Losomich
JF-Expert Member
- Nov 9, 2011
- 371
- 71
Kwa mtazamo wa jumla, kwa hali ilivyo hapa kwetu Tanzania tunahitaji wanaharakati wajasiri wenye nia ya dhati ya kuikomboa taifa letu kama huyu mheshimiwa Lema. Huyu mwanaharakati ameonyesha njia. Mheshimiwa ameutuma ujumbe kwa ulimwengu kuwa ukombozi sio lelema. Ni lazima mtu ujikane nafsi yako na kuubeba furushi kubwa usio kadirika ambamo ndani yake umejaa kuonewa, kudhihakiwa, kudhalilishwa, kejeli za kipuuzi, kuzingizwa, kutukanwa, makesi ya kubambikiziwa, kupigwa mabomu ya kutoa machozi, kumwagiwa maji ya tindi kali n,k. Lakini mwisho wa yote kwa mzaada wa nguvu ya umma hilo furushi kubwa la hayo yote litatupwa kwenye shimo kubwa ya hewa ambapo litasahaulika milele. Mwenye haki ataishi kwa imani bali asiye haki ataisha kwa mashaka siku zote. Mheshimiwa lema tuko pamoja mpaka ukamilifu wa dahari!!!