Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Ndo maana watu wenye mapenzi mema na nchi yetu wanawapa tahadhari mapema. Kwa sababu kama hawatataka kuyakubali matokea basi wajiandae kulazimishwa kuyakubali. Na huo ndio upuuzi ambao watu wengi hawautaki kwa sababu madhara yake yatakuwa makubwa sana kwao na wananchi wasio na hatia.
Naunga mkono maneno yako kwa asili mia. Hatupendi kazi kubwa iliyofanywa na waasisi wa taifa letu kujenga misingi ya amani na utulivu ije ibomolewe kwa sababu ya watu kutaka uongozi kwa lazima. CCM chama changu, kama wana mipango hiyo basi watakuwa wamepotoka kupita kiasi. Mungu alinusuru taifa letu na mabaya ya aina hiyo.