Samaki aina ya Pomboo

njiwa

JF-Expert Member
Apr 16, 2009
12,369
5,514
habari zenu wanajamii .. mimi huwa najitatiza swala zima la huyu samaki pomboo
sijapa kumuona na pia sijui kizungu aitwaje? je ni kama wale binti wazuri wa kusadikaka katika hadithi zetu samaki nguva?

na je kuna ushahidi kuhusu sama mtu!?

naomba mnitatulie

kuna watu wapenda kubeza wenzao kwa maswali waulizayo.. kama ukiona upuuzi naomba usinijibu..
 
Pomboo kwa kizungu anaitwa dolphin. Nilisikia kwenye BBC siku moja nisielewe ni aina gani ya samaki.
Wapi ulisikia likitajwa neno hilo?

attachment.php
 
Attachments

  • dolphin-cow.jpg
    dolphin-cow.jpg
    30.4 KB · Views: 9,673
Dolphin si samaki bali ni mamalia. Ni mmoja kati ya viumbe wenye akili sana, Douglas Adams katika hadithi zake za sayansi ya kuyumkinika amesema kuwa hawa Dolphin wana akili kuliko binadamu :).
 
habari zenu wanajamii .. mimi huwa najitatiza swala zima la huyu samaki pomboo
sijapa kumuona na pia sijui kizungu aitwaje? je ni kama wale binti wazuri wa kusadikaka katika hadithi zetu samaki nguva?

na je kuna ushahidi kuhusu sama mtu!?

naomba mnitatulie

kuna watu wapenda kubeza wenzao kwa maswali waulizayo.. kama ukiona upuuzi naomba usinijibu..
Nguva: Mnyama aelezwaye ``ndivyo sivyo``

Source: Nguva: Mnyama aelezwaye ``ndivyo sivyo``

Mnyama aina ya Nguva ambaye watu wamekuwa wakimwelezea kwa namna tofautitofauti, yuko hatarini kutoweka endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kama Mwandishi Joseph Mwendapole anavyofafanua.

Watu wengi hawajui uhalisi wa mnyama huo kwani baadhi ya watu wamekuwa wakisema ni upande mmoja samaki na mwingine mwanamke.

Makumbusho ya taifa ambayo ndiyo ina dhamana ya kuhifadhi mambo ya kale imeweka wazi ukweli kuhusu nguva na maisha yake.

Mkurugenzi wa Makumbusho hayo, Bw. Paul Msemwa, anasema mnyama huyo mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu mnyama huyo si ya kweli.

Anasema nguva ni mnyama anayezaa na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine.

Anasema wakati akinyonyesha husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

Anaeleza kuwa watu wengi hawajui ukweli kuhusu nguva na baadhi wamekuwa wakisema kuwa ni nusu mtu.

``Kuna watu wanapotosha wanasema nguva ni nusu mtu kwa maana kuwa chini ni samaki na juu ni mtu lakini si kweli,`` anasema.

Anasema muda mrefu mnyama huyo hukaa baharini na kwamba anapenda mazingira mazuri na tulivu.

Dk. Msemwa anasema mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto mmoja pekee.

Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000.

Dk. Msemwa anataja maeneo ambayo wanyama hao hupatikana kuwa ni Somanga karibu na Rufiji, Kilwa, Mafia, Moa Mombasa, Tanga na Bagamoyo.

Anasema endapo mazingira ya bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho kutoweka.

Alisema kwa kawaida nguva hupenda maeneo tulivu na yasiyo na vitisho.

``Huu uvuvi haramu wa mabomu na baruti utasababisha wanyama hawa kutoweka kabisa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa,`` anasema.

Anasema mnyama huyo hupendelea zaidi kula majani yaliyo chini ya bahari maarufu kama mwani.

Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe.

Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake.

Dk. Msemwa anasema nguva jike ana chuchu kifuani na anaponyonyesha mwanaye husimama kwa kutumia mkia wake chini na kumkumbatia mwanaye kama binadamu.

Aidha, anasema tayari wameanza kuwaelimisha wavuvi kuhusu mnyama huyo ili wamwonapo wasimvue.

Anasema kuna wakati wavuvi walikuwa wakiwavua na kuwala kwa kuwa nyama yao ni tamu zaidi ya ile ya ng�ombe.

Anasema kutokana na mazingira kuharibiwa, hivi sasa mnyama huyo ameanza kutoweka sehemu ambazo alikuwa akionekana.

``Alikuwa akionekana Dar es Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena na hali hii inatokana na usumbufu wa wavuvi na mazingira ya bahari kuchafuliwa,`` anasema.

Anasema mnyama huyo ana aibu na anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huhama na kwenda mbali zaidi.

Dk. Msemwa anasema vifo vya nguva vimekuwa vikitokana na ajali za bahati mbaya mfano kunaswa kwenye vyombo vya kuvulia kama vile jarife, mishipi na kuongezeka kwa shughuli za uvuvi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Viumbe katika makumbusho hayo, Bi. Adelaide Sailema alisema wameanza kuelimisha wavuvi ili wanapowaona wanyama hao wasiwavue.

Anasema kuna umuhimu wa kuweka maeneo tengefu kwa ajili ya kuwahifadhi wanyama hao.

``Tumeishauri serikali itenge maeneo ambayo mnyama huyo anapatikana ili wasitoweke,`` anasema.

Anafafanua kuwa mtawanyiko wa nguva upo zaidi maeneo ya Somanga, Kilwa, delta ya Rufiji, Mohoro na Mafia kuanzia miaka ya 1960.

Anasema nguva amekuwa akionekana mara nyingi zaidi miaka ya 1950 sehemu za Kilwa Kivinje miaka ya 1960 sehemu za Mkwaja na Matapata miaka ya 1970 sehemu za Kilwa kisiwani, Kilwa Masoko na kaole miaka ya 1980 sehemu za Somanga, Pombwe na Olelo miaka ya 1990 sehemu za Masoko Pwani na miaka ya 2000 sehemu za Somanga, Utigi Ngolwe, Pombwe na Mbonde.

Sehemu zingine zilizoripotiwa kuwa na nguva ni Lamu, pangani, Tanga, Buyuni, Kimbiji, Unguja, Pemba, Mafia na Kisiju.

Dk. Msemwa anasema nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

Wakati huo huo, anasema ukumbi wa kudumu wa viumbe (biolojia) ni kati ya kumbi nne za kudumu zilizopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Anasema ukumbi huo ulianzishwa rasmi mwaka 1980 baada ya kumbi nyingine kuwepo ambazo ni ukumbi wa chimbuko la Mwanadamu, ukumbi wa historia ya Tanzania na ukumbi wa mila na desturi za Mtanzania.

Anasema ukumbi wa viumbe ulipoanzishwa ulilenga zaidi maonyesho ya viumbe bahari na mara nyingi ulijulikana ukumbi wa viumbe bahari (Marine Biology Gallery).

Anasema moja ya maonyesho yaliyopo katika ukumbi huo ni maonyesho ya mnyama Nguva ambaye kwa mara nyingi amekuwa akiamisha maswali na majibu ya aina mbalimbali kutoka katika jamii kama ni nusu samaki na nusu mwanamke.

Anaeleza kuwa kutokana na mahitaji mbalimbali ya jamii yaliyojitokeza, ilionekana kuwa ni sahihi kuwa na viumbe kutoka katika mifumo ikolojia mbalimbali ili kuweza kukidhi haja.

Anasema kwa sasa mikusanyo iliyopo imegawanyika katika sehemu kuu tatu kutokana na mifumo ikolojia ilikotoka mikusanyo hiyo.

Anatoa mfano wa mfumo ikolojia wa bahari
Wenye wanyama wanyonyeshao, samaki, kamba kochi, kasapweza, miamba ya matumbawe, majongoo bahari, konokono na kaa.

Huyu ndiye nguva

dugong04.jpg

dugong&homme.jpg

Wapo wanaofirkiria kuwa nguva au Mermaid yupo hivi

Samaki.jpg

Dolphin si samaki bali ni mamalia. Ni mmoja kati ya viumbe wenye akili sana, Douglas Adams katika hadithi zake za sayansi ya kuyumkinika amesema kuwa hawa Dolphin wana akili kuliko binadamu :).

Hizo ni science za kuyumkinika kweli. Ana akili kuliko binadamu?!!
 
kusema ukweli mimi ni mmoja wao niliofikiri nguva ni nusu samaki nusu mtu,
 
nimekulia tanga mjini na nyumbani ni pwani ya moa karibu na mombasa ila kila nikienda nasikia hili neno pomboo.. asante kwa kunijulisha ni dolphin kumbe
 
Kweli sayansi ya viumbe wa bahari ni ngumu.
Akhsantum kwa ufafanuzi wenu
 
Nguva: Mnyama aelezwaye ``ndivyo sivyo``

Source: Nguva: Mnyama aelezwaye ``ndivyo sivyo``

Mnyama aina ya Nguva ambaye watu wamekuwa wakimwelezea kwa namna tofautitofauti, yuko hatarini kutoweka endapo jitihada za makusudi hazitachukuliwa kama Mwandishi Joseph Mwendapole anavyofafanua.

Watu wengi hawajui uhalisi wa mnyama huo kwani baadhi ya watu wamekuwa wakisema ni upande mmoja samaki na mwingine mwanamke.

Makumbusho ya taifa ambayo ndiyo ina dhamana ya kuhifadhi mambo ya kale imeweka wazi ukweli kuhusu nguva na maisha yake.

Mkurugenzi wa Makumbusho hayo, Bw. Paul Msemwa, anasema mnyama huyo mambo mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu mnyama huyo si ya kweli.

Anasema nguva ni mnyama anayezaa na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine.

Anasema wakati akinyonyesha husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

Anaeleza kuwa watu wengi hawajui ukweli kuhusu nguva na baadhi wamekuwa wakisema kuwa ni nusu mtu.

``Kuna watu wanapotosha wanasema nguva ni nusu mtu kwa maana kuwa chini ni samaki na juu ni mtu lakini si kweli,`` anasema.

Anasema muda mrefu mnyama huyo hukaa baharini na kwamba anapenda mazingira mazuri na tulivu.

Dk. Msemwa anasema mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto mmoja pekee.

Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000.

Dk. Msemwa anataja maeneo ambayo wanyama hao hupatikana kuwa ni Somanga karibu na Rufiji, Kilwa, Mafia, Moa Mombasa, Tanga na Bagamoyo.

Anasema endapo mazingira ya bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho kutoweka.

Alisema kwa kawaida nguva hupenda maeneo tulivu na yasiyo na vitisho.

``Huu uvuvi haramu wa mabomu na baruti utasababisha wanyama hawa kutoweka kabisa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa,`` anasema.

Anasema mnyama huyo hupendelea zaidi kula majani yaliyo chini ya bahari maarufu kama mwani.

Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe.

Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake.

Dk. Msemwa anasema nguva jike ana chuchu kifuani na anaponyonyesha mwanaye husimama kwa kutumia mkia wake chini na kumkumbatia mwanaye kama binadamu.

Aidha, anasema tayari wameanza kuwaelimisha wavuvi kuhusu mnyama huyo ili wamwonapo wasimvue.

Anasema kuna wakati wavuvi walikuwa wakiwavua na kuwala kwa kuwa nyama yao ni tamu zaidi ya ile ya ng�ombe.

Anasema kutokana na mazingira kuharibiwa, hivi sasa mnyama huyo ameanza kutoweka sehemu ambazo alikuwa akionekana.

``Alikuwa akionekana Dar es Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena na hali hii inatokana na usumbufu wa wavuvi na mazingira ya bahari kuchafuliwa,`` anasema.

Anasema mnyama huyo ana aibu na anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huhama na kwenda mbali zaidi.

Dk. Msemwa anasema vifo vya nguva vimekuwa vikitokana na ajali za bahati mbaya mfano kunaswa kwenye vyombo vya kuvulia kama vile jarife, mishipi na kuongezeka kwa shughuli za uvuvi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Viumbe katika makumbusho hayo, Bi. Adelaide Sailema alisema wameanza kuelimisha wavuvi ili wanapowaona wanyama hao wasiwavue.

Anasema kuna umuhimu wa kuweka maeneo tengefu kwa ajili ya kuwahifadhi wanyama hao.

``Tumeishauri serikali itenge maeneo ambayo mnyama huyo anapatikana ili wasitoweke,`` anasema.

Anafafanua kuwa mtawanyiko wa nguva upo zaidi maeneo ya Somanga, Kilwa, delta ya Rufiji, Mohoro na Mafia kuanzia miaka ya 1960.

Anasema nguva amekuwa akionekana mara nyingi zaidi miaka ya 1950 sehemu za Kilwa Kivinje miaka ya 1960 sehemu za Mkwaja na Matapata miaka ya 1970 sehemu za Kilwa kisiwani, Kilwa Masoko na kaole miaka ya 1980 sehemu za Somanga, Pombwe na Olelo miaka ya 1990 sehemu za Masoko Pwani na miaka ya 2000 sehemu za Somanga, Utigi Ngolwe, Pombwe na Mbonde.

Sehemu zingine zilizoripotiwa kuwa na nguva ni Lamu, pangani, Tanga, Buyuni, Kimbiji, Unguja, Pemba, Mafia na Kisiju.

Dk. Msemwa anasema nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho.

Wakati huo huo, anasema ukumbi wa kudumu wa viumbe (biolojia) ni kati ya kumbi nne za kudumu zilizopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni.

Anasema ukumbi huo ulianzishwa rasmi mwaka 1980 baada ya kumbi nyingine kuwepo ambazo ni ukumbi wa chimbuko la Mwanadamu, ukumbi wa historia ya Tanzania na ukumbi wa mila na desturi za Mtanzania.

Anasema ukumbi wa viumbe ulipoanzishwa ulilenga zaidi maonyesho ya viumbe bahari na mara nyingi ulijulikana ukumbi wa viumbe bahari (Marine Biology Gallery).

Anasema moja ya maonyesho yaliyopo katika ukumbi huo ni maonyesho ya mnyama Nguva ambaye kwa mara nyingi amekuwa akiamisha maswali na majibu ya aina mbalimbali kutoka katika jamii kama ni nusu samaki na nusu mwanamke.

Anaeleza kuwa kutokana na mahitaji mbalimbali ya jamii yaliyojitokeza, ilionekana kuwa ni sahihi kuwa na viumbe kutoka katika mifumo ikolojia mbalimbali ili kuweza kukidhi haja.

Anasema kwa sasa mikusanyo iliyopo imegawanyika katika sehemu kuu tatu kutokana na mifumo ikolojia ilikotoka mikusanyo hiyo.

Anatoa mfano wa mfumo ikolojia wa bahari
Wenye wanyama wanyonyeshao, samaki, kamba kochi, kasapweza, miamba ya matumbawe, majongoo bahari, konokono na kaa.

Huyu ndiye nguva

dugong04.jpg

dugong&homme.jpg

Wapo wanaofirkiria kuwa nguva au Mermaid yupo hivi

Samaki.jpg

From Wikipedia, the free encyclopedia
For other uses, see Mermaid (disambiguation).
Mermaid

A Mermaid by John William Waterhouse
Creature
Grouping Mythological
Sub grouping Water spirit
Similar creatures Merman
Siren
Ondine
Data
Mythology World mythology
First reported c. 1000BC
Country Worldwide
Habitat Ocean, sea

Mermaid and merman, 1866. Anonymous Russian folk artist.
A mermaid is a mythological aquatic creature with a human head and torso and the tail of an aquatic animal such as a fish or dolphin. The word is a compound of mere, the Old English word for "sea," and maid, a woman. The male equivalent is a merman, however the term mermaid is sometimes used for males. Various cultures throughout the world have similar figures, typically depicted without clothing.
Much like sirens, mermaids would sometimes sing to people and gods and enchant them, distracting them from their work and causing them to walk off the deck or run their ships aground. Other stories have them squeezing the life out of drowning men while attempting to rescue them. They are also said to take humans down to their underwater kingdoms. In Hans Christian Andersen's The Little Mermaid it is said that they forget that humans cannot breathe underwater, while others say they drown men out of spite.
The sirens of Greek mythology are sometimes portrayed in later folklore as mermaid-like; in fact, some languages use the same word for both bird and fish creatures, such as the Maltese word 'sirena'. Other related types of mythical or legendary creature are water fairies (e.g. various water nymphs) and selkies, animals that can transform themselves from seals to humans.
 
A mermaid is a mythological aquatic creature with a human head and torso and the tail of an aquatic animal such as a fish or dolphin. The word is a compound of mere, the Old English word for "sea," and maid, a woman. The male equivalent is a merman, however the term mermaid is sometimes used for males. Various cultures throughout the world have similar figures, typically depicted without clothing.

Mtu asipoelewa maana ya hilo neno huenda akaelewa vibaya ujumbe ulioko hapo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom