tukatae hata kushirikiana na wageni wanapoleta za kwao ili tuzitumie?

Nijakupata vyema bandugu :thinking:

Anachosema PJ ni je wanalipa kodi stahiki ?
 
Siyo hilo tuu kwamba usingizi wa watanzania ni jambo linalomshtua zaidi.Wazawa hawawezi hata kumiliki chopper,wengi ni wageni?Pia kwamba uchumi wa nchi hii unawategemea sana wageni hata kuchuma matunda yao ya ugunduzi wao? Na je wako wapi watoza ushuru mafisadi uchwara wenye kuangamiza nchi kwa jinsi hizo???Huo ndio mshangao wa Paka Jimmy.
 
Kwani Tanzania au bora Tanganyika unafikiri tuna chochote? kama kuna kampuni hapa kwa asilimia za kweli ya mzalendo basi asilimia 5 hazifiki, hebu ondoa nchi jirani ikiwemo wa nchi jirani inayotutawala yaani zanzibar, kama kina bakhresa na wapemba wenzake, halafu ondoa na waasia, kitabaki kitu tanganyika?
 
serikali tu imeshindwa kuwa na Kampuni ya Daladala za Anga, itakuwa raia? nduge hapa Ukiondoa Zan Air ya Zenji, precision ya Kenya Airways, na Coastal Aviation ya Mtaliano wa Slipway Nicola, tutabaki ile ndege moja ya jeshi...
Tanganyika ni shamba na bibi, acha jirani waneemeke.... niseme nini?
 
Mkuu PJ, kama hatuna uwezo wa kuzimiliki ina maana tukatae hata kushirikiana na wageni wanapoleta za kwao ili tuzitumie?

Nijakupata vyema bandugu :thinking:
Mkuu,
Sijajua ni ushirikiano gani unaoongelea hapa, maana sijaona dalili yoyote ya kushirikiana!!
Hawa jamaa wanalipa ada kidogo tu za Air Navigation, lakini kama serikali haiingizi kitu!
Kampuni ya kigeni inapofanya biashara ya namna hiyo nchini nilitegemea kitu kama Mrahaba fulani, au concession fees, mbali ya ada hizo, ikiwa ni namna ya kuenzi eneo ilikopatikana biashara!
Kilichopo hapa ni kuhamisha hela!...
 
Duh! Mi nimeziona hata leo lakini ckujua ni kw ajili ya kuruka kwa Babu. Ama kweli mataifa mengine wametuona lala kabisa.
 
Well nadhani muda si mrefu tutataka ripoti ya ni kiasi gani walichokusanya kwenye issue ya Loliondo na kimefanyia nini kiasi hicho,vipi mkazi wa samunge kafaidika na mengine mengi....PJ nimekusoma mkuu!
 
Jamaa wanachuma kwa mgongo wa Babu! Nchi yetu bado imelala tukiamka, wameshamaliza kama wanavyofanya kwenye madini! Wizara husika mko wapi?
 
Back
Top Bottom