Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #61
Wazazi wa Salva Rweyemamu walizaliwa wapi?
Hivi kuna mtu anajua kama huyu Salva ni raia wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya uraia ya 1995?
mbona miye hata sina tatizo.. Bahati nzuri miye sijabadili upande kwenye suala hili. Nilipoliuliza swali hili mara ya kwanza ilikuwa out of logical deduction nikiwa sina sababu yoyote ya kutilia shaka.. that is why ukienda kwenye thread ya kuteuliwa kwake nimempa pongezi zake.
Nilipouliza mara ya kwanza kama ni raia nilikuwa naendeleza wazo la kuhusu Jenerali Ulimwengu kuwa "kama Generali licha ya kushika nafasi zote za serikalini na kwenye chama, lakini baadaye wakauhoji uraia wake na kumlazimisha aombe upya, je hawataweza kumgeuka huyu bwana (Rweyemamu)?" Niliuliza kwa minajili ya hoja tu.
Sasa swali hilo likafutwa ghafla na majibu yaliyofuatia yakafutwa. Hapo ndipo nilipojikuta nimepata udadisi sasa kwamba inakuwaje tusiulize uraia wa ndugu yetu huyu?
Sasa nilipoliformulate swali hili upya kwa kutumia article ya "The East African" nilitaka kuonesha kuwa "siyo ajabu kuwa Tanzania imeruhusu watu wenye uraia nje ya Tanzania kushika nafasi mbalimbali". Sasa tunapouliza kuwa kama huyu naye ni Raia si kwake binafsi, as a matter of fact, kama kuna mtu ana mashaka na Uraia wa Mwamunyange, Kallaghe, au mtu yeyote aliyeteuliwa kushika nafasi yoyote nyeti, ni lazima jibu hilo liwe la uhakika.
Nisingeendelea na mada hii kama mtu mmoja angesema tu.. "Salva alizaliwa mahali fulani, na wazazi wake walizaliwa mahali fulani".
Sasa kwa mujibu wa sheria yetu ya Uraia, Wazazi wako kama walikuwa ni raia wa Tanzania kabla ya Muungano au raia wa Tanganyika au Zanzibar basi watoto wanaozaliwa wanakuwa ni raia. Hata hivyo kama wazazi wako walikuwa na uraia wa nchi nyingine kabla ya Muungano, na wewe ukazaliwa katika Tanzania iliyoungana hauwi raia automatically, siyo kama Marekani ambao ukizaliwa katika eneo lolote la Marekani unakuwa ni raia.
Hivyo, Salva anaweza kabisa kuwa amezaliwa na kukulia Tanzania (kama ilivyokuwa Generali) lakini kama wazazi wake walikuwa hawana uraia wa TAnzania alitakiwa (kwa mujibu wa sheria) kuukana uraia wa wazazi wake alipofikisha miaka 18. Kama ameendelea kuishi na kufanya kazi kama Mtanzania na baadaye ikaja gundulika kuwa hakuwa raia, basi anayo kila sababu ya kuomba uraia wa TAnzania na akikubaliwa ana haki kama Richa Adhia na mtanzania mwingine yoyote yule.
Kwa wale wanaoshangaa inakuwaje niulizie uraia wa Salva wakati nilikuwa nautetea uraia wa Richa jibu ni rahisi. Richa wazazi wake wote wawili walikuwa ni Raia wa Tanganyika, na Raia wa Jamhuri ya Zanzibar kabla ya Muungano.
Sihoji uraia wa Salva ili anyimwe nafasi fulani (kama wabaguzi wetu wa rangi walivyofanya kwenye suala la Richa) ninahoji uraia wake ili astahili nafasi hiyo, kwani kama siyo Raia wa Tanzania kumpa nafasi nyeti Ikulu ni sawa na kuwategemea wale wa kufunzi wa Chuo cha Benki na wale wa Mzumbe ambao kwa miaka nenda rudi na kwa jasho la Watanzania walisomesha na kupewa nafasi mbalimbali hata hivyo Rwanda ilipokuwa imetengamaa, wao wakaacha kazi zao wakarudi kutumikia nchi walizokuwa na utii nazo.
Ndiyo maana Mwalimu alisema msingi wa uraia wowote ni utii kwa nchi.
mbona miye hata sina tatizo.. Bahati nzuri miye sijabadili upande kwenye suala hili. .
Ngabu,
hayo ma-vyeti ya kuzaliwa bongo si unaenda tu pale uzazi na vifo una nunua na kuweka mwaka unaotaka wewe kuwa umezaliwa.........jamaa ana point anataka ku-make, tumsubiri tuone ni nini hasa hiyo point. Kwani msee mwkjj anatembea kwenye very thin line inayotenganisha watu wawili wenye tatizo la uraia ktk almost same circumstances.........interesting!!!!!!!
Kichwamaji
Nadhani hapa kinachoonekana ni kuwa dhambi ambayo Salva alimtendea Salim inataka kumtafuna mwenyewe, Salim kimsingi ameondoka kwenye Politics kutokana na mkono wa Salva. Na ukiangalia utakuta si watanzania wengi ambao hawana uraia wa Tanzania. Wapo wachache, lakini wakianza kusumbua wenyeji ndio wanaanza kupekuliwa uraia wao....i hate Salva. Alifanya watanzania tupoteze mtu mzuri, na matokeo yake we now have a bogus government