Nsennah
JF-Expert Member
- Jan 9, 2021
- 1,560
- 1,085
Ndoto iliyopitishwa!! Usiku ule nikiwa ndotoni ghafla nikaona madaraja matatu mazuri ambayo ni msaada mkubwa kwa wananchi wote; Nyerere bridge, Busisi bridge na Samia Bridge!! Daraja moja limeanzishwa na kujengwa na Mama mzaliwa wa visiwa vya Zanzibar hadi kukamilika hivyo kwa kuheshimu na kuuthamini mchango wake kwa sauti ya pamoja daraja hilo likaitwa Samia bridge ili akumbukwe kutoka kizazi hadi kizazi. Madaraja mengine yanafahamika lakini daraja la Samia ndiyo ndoto inayoishi. Daraja la Samia linaunganisha kisiwa na ni wilaya ya Ukerewe hadi wilaya ya Bunda. Mbali ya kuwa kivutio kikubwa pia linakuwa msaada mkubwa sana kwa watanzania wa kisiwani humo na watanzania wengine wote kwa kuwarahisishia shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matibabu ya watu wa kibara katika hospitali ya rufaa inayojengwa wilayani Ukerewe. Ndoto ya muda mrefu inaenda kutimizwa na Mama huyu shujaa, kwa hakika mama anaifungua nchi ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Nawasalimu kwa jina la Jamhuri, wote mnatakiwa kujibu KAZI IENDELEE. Mungu ibariki Tanzania na Mungu mbariki shujaa huyu wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan katika kutimiza ndoto hii inayoishi.