Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Yaani kwa haya mawazo yako unayomwaga hapa hivi kweli ni kwa mtu aliyejipenyeza katika mkutanao wa siku ya vyuo vikuu, na isitoshe ni mdau mwenye elimu ya Chuo unatoa hizi pumba hapa? Tena huna aibu kusema siku ya vyuo vikuu, ukimaanisha na wewe ulikua mdau?Majuzi tumepokea salamu za mshikamano kwenye kongamano la wanafunzi lililoitishwa na CHADEMA kutoka kwa mtu anayejiita M.M. Mwanakijiji. Lakini hatukuambiwa kwamba huyu bwana ni nani na ametuma hizi salamu kama nani. Je, iweje chama cha siasa kiruhusu mtu ambaye wameshindwa kumtambulisha alete salamu za mshikamano. Kwenye hizo salamu za MM Mwanakijiji anawahamasisha wanafunzi waafanye uasi, wagome na mambo mengineyo. Sasa hivi hao wanafunzi ni mafala kiasi gani kwa kupokea ujumbe bubu, ambao aliyeuandika ni kunguru asiyejitambulisha?
Hata kama aliwachochea kugoma, hakuna mbaya kwani dawa ya serikali dhalimu ni nini? Hata mimi nilichelewesha tu salamu zangu, nilitaka nizitume niwahamasishe vijana juu ya umuhimu wa kufanya yale ya BOLIVIA, INDONESIA nk.
Muda uliobaki ni mchache sana, tutafanikiwa tu.
Halafu siku nyingine ukipost hapa usome kabla hujapost ndugu yangu, kwa nini ujikosee heshima namna hiyo?
Mdau wa Chuo Kikuu? Hata common sense ni za muhimu sana.