~^^~ Sambusa ni tamu bwana! ~^^~

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
sambus.jpg

Sambusa ni tamu bwana,
Nyingine hakuna tena,
Wa kijiji ninanena,
Vingine sijaviona! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Ukishaonja sambusa,
Vitumbua utasusa
Na utatumia mapesa,
Uje upate sambusa! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na zile zenye mafuta
Ulimini zinanata,
Na ladha ukishapata
Waweza tangaza vita - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye nyamanyama
Zaliwa Kijitonyama
Hata ukenda Dodoma
Sambusa hutojinyima - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zile zenye mboga
Zilochumwa kama boga
Wale wasio waoga
Wazila hata Msoga! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye vitunguu
Zilotiwa karafuu
Ukila mluzi huu
Waimba "mikono juu" - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na sambusa za Kihindi,
Utazikuta Malindi
Hata Mtwara na Lindi
Zinapikwa na mafundi! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Uonje 'zopikwa Tanga
Ngonjera utazitunga
Ukipata za Iringa
Na baridi la Mafinga - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Beti zangu nazifunga
Tungo nimeshazipanga,
Sambusa sitojivunga
Nayeya ninapuyanga
SAMBUSA NI TAMU BWANA, HASA ZISIZOFANANA!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Zisizofanana wapi zipo
Ewe malenga lojaa fumbo,
Kila nfumbapo jicho,zanijia kufanana

Hadi iitwe sambusa
Si mradi iwe hasusa
Ingekuwa vile rukhsa,basi mbona wangejirusha?

Labda ninyambulie
Ni kipi kitangulie
je ni lile umbile, au ni kilichomo mle?
 
Ni ipi hiyo sambusa ,malenga wetu nijuze
Ile ya kwa mama lishe au ya mama nyumbani
Ile ya five star utamu ulokithiri kuing'ata kwa zako mbwembe au ya bibi kijijini ilopikwa asilia
Malenga hebu nijuze ni ipi hiyo sambusa Ya kijiji au mji ipi waiongelea ?
 
Mwana unatisha kwa mashairi yako, unaonaje ukatengeneza kasingle? Ila nakuuliza kwa nini waisifia sambusa namna hii? Mbona hujasifia kitumbua? Hebu nipe mshairi ya kukisifu kitumbua kidogo Mwana.
 
Mwanakijiji!!

Sambusa ushasifia
kidondani sijefia
Zenye mboga na nyama
Tanga na kijitonyama- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

Sambusa zile za nyama
Kula hovyo ni kiyama
Si zote zenye ubora
zipo zenye matambara- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

Za mboga nazo si salama
Wengi wameshalalama
Mboga nyingi zimeoza
Ndani wakasokomeza- Hala hala kaka yangu, sijezila zilooza

Mwisho ninamalizia
wasijekukuuzia
Sidanganyike na ganda
makini hata uganda- hala hala kaka yangu, sijezila zilooza.
 
Sambusa ni tamu bwana,
Nyingine hakuna tena,
Wa kijiji ninanena,
Vingine sijaviona! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Ukishaonja sambusa,
Vitumbua utasusa
Na utatumia mapesa,
Uje upate sambusa! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na zile zenye mafuta
Ulimini zinanata,
Na ladha ukishapata
Waweza tangaza vita - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye nyamanyama
Zaliwa Kijitonyama
Hata ukenda Dodoma
Sambusa hutojinyima - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zile zenye mboga
Zilochumwa kama boga
Wale wasio waoga
Wazila hata Msoga! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye vitunguu
Zilotiwa karafuu
Ukila mluzi huu
Waimba "mikono juu" - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na sambusa za Kihindi,
Utazikuta Malindi
Hata Mtwara na Lindi
Zinapikwa na mafundi! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Uonje 'zopikwa Tanga
Ngonjera utazitunga
Ukipata za Iringa
Na baridi la Mafinga - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Beti zangu nazifunga
Tungo nimeshazipanga,
Sambusa sitojivunga
Nayeya ninapuyanga
SAMBUSA NI TAMU BWANA, HASA ZISIZOFANANA!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Haya malenga wa mtang'ata,
Kama siyo kule Tanga,
Mbona watupa kutanga?

Sambusa ulotuwekea
Kumbe zile tuzozoelea
Ila kweli hukupotea, kutaka zisizofanana

Kila nikicheki picha
macho ninayafikicha
Hizo ni sambusa au picha,

Nijuavyo sambusa mie
Shurti vyote vitimie
Mtu asikupimie
 
Sambusa ni tamu bwana,
Nyingine hakuna tena,
Wa kijiji ninanena,
Vingine sijaviona! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Ukishaonja sambusa,
Vitumbua utasusa
Na utatumia mapesa,
Uje upate sambusa! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na zile zenye mafuta
Ulimini zinanata,
Na ladha ukishapata
Waweza tangaza vita - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye nyamanyama
Zaliwa Kijitonyama
Hata ukenda Dodoma
Sambusa hutojinyima - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zile zenye mboga
Zilochumwa kama boga
Wale wasio waoga
Wazila hata Msoga! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Zipo zenye vitunguu
Zilotiwa karafuu
Ukila mluzi huu
Waimba "mikono juu" - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Na sambusa za Kihindi,
Utazikuta Malindi
Hata Mtwara na Lindi
Zinapikwa na mafundi! - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Uonje 'zopikwa Tanga
Ngonjera utazitunga
Ukipata za Iringa
Na baridi la Mafinga - sambusa ni tamu bwana, hasa zisizofanana!

Beti zangu nazifunga
Tungo nimeshazipanga,
Sambusa sitojivunga
Nayeya ninapuyanga
SAMBUSA NI TAMU BWANA, HASA ZISIZOFANANA!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)

Mwanakijiji weeeeee unamambo!!!!!!
 
Alafu hizi sambusa zaliwa kwa kijiko au? maana kwenye picha naona kuna kijiko ati au ni kwa ajili ya kusevia tu alafu baada ya hapo hakina kazi?
Mwana kijiji bana!!
 
i am very sure kwamba watu hawajamsoma huyu babu anachokihubiri na utamu wake kwa kupitia taswira ya SAMBUSA!
lakini twende tu hivo hivo
 
Ni nini kimekufanya, kuzipenda sambusa
Mawazo nimetawanya, jibule nimelikosa
Ni nyama imekufanya, kuisifia sambusa
Tuambie ni kitu gani, kwenye utamu wa sambusa.

Kama nyama upendayo, hata kababu wanaweka
Au mboga waiwekayo, mpaka waweweseka,
Ni sahani wawekeyayo, inayokupa mzuka
Siioni tofauti, ya sambusa boflo bagia

Labda ni umbo lake, hasa ukiliangalia
Ndo chakula pekee, pembe tatu kuwekea
Ncha chini uiweke, hisia zanisongea
Hapo jibu nalipata, utamu wa hiyo sambusa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom